Azim Dewji: Lissu amuombe radhi Biteko; Matamshi wanayotoa wapinzani hayapaswi kuumiza watu wengine

Azim Dewji: Lissu amuombe radhi Biteko; Matamshi wanayotoa wapinzani hayapaswi kuumiza watu wengine

Natumaini barabara hiyo ilikwishafahamika kwa uongozi wa Mkoa kuwa unatumika kwa maandamano ya CHADEMA basi kama ndo hivyo Mhe. Naibu Waziri Mkuu angejulishwa na uongozi wa Mkoa na aidha angesubiri kupita barabarahiyo au vinginevyo. Hapo naona ni kasoro ya uongozi wa Mkoa. Kila mtu/Taasisi lazima iheshimiwe.
 
Mfanyabiashara maarufu wa Magari mapya nchini Bilionea Azim Dewji amewataka Chadema wawe Wastaarabu vinginevyo Rais atayafungia Maandamano

Source: Jambo TV
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Huyu mhindi ni ukoo wa nani kule Singida? Lissu siyo muuza sembe na mkwepa kodi
 
Wananchi tumekata tamaa ,serikali ilitambue hili.
 
Back
Top Bottom