Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,496
Kuna matangazo ya makampuni mbalimbali wakati wa mechi.1.data Za Tcra kuna Madishi 1.1m Tanzania nzima, hapa Angalia
Watumiaji wa ving’amuzi wapungua kwa asilimia 3.2 Tanzania - Nukta Habari
Tangu mwaka 2014, idadi ya watumiaji wa ving’amuzi imekuwa ukiongezeka kila mwaka hadi kufikia mwaka 2018 kabla haijapungua hadi milioni 2.68 mwaka uliofuata.nukta.co.tz
Ni data za mwaka uliopita, hio 1.1m ni wote DSTV, Zuku, Azam na wengineo.
Hivyo kuna uwezekano Azam hana 1m monthly subscribers.
2. Kama Data zako zipo sahihi anapata 80B kwa mwaka still kutoa 22B kudhamini ligi ni kubwa sana Kibiashara.
-Uganda azam analipa around 4B tsh
-kenya kila timu wanapewa ksh 10m ambayo ni around milioni 200 tsh.
Kwa East Africa hakuna anaepata kama sisi.
Si hivyo tu, hata ukiangalia makampuni ya Kimataifa dstv analipa epl around 200m akiwa na Pato la around 2B kwa mwaka ambayo roughly ni kama 10% ya Pato lake.
Hio 22B ni ligi Ya Tanzania tu, bado analipa Ligi za nje, chanel za kulipia kama za Kihindi, movies na series wanazo tafsiri etc.
3. Naunga hoja wanaohoji miaka 10 wana point, Kwa muono wangu hili deal linamungizia Hasara Azam kwa short term, no way Ligi yetu iwe na thamani hii.
DSTV analipa around Bilioni 500 kwa nchi takriban 46 za kusini mwa jangwa la sahara hii ni around 10B kwa kila Nchi. Kwamba ligi ya Tanzania ina thamani kuliko Epl?
Inaonekana Azam wame project kwa miaka 10 baadae Ligi yetu inaweza kuwa na thamani zaidi ya hii, hivyo mapema tu wamejipanga na kununua kabisa.
Ama kuna faida nyengine wa napata Toka serikalini kama Ruzuku.
Inampunguzia gharama za kuendesha.