Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Katika kugawana pesa team zote hapa ndio TFF walitakiwa waweke wazi ili kuzisaidia team zote. Nadhani wangeiga mfumo wa EPL japo sio kila kitu ila wangechukuwa mfumo huo kwa maana kila aliye kwenye VPL haijalishi nafasi ya ngapi kuna kiasi unapewa halafu ziada inategemea kama game yako itakuwa live au game itakayokuwa inatizamwa na watu wengi unapata zaidi ukiondoa na zawadi ya wa kwanza mpaka wa 4 hii italeta ushindani mkubwa na kuzisaidia team ndogo kuweza kulipa vizuri wachezaji wao. TFF na Board ya league wanatakiwa waweke wazi pesa hizi zitanufaisha vipi team kwa ujumla na mgao utakuwa namna gani. Maana 22 Billion kwa mwaka sio pesa ndogo na kuna wadhamini wengine wadogo watasaidia ili ukiviwezesha vilabu ndio league inakuwa bora na thamani yake itapanda ila yakija yake magumashi tena mnagawa 10 billion tu zingine matumizi ya kawaida hapo vilabu visikubali kabisa team za VPL zipate mgao mkubwa na pesa kidogo sana ziende kuendesha au kusaidia TFF sio tena pesa ya VPL inaenda team ya Taifa hii haihusu, pesa ya VPL iwe kama kampuni team za VPL wawe ndio wanahisa tu copy mfumo wa EPL ndio maana team ya mwisho EPL unaweza kukuta wanapesa kuliko team ya 4 La liga. Team zikiwa na pesa zita invest pia huku chini kwa wachezaji wadogo baada ya miaka 10 unakuta team kama Mbeya city wanaweza kuleta wachezaji wazuri. Kitu kimoja team za jeshi hapana kama jeshi wawe na team moja tu hakuna sijui JKT Ruvu, Ruvu shooting, Prison, Police sijui nini Orjoro hapana hawa wanaturudisha nyuma.
Hiki ndio nimekipenda, azam anafanya kaz nzuri ya kuleta thamani ya timu na league
 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Azam TV Limited kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10 wenye thamani ya Shilingi bilioni 225.6.

Kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea Afrika Mashariki na kuifanya thamani ya soka ya Tanzania kuongezeka.

BINGWA WA VPL kwa misimu mitatu ijayo, atapata TSH MIL 500 kama 'Bonus' kutoka Azam TV

Pia
Mshindi 2: Tsh Mil 250
Mshindi 3: Tsh Mil 225
Mshindi 4: Tsh Mil 200

Meko aliiba Trilioni moja.
 
Hii football industry ni kubwa Sana na vilabu kila kukicha wanalia juu ya Gharama za uendeshaji zipo juu Sana .
Sasa kwa Watu wa Taaluma ya Uchumi na Fedha wanaelewa ...
Hizi 225/225/200. Sawa na Chumvi Baharini🥱
 
TFF na Bodi ya Ligi wameingizwa choo cha kike, huwezi kuingia mkataba muda mrefu namna hiyo lakini kitu kingine sidhani kama walipokuwa wanatangaza tenda walitangaza utakuwa mkataba wa miaka 10. Ilitakiwa angalau uwe mkataba wa miaka mitano ili kusudi wanapotaka kungia mkataba mwingine wafanye evaluation ya mkataba uliopita.
Pia nimeona vilabu ambao ni wanufaika watapata asilimia 67 na vilabu vinachekelea bila kuangalia vilabu ndio vinabeba gharama kubwa kuliko wadau wengine.
Watoe uwaingize choo cha kiume, ukute huna hata 40,000 kwenye account kama balance afu unapayuka hapa
 
Data nyengine hizi, hii mechi baina ya Ruvu shooting na Prison iliingiza kiingilio 245,000 mechi nzima, then watu wanakwambia Bilioni 22 ni ndogo

Kwenye mgawanyo Prison wa kapata 32,000 [emoji23], serious dah.

Azam anatoa tu sadaka.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wapuuzi hao wanapayuka tuu hata biashara ya vocha hawana na kama wanazo hawajielewi
 
Hii football industry ni kubwa Sana na vilabu kila kukicha wanalia juu ya Gharama za uendeshaji zipo juu Sana .
Sasa kwa Watu wa Taaluma ya Uchumi na Fedha wanaelewa ...
Hizi 225/225/200. Sawa na Chumvi Baharini🥱
Biashara haiendi hivi aisee, matatizo ya pesa hayamhusu Azam, kesho simba wakikopa Hela alipe Azam? Kesho kutwa Yanga wakisajili alipe Azam?

Wewe unachotakiwa kuleta ushahidi hapa ni kiasi gani azam anaingiza kupitia hio ligi.
 
Yaani bongo population ni kubwa lakini hamna biashara za ushindani yaani unashangaa hadi media kubwa hazina matangazo yakuwafanya waendeshe vituo vyao kwa faida kubwa na kwa ubora..wanafika kujilizaliza kuomba matangazo.

Hakuna stiff competition kabisa.
Chama lenu la maccm limefukarisha watu unajifanya hujui? Hujui kwamba licha ya watu wengi kumiliki simu Takwimu za matumizi ya salio utashangaa.

Au nenda bank ukaokote vile vi bank statement utakuta salio kwa wengi hawazidi 200,000
 
Na watumizi wanazidi kila mwaka...TFF Wangesign mikataba ya miaka isizidi 3 ili wapate muda wa kupitia mafanikio ya mkataba mara kwa mara.

Hii ina maaana wapo marais wa TFF ambao hawatakuwa na uwezo wa kurekebisha mikataba hiyo hata kama wataona mapungufu

Ni mpuuzi pekee atakubali kuwekeza pesa yake nyingi hivyo halafu angie mkataba wa miaka 3.

Kurusha matangazo ya mpira ni gharama kubwa sana, kuwa na facities pekee na uendeshaji wake sio fedha ndogo.
 
Kwa nature ya hii biashara (Haki za kuonesha mpira) ilivyo ni ngumu sana investors wawili kuexist kwa pamoja..Lazima mmoja afe..kwasababu

Market bado ni dogo sana kuhitaji two suppliers...Gharama za kuendesha biashara zinakuwa juu kuliko faida mtakayogawana..chukulia mfano kwenye soko la ving'amuzi tu..kuna kampuni zingine naamini zinapata faida ndogo sana au inawezekana zinapata loss kwasababu tayari soko ni dogo halitoshi watu wawili..Kuna aina za ving'amuzi huwa nazisikia tu redioni ila hadi leo sijawahi kuviona vinatumika majumbani..vipo ila wateja ni wachache sana.

sasa Ukimuweka AZAM na DSTV kwa ligi moja ya bongo na ambayo market 99.5% ipo bongo lazima wagawane faida na mmoja lazima aanguke maana cost of production ni kubwa kuliko market share.

Najua utakuwa unajiuliza kwanini kuna TIGO, VODA, AIRTEL, HALOTEL, ZANTEL n.k at the same time na wote wanapata faida...Jibu ni rahisi tu kuwa market ni kubwa (zaidi ya watu 30m wanatumia simu) na unakuta mtu mmoja anamiliki line zote...ila watu wanaomiliki ving'amuzi viwili kwa pamoja ni wachache sana kutokana na per capital income za raia.

So, kwa hii biashara ya kuonesha mpira wa ligi ya bongo (taking into consideration the current situation) ni ngumu sana sana sana DSTV na AZAM kuonesha kwa pamoja...Kwanza kati yao hakuna atakaekubali...Kitu pekee ambacho watakubali kufanya ni kugombania tender tu ila sio kuonesha kwa pamoja..

Ndio maana watu wanalalamika miaka 10 ni mingi sana ilibidi iwe michache ili kutoa nafasi kwa bidders kugombania tenda na TFF pamoja na vilabu kuzidi kupata masilahi mazuri. Hii ya mtu mmoja kumiliki soko kwa 10yrs inaua ubunifu.

swali fikirishi kidogo kwako mkuu:

Yule MO kama mjasiriamali, unadhani hajaiona fursa kwenye kuonesha soka?, unadhani anashindwa kuanzisha channel yake ili aoneshe?..Anaweza 100% ila tatizo soko automatically haliruhusu more than one supplier/producer...

Otherwise angekuwa tayari kuanzisha TV ili agombee tender lakini ndo hivo miaka 10 inabidi abaki na idea + ubunifu kichwani.....TFF wamefeli sana.
Miaka 10 mingi sana ingetakiwa iwe mkataba wa miaka 3 tenda ikatangazwa tena...yawezekana akaja mwekezaji akaweka Bil 32 mezan kwa mwaka......lakini huu ujinga wa kupiga msumari miaka 10 haufai....

Hata aje nani TFF atake kufanya mabadiliko yenye tija kwenye mkataba huo hawezi
 
Yanga na Simba ni Zaidi ya Fedha sasa tusipo yasema haya mapema tutaacha picha mbaya kwa vizazi vijacho[emoji736]
 
Miaka 10 mingi sana ingetakiwa iwe mkataba wa miaka 3 tenda ikatangazwa tena...yawezekana akaja mwekezaji akaweka Bil 32 mezan kwa mwaka......lakini huu ujinga wa kupiga msumari miaka 10 haufai....

Hata aje nani TFF atake kufanya mabadiliko yenye tija kwenye mkataba huo hawezi
Merchant za klabu Pekee kwa Yanga na Simba Tayari ni Pesa kubwa Sana..
Angalia Simba Day.....
Mwananchi Day .........
Viingilio + Mauzo ya Product zao + Wauze haki yakuonyesha tu hizi Tamasha kwa Tv wanazo zitaka watapa Fedha kiasi Gani.??
 
Hivi Leo hii TFF INASHINDWA KUWA NA FACILITY ZA UKWELI KAMA UWANJA NA OFISI YENYE HADHI KAMA FEDERATION[emoji15][emoji15]
 
Hivi leo tumeshuhudia, TFF na AZAM wakiingia mkataba mnono wa kuonyesha ligi kwa kipindi cha miaka 10.

unaonekana ni mkataba mnono sana, lakini mimi kama mdau umeniacha kwenye maswali mengi sana, kwanini ni mkataba wa miaka 10? Miaka 10 ni mingi sana katika soko huria.

Inamaana hakuna washindani ambao wangeweka dongo nono zaidi mbele? au thamani ya ligi itabaki kama ilivyo kwa kipindi chote?

na hata kama hakuna washindani je wanauhakika gani ndani ya muda huo hakutakuwa na mshindani mwingine?

Binafsi naamini pamoja na unono wa kitita kilichotolewa na Azam lakini miaka 10 ni mingi sana hasa kwenye soko huria na kwenye maendeleo ya sayansi na teknologia.
 
Kwa jinsi waTz tulivyo hata Azam angeweka Trillion Bado wangelaumiwa, Naamini Kuna hasara nyingi tu Azam pia anazipata
Mihimu tu appreciate alichokitoa Azam

Baadhi ya mikoa anatumia huduma za mashirika mengine kurusha matangazo mfano uwanja wa Gwambina azam anatumia TCCL Kurusha matangazo ya mpirs ambapo wanalipa si chini ya 40m kwa game moja.
 
Back
Top Bottom