Boss, ukizungumzia wataalamu na nchi yetu, basi sahau kabisa kuhusu huo utalaamu wenyewe.
Sisi tuzungumzie 10% na upigaji usio na aibu, dhuluma na husda, uzandiki na unafiki, umelo na ulafi, majivuno na majigambo, ubabe na uhafidhina, uzuzu na umbumbumbu na yote yafananayo na tunayofanya.
Utaalamu? Upi? Sayansi? Ipi? Angalau tunao uwezo kwa kukariri na kukumbuka historia ya sayansi, kubeba ya watu kichwani na kufanya ni yetu!
Huna utaratibu maalum wa kupima watu, huna takwimu zozote za jambo hili, unasema kuna wagonjwa 680 wa covid-19! Sina hakika kama wenzetu wanazungumzia mamia tena, ina maana hatukua na rekodi kabla, sio? Wangapi wamekufa kwa covid-19 mpaka sasa? Wangapi wamepona? Wangapi wako ICU, tupe taarifa hata ya kupika tu ili tujue tuko wapi!
Imeundwa kamati, miezi 4 mbele unaliambia taifa kwa kusisitiza, mimi ni waziri wenu, hali ni mbaya! Kuna siri gani ya kutosema kwa namba ubaya wa hali hiyo? Kama chanjo zishafika, nini kingine tunaogopa? Kama ni JPM, hayupo tena, kigugumizi kinatoka wapi?
Ubavu wa kutoa matokeo ya kusema wewe ni COVID-19 positive huna, kwamba usipopewa cheti wewe ni mgonjwa au eti unatoa majibu NOT NEGATIVE, mtu huyo akirudia ndani ya siku 5 bila kinga wala isolation unampa cheti kuwa NEGATIVE, na bado unataka tuamini kuwa unajua unachokifanya? Unipime kwa takribani sh 400,000, ambapo dola 100 za serikali na pesa kadhaa za kituo, halafu unipe chanjo bure? Na bado zikipita saa 72 cheti ni invalid, biashara iliyoje hii.
Huruhusiwi kupanda daladala bila barakoa na yote waliotangaza, ila kundi la wanafunzi shuleni wanaokaa 90 kwa chumba kimoja cha darasa hawajazungumzwa itakuaje! Barakoa zibadilishwe kila baada ya saa 4, sijui kama kule Nanjilinji wataweza. Wataalamu walioshindwa kuthibitisha kama barakoa tulizonazo, ama za vitambaa au zile za hospitali kama zinaweza kuzuia mdudu kupita! Vyuoni huko wanaweza kukaa mita 1 apart?
Nchi ina wagonjwa wangapi wa njaa? Malaria? Watuambie hapa kwetu, ni ugonjwa gani uko kwa wingi na unaongoza kwa kuua, ili tujue tahadhari zaidi zielekezwe wapi!
Tumepitisha bajeti juzi, tumesema tunaongeza tozo kujenga barabara na zahanati, kama tungejali sana, tungetenga fedha za kununua hivyo vifaa vya kusaidia upumuaji na kuongeza ICU facilities kwa dharura, mpaka sasa tumeongeza ngapi? Uliza wakurugenzi wangapi wanapewa pesa za magari mapya kama yamekosekana kabisa ya kuwabeba! Majumba mangapi ya ma RC na DCs yanajengwa/karabatiwa kwa mafedha chungu mzima kwa mujibu wa bajeti, lakini tuna uhaba wa mashine za kusapoti upumuaji?
Jokate anaweka taa mbele ya ofisi yake kwa mamilioni ya fedha, Temeke hospitali tuna mitungi mingapi ya gesi ikitokea kweli kitu kimelipuka?
Sipingi chochote mkuu ILA najaribu kuomba kama kweli kuna dharula, basi tufanye vitu umuhimu wa dharula hiyo na sio hata wasio na mamlaka ya kusema wanasema tu.