Bujibuji umenena Sawa bin Sawa. AMRI KUU NI UPENDO. Soma hapa...
Urafiki Wa Wakristo
Maelezo yanaanzia na Aya 82 iliyokuwa mwisho wa juzuu ya sita, kwa vile inaungana hapa.
Maana
Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu wengine kwa walioamini nimayahudi na washirikina.
Yaani mayahudi na washirikina ndio waliokuwa maadui zaidi kwa Waislamu. Mara nyingi watu wameitolea ushahidi Aya hii, kuwa dini ya kikristo iko karibu zaidi na Uislam kuliko dini ya kiyahudi. Hilo ni kosa ikiwa inakusudiwa dini ya kiyahudi na ya kikristo kabla ya kugeuzwa. Kwa sababu dini kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake ni moja tu kwa upande wa itikadi na msingi yake. Na kama ikikusudia baada ya kubadilishwa, basi zote mbili ni sawa (Ukristo na Uyahudi) hakuna yenye afad- hali.
Usahihi ni kuwa uhasama wa mayahudi na washirikina katika Uislam una- tokana na mgongano baina ya mwito wa kiislam na tabia iliyokuwa imeshi- ka kasi katika Bara arabu mwanzo wa utume. Tabia hiyo ilikua ni mashindano ya kupora mali na watumwa. Vilevile riba, ghushi na mengineyo ya kutumia nguvu na utapeli. Tabia hii iliambukiza wafanyibiashara wa kigeni, kama walivyoambukizwa viongozi wa kiyahudi waliokuwa wakimiliki viwanda na biashara ya ndani.