Azim Dewji: Nilimkataa Robertinho kuwa Kocha wa Simba

Azim Dewji: Nilimkataa Robertinho kuwa Kocha wa Simba

"Niliwauliza viongozi wa Simba Sc huyu kocha ametoka timu gani wakaniambia ametoka Vipers ya Uganda, niliwaambia mbona Vipers ni timu ndogo sana sisi tunataka kocha mkubwa sio kocha wa kutoka kwenye timu ndogo sisi malengo yetu ni makubwa”

Azim Dewji - Mfadhili wa Zamani wa Simba na mdau wa soka nchini akizungumza sakata la kocha Roberto Oliveira kutimuliwa.
Watasema maneno yote msimu huu.
 
Waacheni Matusi nyie Simba
Mlipoifunga Yanga zile Goli Nne moja mbona wenzenu walitulia.

Mi naona Kocha Mgunda asingeondolewa Simba, tunathamini Sana Makocha wa Kigeni.

Kwa sasa wamrudishe Mgunda tu.
Haina haja ya kuhangaika na Makocha wa haraka haraka.

Maneno yenu yaheshimu wawekezaji .
Hiyo Man United inafungwa goli Sita sembuse Simba.
 
Hana ujinga na yuko sahihi. Labda wewe ndo una ujinga.

Wadau wengi wa Simba walikuwa wanataka aje kocha aliyewahi kupata mafanikio makubwa kwenye soka la Africa (CAFCL au CAFCC). Robertinho ana CV gani kubwa kwenye hayo mashindano?

Wanasimba walitaka uongozi usilete tena hawa makocha wa kizungu wasiolijua vyema soka la Afrika (wakiwemo Sven Vandernbrock, Robertinho,n.k) bali waletwe wababe wa Kiafrika kama akina Florent Ibenge,aliyekuwa kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Ghana,n.k. Haya huyo Robertinho anafikia CV ya hao niliowataja?

Credit haikuwa kufundisha Fluminense, maana kuna mtu alikuwa kutoka Real Madrid (Gomez) na bado akachemka.Credit ilikuwa kulijua na kuliweza soka la Africa.
Umeandika sana ila umeandika mambo yasiyoeleweka.
Ni lini Gomez alifundisha Madrid? Kama unakosea vitu vidogo kama hivi, hayo mengine uliyoandika kuna haja ya Kujadili?
 
Umeandika sana ila umeandika mambo yasiyoeleweka.
Ni lini Gomez alifundisha Madrid? Kama unakosea vitu vidogo kama hivi, hayo mengine uliyoandika kuna haja ya Kujadili?
We mpuuzi, wakati Gomez anakuja CV yake ilionyesha amepita wapi na wapi?

Au ukisikia Real Madrid ni mpaka iwe ile Madrid ya wakubwa(akina Vinicius Jr)?

Alipoanza kufanya vibaya siyo Uto walioanza kuitania Simba kuwa wameleta kocha kutoka Real Madrid na bado wanachemka. Hiyo kauli 'kutoka Real Madrid' unadhani ilitokana na nini?
 
We mpuuzi, wakati Gomez anakuja CV yake ilionyesha amepita wapi na wapi?

Au ukisikia Real Madrid ni mpaka iwe ile Madrid ya wakubwa(akina Vinicius Jr)?
Unarudia tena makosa, sababu ya Ujuaji.
Ulishindwa hata kugoogle? Hata kama hujui vitu.
Ni lini Gomez CV yake iliandikwa amepita Madrid?
Acha kujitia aibu, ujanja mwingi mbele kiza.
 
Unarudia tena makosa, sababu ya Ujuaji.
Ulishindwa hata kugoogle? Hata kama hujui vitu.
Ni lini Gomez CV yake iliandikwa amepita Madrid?
Acha kujitia aibu, ujanja mwingi mbele kiza.
Nilimaanisha kocha Pablo Franco. Na kusahau kupo hata wewe huwa unasahau, ila hiyo haifanyi hoja niliyoitoa hapo juu ionekane haifai.

Sema kama wewe hujawahi kusahau.
 
"Niliwauliza viongozi wa Simba Sc huyu kocha ametoka timu gani wakaniambia ametoka Vipers ya Uganda, niliwaambia mbona Vipers ni timu ndogo sana sisi tunataka kocha mkubwa sio kocha wa kutoka kwenye timu ndogo sisi malengo yetu ni makubwa”

Azim Dewji - Mfadhili wa Zamani wa Simba na mdau wa soka nchini akizungumza sakata la kocha Roberto Oliveira kutimuliwa.
Kama Dewji anamaanisha na yeye yupo kwenye Kamati ya ushauri basi wamchukuwe Pitso Masomane ndio kocha wanayemtaka Simba.
 
Waacheni Matusi nyie Simba
Mlipoifunga Yanga zile Goli Nne moja mbona wenzenu walitulia.

Mi naona Kocha Mgunda asingeondolewa Simba, tunathamini Sana Makocha wa Kigeni.

Kwa sasa wamrudishe Mgunda tu.
Haina haja ya kuhangaika na Makocha wa haraka haraka.

Maneno yenu yaheshimu wawekezaji .
Hiyo Man United inafungwa goli Sita sembuse Simba.
Nitajie kocha mmoja tu mzawa anayefundisha klabu kubwa nje ya Tanzania.
 
Kutoka timu ndogo sio sababu, huyu mzee siku hizi anaropoka sana ndio tatizo lake.

Yule kishingo hata hajulikani alitoka timu gani, lakini mpira ilioucheza Simba ikiwa chini yake ilimfanya mpaka vilabu vikubwa Afrika vikamuona na kumchukua.
 
Tatizo ni kuropoka kwingi as if mtaweza kuwalipa, msidhani kupata kocha mwenye mafanikio ya kimataifa mtakuwa mnamlipa pesa ya madafu, inahitajika hela kweli

Jaribu kufuatilia wenzetu wa Afrika Kaskazini ama Kusini wanawapipa sh ngapi ndio utajua kuwa, viongozi na mashabiki kinachowaponza ni kuropoka ilhali kugharamia hawawezi
Gamond anakuja mrefu mbona.
 
Back
Top Bottom