Kwa wale wanaoona ni pesa ndogo watuoshe macho kimahesabu
Mkuu umetumia busara sana kuhitaji arguments za sisi tunaoona pesa ni ndogo...Iko hivi
1. Umewahi kujiuliza ni vibanda umiza vingapi, watanzania wangapi na lounge au lodge ngapi zinazolipia kile kifurushi ili tu kuangalia mpira (hapa naongelea active customers)..achana na channel zingine.
Mfano, tuweke makadirio ya chini..wenye ving'amuzi nchi nzima ni Milioni moja...na tuweke makadirio ya chini tu kuwa kifurushi kwa mwezi ni elfu kumi.
so, mapato kwa mwezi 1 tu ni 1,000,000 * 10,000 = 10,000,000,000 (bilion 10) ambayo ni sawa na Bilion 80 kwa mwaka (nimepiga mahesabu tu ya ile miezi 8 ambayo ligi inakuwa active)..Hapo sijaongelea wateja wapya wanaonunua ving'amuzi vyao kwasababu tu ili waone mechi za vpl.
Kumbuka hapo bei halisi sio 10k (kwa sasa ni 20k) na wateja wanaohitaji kuangalia mechi ni zaidi ya 1m...Hapa lets assume ile gharama nyingine ya king'amuzi na idadi ya nyongeza ya wateja (10,000 * 500,000 = 5b kwa mwezi), mapato yao yatatumika kwenye kucover costs of operations..
2. Channel zao zinazoonesha mechi zitapata matangazo ya wadhamini wengi sana...kama ambavyo hawa wauza solar wanatangaza kwenye hizi channel...
3. Miaka 10 ni muda mrefu sana, ndani ya huo muda usitegemee gharama ya kulipia vifurushi itabaki constant (20k per month).. Kuna expectation kubwa kuwa itapanda maana demand ya service inaongezeka...hapo faida itakuwa maradufu.
Risk pekee kwa azam ni endapo majanga kama haya ya covid yatatokea (siombei yatokee).
Wengine wataongezea.