Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
Mpira ni ukezaji sio laziama utegemee za mdhamini watu wawekeze kwenye mpira
Upo sahihi ila watu tunajudge hiyo miaka 10 na ukizingatia kila siku bidhaa hiyo inaongezeka thamani pamoja na gharama za uendeshaji kwa vilabu, nafikiri wengi mnakimbilia kuangalia bonus kwa bingwa atapata nini na anaemfuatia na kwa mbaali yule mshindi wa tatu ambavyo bila shaka katika kipindi hicho cha miaka 10 timu 3 ambazo wote tunazifahamu uenda zikabadilishana tu nafasi hizo hizo karibia miaka 9 hivi kama sio miaka yote.
Vipi kwa zile timu zingine ndogo katika Ligi Kuu ambapo sio ajabu pesa hizo watakazo gaiwiwa ndo wakawa wanaingiza kama chanzo chao kikubwa cha mapato ukilinganisha na udhamini mwingine watakao kuwa nao kwasababu hizi timu zinakuwaga na wadhamini wachache ambao pia wanawapa dau kidogo au mara nyingine wanakosa kabisa wadhamini ukilinganisha na hao wakubwa?!
Ambao sio ajabu ukakuta kiasi cha pesa watakachopata plus na bonus hizo ukikiweka kwenye mzani unaweza kuta thamani yake inashika nafasi ya 3 na kuendelea katika chanzo cha mapato klabuni.