Azim Dewji: Iran walitusaidia, ni muda wa kuwaunga mkono

Azim Dewji: Iran walitusaidia, ni muda wa kuwaunga mkono

Mfanyabiashara Azim Dewji amesema Iran imewahi kuisaidia Tanzania katika nyakati ngumu, ikiwemo msaada wa meli mbili za mafuta miaka ya 70 wakati wa uhaba mkubwa.

Amesisitiza kuwa urafiki wa kweli huonekana wakati wa shida, hivyo Tanzania ina sababu ya kuonyesha mshikamano kwa Iran katika kipindi hiki wanachokipitia.

Hivi huyu makalio anaongea nini? Nchi nyingi hata za kiarabu hasa Kuwait, Saudi Arabia na UAE walitusaidia sana, kwa hiyo tupeleke watanzania wengine waende Ghuba na wengine waende Iran....Kwa sababu walitusaidia. Sikubaliani na Marekani na Israel siwakubali kabisa lakini tuangalie na tujiepushe na maneno ya kijinga kijinga kama nchi, la sivyo tutakuwa kama General fake....Muhoozi Kainerugaba, huyu akilewa anaongea utumbo hasa.
 
Tanzania ni nchi isiyofungamana na taifa lolote lile.
Tukokotoe thamani ya misaada kutoka pande hizo mbili halafu tuchague wa kuungana naye.

NB:Lengo kwa sasa liwe vita kusitishwa,mkeka ujao wese ni 5K/litre na kupatikana ni kwa mbinde.
 
Kipindi hicho uongozi wa irani ulikuwa chini ya Ayatolla?
Ndio baada ya vita na uganda Tz ilikuwa na uhaba mkubwa wa mafuta hadi sheria ikapitishwa magari ya serikali yasiwe yanatumika au limit ya kutumika..

Ndipo nyerere alimtuma sabodo kwenda kwa ayatollah kuomba ndipo mafuta yakaletwa na ubalozi ukafunguliwa wa iran TZ
 
Mfanyabiashara Azim Dewji amesema Iran imewahi kuisaidia Tanzania katika nyakati ngumu, ikiwemo msaada wa meli mbili za mafuta miaka ya 70 wakati wa uhaba mkubwa.

Amesisitiza kuwa urafiki wa kweli huonekana wakati wa shida, hivyo Tanzania ina sababu ya kuonyesha mshikamano kwa Iran katika kipindi hiki wanachokipitia.


Azim Dewji mmoja wa vigogo wa jumuiya ya Mashia Tanzania anafikiria kutumie ushawishi wa Jumuiya ya Mashia, ili Tanzania iende kichwa kichwa kuingua mkono Iran bila kuwaza madhara yake makubwa

Diplomasia laini ( Soft Diplomacy) lazima ufikiri nje ya imani la sivyo nchi zote kubwa Marekani n.k pia mataifa ya Qatar, UAE, Saudia, Kuwait zinazoikataa Iran chini ya maAyatollah zinaweza kuiwekea vikwazo Tanzania

TOKA MAKTABA :

Dar es Salaam, Tanzania

WATANZANIA DHEHEBU LA SHIA WAOMBOLEZA KIFO CHA ALI KHAMENEI

View: https://m.youtube.com/shorts/LI9tOXUTewc


Kwa undani :

Toka maktaba:

Simulizi za Mjukuu wa Mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga wa maeneo ya Wamachinga Pwani aliyekuwa na mguso mpana kuendeleza madhehebu ya Shia
Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 

27 March 2026​

Mantashe - 'Mizigo inayoelekea Afrika ya Kusini kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz haipati usumbufu '​


Mantashe - Kutokuwa marafiki na waMarekani na Israel kumetuponya kutopata dhahma kutoka Iran​


Mantasheg.sg

Picha ya skrini: Habari za gazeti la Mwananchi la Afrika ya Kusini

Waziri wa Madini na Petroli wa Afrika Kusini Gwede Mantashe amewasihi Waafrika Kusini wasiwe na hofu kuhusu uhaba wa mafuta unaowezekana, akisema meli zinazobeba mizigo na vifaa vinavyoelekea Afrika Kusini zinapita katika Mlango-Bahari wa Hormuz bila usumbufu au vitisho vya mashambulizi kutoka Iran.

Mantashe alikuwa akijibu maswali katika Bunge la Kitaifa Jumatano huku Waafrika Kusini wakiendelea kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu uhaba wa mafuta na ongezeko kubwa la bei ya mafuta, ambalo linatarajiwa kuanza wiki ijayo.

Ugavi wa mafuta

Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimeibua hofu duniani, huku mzozo huo ukitarajiwa kuathiri pakubwa bei ya mafuta na usambazaji.

Wakati wa kikao katika Bunge la Kitaifa, Mbunge wa ANC Fasiha Hassan alimuuliza Mantashe kama mipango ya usalama wa usambazaji wa mafuta ya petroli ya Afrika Kusini inatosha kuhimili usumbufu unaoendelea wa usambazaji wa nje unaotokana na vita.

Mantashe alisema hakuna haja ya kuogopa.

"Utaona kwamba swali hilo linaonyesha hofu. Na kama mfanyakazi wa migodi, jambo moja nililojifunza mapema maishani ni kwamba hofu huua. Licha ya hatari kubwa ya kijiografia, ikiwa ni pamoja na kuvurugika kwa njia za meli za Mashariki ya Kati, mpangilio wa sasa wa usalama wa usambazaji wa mafuta wa Jamhuri unabaki imara."

Mlango-Bahari wa Hormuz

Mantashe alisema msimamo uliotajwa wa Iran unapaswa kupunguza hofu ya usumbufu wa haraka wa usambazaji, haswa kwa Afrika Kusini.

"Nina uhakika ukifuatilia habari, utafahamu kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz unaruhusu mizigo inayokwenda Afrika Kusini bila usumbufu. Kwa hivyo hiyo ina maana kwamba tuna nafasi ya kudumisha usambazaji thabiti kwa muda mrefu. Hakupaswi kuwa na hofu nchini Afrika Kusini; hofu huua."

Mahitaji ya Iran
Mantashe aliongeza kuwa Iran ilizipa nchi hizo mahitaji mawili ya kuendelea kufanya kazi katika eneo la bahari, akisema Pretoria ilikuwa ikiwashirikisha washirika wa Brics kuhusu mzozo wa sasa.

"Katika Mlango-Bahari wa Hormuz, kuna sharti moja wanalotaka, unaweza kulipitia ikiwa wewe si mshirika au katika muungano na Marekani na Israeli. Ikiwa huna muungano na hizo, unaruhusiwa kulipitia. Sharti la pili ni kwamba utalipa Iran kwa rial, si dola."

"Huo ni uamuzi wa kisiasa uliochukuliwa na Iran," Mantashe aliwaambia wabunge. "Mizigo yote inayokuja Afrika Kusini inaruhusiwa kupita. Hakuna hofu ya hili. Isipokuwa unataka kujitambulisha na [Marekani] na Israeli."

SA mdogo anaweza kufanya

Huku bei ya petroli ikitarajiwa kutangazwa wiki ijayo, Mantashe alisema hakuna kitu kikubwa ambacho Afrika Kusini inaweza kufanya kuhusu mishtuko ya bei ya mafuta.

"Kuna mambo tunayoweza kufanya na mambo ambayo hatuwezi kufanya. Ikiwa mizigo haiwezi kutufikia kutoka Mashariki ya Kati, basi ifike Aprili 1, unaweza kutarajia ongezeko la bei. Njia pekee ambayo Afrika Kusini mwa Afrika inaweza kupunguza hatari ya mshtuko wa bei ya mafuta ni kwa nchi hiyo kuendeleza rasilimali zake za mafuta."

"Njia pekee ni kuchimba, kuchimba, kuchimba na kuzalisha mafuta yetu wenyewe. Tusipofanya hivyo, hatutashinda hatari za vita. Kila wakati tunapochimba, tunapelekwa mahakamani. Kama tungekuwa na mahakama maalum zinazoshughulikia kesi hizo, ingesaidia sana kutatua tatizo hilo. Kama tuna vyanzo vyetu vya nishati, tunaweza kupunguza," Mantashe alisema.

Wakati huo huo, huku Waafrika Kusini wakijiandaa kwa ongezeko kubwa la bei ya petroli linalokaribia, wakazi katika Rasi ya Cape tayari wanahisi shida.

Ripoti za mgao katika vituo vya huduma vya Garden Route na kuchelewa kwa usafirishaji wa dizeli kumeibua wasiwasi, hasa ndani ya sekta ya kilimo katika wakati muhimu katika kalenda ya kilimo.

Mbali na dizeli, bei za pembejeo, kama vile mbolea, pia zinaongezeka kutokana na ongezeko lililopangwa la gharama za mafuta na dizeli.

Bei za petroli

Kulingana na data ya hivi karibuni ya Mfuko Mkuu wa Nishati (CEF) wa Afrika Kusini mwezi Machi, bei za petroli na dizeli zinaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa bei kutokana na vita vinavyoendelea nchini Iran.

Takwimu za CEF zinaonyesha kuwa petroli ya oktani 93 ina upungufu wa urejeshaji wa 507, huku petroli ya oktani 95 ikiwa na upungufu wa urejeshaji wa 562.

Madereva wanaotumia magari yanayotumia dizeli wanakabiliwa na kupanda mlima kwa kasi zaidi.

Bei ya dizeli (0.05% sulfuri) ina upungufu wa uzalishaji wa 937, huku dizeli yenye (0.005% sulfuri) ikiwa 950.

Utabiri

Ikiwa utabiri huu hautabadilika, madereva nchini Afrika Kusini watalazimika kubeba uchungu wa kupanda milima mikubwa tarehe 1 Aprili.

  • Petroli 93: Ongezeko la R5.07 kwa lita;
  • Petroli 95: Ongezeko la R5.62 kwa lita;
  • Dizeli 0.05%: Ongezeko la R9.37 kwa lita;
  • Dizeli 0.005%: Ongezeko la R9.50 kwa lita; na
  • Mafuta ya taa yanayotoa mwanga: Ongezeko la R11.00 kwa lita.
Chanzo: The Citizen, Afrika Kusini

​

‘Cargo destined for SA passing through Strait of Hormuz without interruption’ – Mantashe​


Mantasheg.sg

Screengrab: The Citizen News
South Africa’s Mineral and Petroleum Resources Minister Gwede Mantashe has urged South Africans not to panic about a possible fuel shortage, saying vessels carrying cargo and supplies destined for South Africa are passing through the Strait of Hormuz without interruption or threats of attacks from Iran.

Mantashe was responding to questions in the National Assembly on Wednesday as South Africans remained deeply concerned about fuel shortages and a possible massive spike in fuel prices, which is expected to kick in next week.

Fuel supply

The United States and Israel’s war in Iran has ignited global panic, with the conflict expected to severely impact fuel prices and supply.

During the session in the National Assembly, ANC MP Fasiha Hassan asked Mantashe whether South Africa’s petroleum supply security arrangements are adequate to withstand sustained external supply disruptions resulting from the war.

Mantashe said there was no need to panic.

“You will see that the question reflects panic. And as a mineworker, one thing I learnt early in life is that panic kills. Despite the heightened geopolitical risk, including the disruption to the Middle East shipping routes, the Republic’s current petroleum supply security arrangement remains robust.”

Strait of Hormuz

Mantashe said Iran’s stated position should allay fears of immediate supply disruption, especially to South Africa.

“I am sure if you monitor the news, you will appreciate that the Strait of Hormuz allows cargo that goes to South Africa without interruption. So that means we have a chance to maintain a stable supply for a long period of time. There should be no panic in South Africa; panic kills.”

Iran’s requirements
Mantashe added that Iran gave countries two requirements to continue operating in the strait, saying Pretoria was engaging Brics partners about the current conflict.

“In the Strait of Hormuz, there is one requirement they want, you can go through if you are not a partner or in alliance with the US and Israel. If you are not in alliance with those, you are allowed through. The second requirement is that you will pay Iran in rial, not dollars.

“That is a political decision taken by Iran,” Mantashe told MPs. “All cargo coming to South Africa is allowed through. There is no fear of this. Unless you want to identify yourself with [the US] and Israel.”

Little SA can do

With the price of petrol expected to be announced next week, Mantashe said there was little South Africa could do about oil price shocks.

“There are things we can do and things we can’t do. If cargo cannot reach us from the Middle East, then come 1 April, you can expect a price increase. The only way that SA could mitigate the risk of oil price shocks would be for it to develop its own petroleum resources.

“The only way is to drill, drill, drill and produce our own petroleum. If we don’t do that, we will not overcome the risks of war. Every time we drill, we are taken to court. If we could have special courts dealing with those cases, it would go a long way to solving that problem. If we have our own sources of energy, we can mitigate,” Mantashe said.

Meanwhile, as South Africans brace for a massive looming petrol price hike, residents in the Cape Peninsula are already feeling the pinch.

Reports of rationing at Garden Route service stations and delayed diesel deliveries have raised concern, particularly within the agricultural sector at a critical time in the farming calendar.

In addition to diesel, input prices, such as fertiliser, are also rising due to the planned increases in fuel and diesel costs.

Petrol prices

According to South Africa’s Central Energy Fund’s (CEF) latest March data, petrol and diesel prices are showing massive under-recoveries due to the ongoing war in Iran.

The CEF data show that 93-octane petrol has an under-recovery of 507, while 95-octane petrol has an under-recovery of 562.

Motorists using diesel-powered vehicles face an even steeper hike.

The price of diesel (0.05% sulphur) has an under-recovery of 937, while diesel with (0.005% sulphur) is at 950.

Forecast

If these forecasts remain unchanged, motorists in South Africa will have to bear the pain of massive hikes on 1 April.

  • Petrol 93: Increase of R5.07 per litre;
  • Petrol 95: Increase of R5.62 per litre;
  • Diesel 0.05%: Increase of R9.37 per litre;
  • Diesel 0.005%: Increase of R9.50 per litre; and
  • Illuminating paraffin: Increase of R11.00 per litre.
Source: The Citizen, South Africa
 
Azim Dewji askari / mgambo mstaafu aliyeshiriki katika vita vya Kagera anafahamu madhara ya kwenda kinyume na wakubwa wa dunia ?

Machi 27, 2026, 04:02 AM

SOUTH AFRICA 'MGENI WA KAWAIDA' WA MIKUTANO YA G7 YAENGULIWA KUTOKA NAFASI YA KUIWAKILISHA AFRIKA MKUTANO WA MAARUFU WA MATAIFA MAKUBWA YA KIUCHUMI WA G7
1775034948173.jpeg

Vincent Magwenya, Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari pembeni, siku ya ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa G20 katika Kituo cha Maonyesho cha Nasrec jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Novemba 22, 2025. REUTERS/Siphiwe Sibeko/Picha ya Faili

PARIS /JOHANNESBURG, Machi 26 - Maafisa wa Ufaransa siku ya Alhamisi walikana kuitenga Afrika Kusini kutoka kwenye orodha ya walioalikwa kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa G7 mwezi Juni 2026 kutokana na shinikizo kutoka Washington, wakisema Kenya ilikuwa imealikwa badala yake kabla ya ziara ya Rais Emmanuel Macron huko baadaye mwaka huu.

Ufaransa ilitangaza mapema kwamba itawakaribisha viongozi wa India, Korea Kusini, Brazil na Kenya katika mkutano huo utakaofanyika Evian-les-Bains.

Afrika Kusini, amekuwa mgeni wa kawaida katika mikutano ya G7 iliyopita, ilisema ubalozi wa Ufaransa huko Pretoria South Africa uliwasilisha uamuzi huo kwa serikali yapata wiki mbili zilizopita, ikisema Marekani imetishia kususia mkutano huo ikiwa Afrika Kusini itaalikwa.

"Tumekubali uamuzi wa Ufaransa na tunathamini shinikizo walilopata," alisema Vincent Magwenya, msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Alipoulizwa katika mkutano kama Afrika Kusini ilitengwa kwa ombi la Marekani, afisa mmoja wa Ufaransa alisema sivyo ilivyo na kwamba Ufaransa imeamua kuialika Kenya wakati huu. Macron anatarajiwa kutembelea Kenya mwezi Mei 2026 kwa ajili ya mkutano wa siku mbili kati ya Afrika na Ufaransa.

Afisa mmoja wa Ikulu ya White House aliunga mkono kauli ya Ufaransa, akisema uamuzi wa kuialika Kenya ulikuja baada ya mazungumzo miongoni mwa wanachama wa G7, bila kutoa maoni moja kwa moja kuhusu sababu haswa za kutengwa mgeni wa kawaida wa G7 kutengwa yaani Afrika Kusini. Viongozi wa G7 mara nyingi hualika nchi nyingi kama wageni.

"Wafaransa, kwa uwezo wao kama mwenyeji wa G7 wa 2026, walielezea hamu yao mnamo Januari kualika taifa la Afrika kwenye mkutano wa kilele wa viongozi wa G7 wa Juni huko Evian. Baada ya majadiliano miongoni mwa wanachama wa G7, iliamuliwa kwa pamoja kwamba Kenya inapaswa kualikwa kwenye mkutano huo. Marekani inakaribisha ushiriki wa Kenya," afisa huyo wa Ikulu alisema.

1775034917222.jpeg

Picha maktaba : Rais Macron wa France na Rais Ramaphosa wa RSA wakati wa mkutano Viongozi wa mataifa ya G20 uliofanyika ukumbi wa Expo Centre Johannesburg South Afroca 22 Novemba 2025
 
USA wametujengea vyoo vya shule bure, wamejenga rami(Mkeka wa tunduma sumbawznga ova tupo Ulaya), sijagusia misaada ya Fedha, madawa kama ya HIV nakadhalika.....huyu mzee anaongea nini

Na kondomu za kutosha miaka nenda miaka rudi. La sivyo wengine tungeshakuwa statistics.
 
Naunga mkono hoja, naomba kupitia ccm tupeleke uvccm wakiongozwa na lucas mwashambwa ili wote warejee nchini wakiwa kwenye masanduku maana hawana faida yoyote kwa taifa zaidi ya uchawa!.
 
Dewji anafahamu ni kina nani walihusika kujenga yale majengo ya UDSM!

Dewji anafahamu ni kina nani walimsaidia Nyerere kuzima mapinduzi ya kijeshi!

Kuna sababu ni kwanini Tanzania iliamua kuchukua sera ya kutofungamana na yeyote.
 
Mwaka 1955 tulijiunga na Non Aligned Movement (NAM) lengo likiwa kupata misaada kotekote pasi na kuonesha malengo wowote ule. Ni njia ngumu ila ni njia sahihi ya kujihami.
 
Wawapeleke JW wakafyekwe wote na Netanyahu. Hawana faida kwa nchi mbwa hawa.
 
Huyu babu mbona amekua na kiherehere sana
 
Mfanyabiashara Azim Dewji amesema Iran imewahi kuisaidia Tanzania katika nyakati ngumu, ikiwemo msaada wa meli mbili za mafuta miaka ya 70 wakati wa uhaba mkubwa.

Amesisitiza kuwa urafiki wa kweli huonekana wakati wa shida, hivyo Tanzania ina sababu ya kuonyesha mshikamano kwa Iran katika kipindi hiki wanachokipitia.

si ndio TUMEWASAIDIA KWA KUPANDISHA BEI YA MAFUTA AU NI GANI WAJAMENI
 
sasa Tanzania imsaidie nani, imsaidie nini? fedha au zana za kivita
rasirimali watu wakazichape vita vya aridhini make najua wa kwetu wamezoea mstuni.
Na technolojia hatuna
 
Mfanyabiashara Azim Dewji amesema Iran imewahi kuisaidia Tanzania katika nyakati ngumu, ikiwemo msaada wa meli mbili za mafuta miaka ya 70 wakati wa uhaba mkubwa.

Amesisitiza kuwa urafiki wa kweli huonekana wakati wa shida, hivyo Tanzania ina sababu ya kuonyesha mshikamano kwa Iran katika kipindi hiki wanachokipitia.

Iran supports Islamic institutions in Tanzania primarily through cultural exchange, educational initiatives, and charitable aid, largely coordinated by the Iran Cultural Center in Dar es Salaam and the Iranian embassy. These efforts focus on promoting Shiite Islamic teachings, supporting Muslim schools, and providing social services
 
Back
Top Bottom