Azam Tv kutoonyesha Michuano ya Afcon 2022

Azam Tv kutoonyesha Michuano ya Afcon 2022

Status
Not open for further replies.
Sawa lakini azam kama anashindwa kuonesha uefa walau afcon alitakiwa aoneshe yaani aweke mzigo apate haki za matangazo
Hela inayotolewa na Multichoice kuonesha EPL, UEFA, EUROPA ni kubwa kuliko utajiri Cash wa Azam.
 
Na tulio na ving'amuzi tumenunua kwa ajili ya ligi kuu,kwa style hii DSTV wataendelea kutukimbiza kwa vifurushi ,huwezi kuamini bongo tu vifurushi vya dstv ndo ghali Ila kwa nchi zingine bei kama za Azam tu
Siku wakifikisha subscribers 500K na wakapewa FTA watashusha bei
 
Usilazimishe kila mtu ajue uchoko wako, nimesema bei ya ving'amuzi hayo ya vifurushi uyaseme wewe bila kuniquote, dstv hadi anafikiria kufunga oparesheni zake tz kwa taarifa yako, ving'amuzi anauza 59000 bado wateja shida maana hawamudu malipo ya mwezi sasa kama mteja hamudu malipo ya mwezi dstv atapona vipi?
Hiyo ya kufunga HUO NI UMBEA NA UONGO WADANGANYE WASIO IJUA DSTV....NA PIA KAMA WEWE HUWEZ LIPIA HILO NI TATIZO LAKO...
UKWELI UTABAKI PALE PALE DSTV IKO VIZURI..na watu wananunua ving'amuzi na wanaendelea kuenjoy soka mubashara
 
Usilazimishe kila mtu ajue uchoko wako, nimesema bei ya ving'amuzi hayo ya vifurushi uyaseme wewe bila kuniquote, dstv hadi anafikiria kufunga oparesheni zake tz kwa taarifa yako, ving'amuzi anauza 59000 bado wateja shida maana hawamudu malipo ya mwezi sasa kama mteja hamudu malipo ya mwezi dstv atapona vipi?
Punguza uongo DStv bado yupo sana bongo
 
Kuna tetesi kuwa AzamTv hawana haki ya kuonyesha michuano ya Afcon 2022 itakyofanyika mapema mwakani!

Kama ni kweli basi, AzamTv watakuwa wamefeli pakubwa sana, maana wanashindwa kuonesha michuano mikubwa na yenye mvuto na hii inapelekea kuwashushia uweledi!
Azam hawajawahi kupata hiyo haki na hawewezi kwa kuwa huwa zinatolewa kwa Tv za Taifa husika, ndio maana wanarusha kupitia TVZ.

Vv
 
Na dstv wanakimbiza nchi nyingine tu ila kwa bongo wanapumulia mashine wana hali mbaya balaa, imefikia hatua azam anamzidi mara mbili bei ya king'amuzi
Sio kweli DStv wajanja kibiashara, wanashusha bei ya dishi wanakubana kwenye kulipia king'amuzi, ni kama walivyofanya makampuni ya simu, kutoa line bure wanakubana kwenye vocha na vifurushi
 
Sio kweli DStv wajanja kibiashara, wanashusha bei ya dishi wanakubana kwenye kulipia king'amuzi, ni kama walivyofanya makampuni ya simu, kutoa line bure wanakubana kwenye vocha na vifurushi
Sasa wanakubana vipi ikiwa unaweza kuweka ndani na usilipie?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom