Ataijulia wapi hiyo sheria, labda siku wakimtia jamba jamba na mambo ya kuficha sukari ndio atamuelewa huyo Mnyanturu Mwenzake...
Ilikuwa bahati sana waandamanji hawakumkamata huyo Biteko na kumchinja pale pale barabarani, ile ilikuwa provocation ya hali ya juu sana, kwa kitendo kile alichofanya, kutaka kukatiza katikati ya maandamano, na yeye kama NPM, ni kwamba hatoshi katika nafasi yake. Watu wana hasira na umeme, na yeye ndio mwenye dhamana, halafu anakwenda kuwasanifu na kuwapitiliza bila hata kutoa neno la faraja kwao...
Polisi nao wajitafakari, siku nyingine wasichanganye maandamano na hii misafara ya viongozi, ni hatari tupu ikiwa waandamanaji watageuka Mbogo na polisi kutumia risasi za moto kuwatawanya. Itakuwa maafa makubwa sana, na polisi ndio wa kwanza kulaumiwa... Hili liwe funzo kwa siku zijazo. Provocation haitakiwi kwa wenye hasira na maisha ya kuunga unga- umeme tabu tupu, sukari hata kijiko kimoja ni anasa, dollar hazipo za kutosha, nchi kama nchi tumekuwa Matonya (RIP) huko duniani, mashirika ya kutuma fedha kama world remit sasa wanakataa kufanya muamala kwa cash, na tunako elekea, Mungu anapajua... Ingawaje mwenye shibe hamjui mwenye njaa, tunawahitaji wenye shibe na watawala wasikie kilio cha wenye njaa na watoe suluhisho kabla mambo hayajawa mambo, ni hayo tu. Mwenye kusikia na asikie.