Kwa nature ya hii biashara (Haki za kuonesha mpira) ilivyo ni ngumu sana investors wawili kuexist kwa pamoja..Lazima mmoja afe..kwasababu
Market bado ni dogo sana kuhitaji two suppliers...Gharama za kuendesha biashara zinakuwa juu kuliko faida mtakayogawana..chukulia mfano kwenye soko la ving'amuzi tu..kuna kampuni zingine naamini zinapata faida ndogo sana au inawezekana zinapata loss kwasababu tayari soko ni dogo halitoshi watu wawili..Kuna aina za ving'amuzi huwa nazisikia tu redioni ila hadi leo sijawahi kuviona vinatumika majumbani..vipo ila wateja ni wachache sana.
sasa Ukimuweka AZAM na DSTV kwa ligi moja ya bongo na ambayo market 99.5% ipo bongo lazima wagawane faida na mmoja lazima aanguke maana cost of production ni kubwa kuliko market share.
Najua utakuwa unajiuliza kwanini kuna TIGO, VODA, AIRTEL, HALOTEL, ZANTEL n.k at the same time na wote wanapata faida...Jibu ni rahisi tu kuwa market ni kubwa (zaidi ya watu 30m wanatumia simu) na unakuta mtu mmoja anamiliki line zote...ila watu wanaomiliki ving'amuzi viwili kwa pamoja ni wachache sana kutokana na per capital income za raia.
So, kwa hii biashara ya kuonesha mpira wa ligi ya bongo (taking into consideration the current situation) ni ngumu sana sana sana DSTV na AZAM kuonesha kwa pamoja...Kwanza kati yao hakuna atakaekubali...Kitu pekee ambacho watakubali kufanya ni kugombania tender tu ila sio kuonesha kwa pamoja..
Ndio maana watu wanalalamika miaka 10 ni mingi sana ilibidi iwe michache ili kutoa nafasi kwa bidders kugombania tenda na TFF pamoja na vilabu kuzidi kupata masilahi mazuri. Hii ya mtu mmoja kumiliki soko kwa 10yrs inaua ubunifu.
swali fikirishi kidogo kwako mkuu:
Yule MO kama mjasiriamali, unadhani hajaiona fursa kwenye kuonesha soka?, unadhani anashindwa kuanzisha channel yake ili aoneshe?..Anaweza 100% ila tatizo soko automatically haliruhusu more than one supplier/producer...
Otherwise angekuwa tayari kuanzisha TV ili agombee tender lakini ndo hivo miaka 10 inabidi abaki na idea + ubunifu kichwani.....TFF wamefeli sana.