#COVID19 Azim Dewji amvaa Gwajima sakata la chanjo, amwambia ana akili ya kuhubiri siyo Sayansi

Kama wao hiyo johnson & jonosn wameikataa leo wewe ndo unaiona ni bora!!!! Kwa maabara gani ulizonazo acheni kujitoa ufahamu
 
Btw huyo mfadhili wa zamani wa Simba sikuwa namsikia tena kwa kipindi kirefu, lakini kipindi hiki kaibuka nae..... ngoja tuonesie watazamaji aiseee.......kaazi kwelikweli.
Chimeumana 😂😂😂😂!
 
Gwajima anapaswa kujibiwa kwa hoja

1) Anataka tuambiwe ni daktari yupi Tanzania amefanya thorough analysis ya kilichomo kwenye hiyo chanjo?

2) Tuambiwe chemical composition ya contents za hizo vaccine

3) Tuambiwe kama kuna/hakuna potetial side effects za hiyo vaccine leo, kesho, 30 years later

4) Tuambiwe chanjo wanayopewa wamarekani ndiyo hiyohiyo tunatakiwa kupewa sisi? Kwa mfano, kwanini tumepewa Johnson & Johnson wakati wao wanatumia zaidi AstraZeneca?!

Naona wengi wanatukana tu na kusema eti “ amuheshinu Rais na mwenyekiti”. Akili za kitumwa hizi.
 
Mbunge "ana" au "hana"?
 
Watanzania wengi ni vilaza, Inamaana wameshindwa kabisa kujibu hoja za Gwajima na badala yake wanamtusi na kufosi bila kutia majibu ya maswali yake

Bahati nzuri kasema vita hii ataipiga hata akibaki peke yake
 
hivi hawa wahindi wamezaliwa hapa, wameishi hadi wamezeeka lakini hawajui kiswahili vizuri huwa sababu yake nini, au wanajifanyisha?
 
Hao uliowataja wote siwezi kuwaamin,wakat wa jiwe walituambia corona hakuna,na pia wakatusihi tupige nyungu kwasana,Leo wanatuambia NINI?
 
Umeandika kwa hisia kali sana, wakijibu haya maswali itapendeza!!
 
wana standard zao na viwango vyao ambavyo ni tofauti na sisi yaani una pesa ya kuinunua kumbuka ni dunia ya kwanza vs dunia ya tatu acha kutumia nguvu nyingi sana kwa jambo ambalo ni dhahiri kabisa,kumbuka tu kuwa mzungu angekuwa anahitaji hilo la kuiangamiza Africa wala asingesubiri covid na asingefanya hadharani kama picha zako zinavyomaanisha.Na ndio maana hata dawa za ukimwi hizi zinazoletwa africa unadhani ndizo wanazotumia US au CANADA au EU ni tofauti kabisa.(standards)
 
Yeye Azim Dewji ni Mwanasayansi?

 
Wewe nenda kachanje chanjo hakuna aliekuzuia na wale ambao hawatataka kuchanjwa acha waendelee kukataa, swala la watu kumsikiliza Gwajima na kukataa kuchanjwa lipo ndani ya utashi wao hivyo usiwapangie.

Kwani sio nyinyi mnaodai freedom of speech kila siku humu?
 
Mkuu kwani Gwajima kakukingia bunduki Ili isiende kuchanjwa? Wewe nenda kachanjwe wale wasiotaka kuchanjwa baada ya kuskiliza Gwajima achana nao Ili kama ni kufa kwa COVID-19, basi wafe.

Kachanjwe mkuu.
 
mkuu uhuru usio na mipaka si rahisi ila la msingi asingeamua kumtumikia Mungu na Kaisari kwa wakati mmoja haijarishi yuko wapi yeye ni Mbunge wa ccm achunge ulimi wake hayo maneno aliyoyasema sio sawa,ni muda tu ila anaweza kuitwa kuhojiwa na wenye chama.
 
Huko nyuma tuliambiwa tusichanganye dini na siasa, lakini sasa ndiyo ninajua huo msemo ulikuwa na maana gani. Ikiwa itaonekana alichokisema ni kosa na chama chake basi hata wakimwita itakuwa ni sawa tu kwani hayo ndiyo matunda yao wenyewe waliyoyavuna katika uchaguzi uliyopita.
Removing of force from oppositions creates opposition force from within.
 
Dikteta Mwendazake ndio amesababisha Nchi imekuwa na watu wapuuzi na wahuni kama Gwajima Ku address Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…