@Waberoyamkuu una moyo wewe!!
soma tathmini ya Nyerere ya AA baada ya miaka 10
http://www.tzonline.org/pdf/thearushadeclarationtenyearsafter.pdf
soma artcile hii ya mihangwa pengine itakufurahisha kidogo, lakini tatizo la msingi liko palepale tu.....kuwa Nyerere alikosea sana kuanzia mwanzo
Home*»*Insight
1. Nyerere alikosea ujamaa...haukuwa wakati wake na yy alijua hivyo
2. AA ilikuwa aidea yake baada ya miaka 10 likafa watu inaonyesha watu wake au vijana wake hawakujua lolote...unalosema azimio halikuwa azimio bali tamko!!
Hahahaaa haa! mkuu wangu sio moyo ila nazungumzia ukweli. Unajua labda nikupe mfano wa ndugu yetu William. Huyu kaka aliazimia kurudi Bongo akajenga kichwani vision ambayo bila shaka ni kutaka maisha bora zaidi kwa kujitambua uzawa wake, nafasi yake ktk jamii na kwamba future ya maisha yake iko Nyumbani. Hadi hapa ndipo tunaposimama kwamba haiwezekani mtu kuhama toka Marekani kurudi Bongo pasipo kuwa na vision kichwani, vision ambayo imekufanya utake mabadiliko ktk maisha yako na pasipo kujali umri wa mafanikio isipokuwa kwa kujitambua wewe nani, upo ktk mazingira yapi na unataka mageuzi toka maisha haya kwenda maisha fulani.
Kichwani kisha jenga sura ya maisha atakayokusudia kuishi hata kama hatafanikiwa mwaka wa kwanza, wa pili au tatu maadam umeshaweka nia, sababu na uwezo wa kubadilika hayo mengine yanakuwa ni HOPE ya mafanikio. Kwa hiyo kuondopka Marekani ukaenda Bongo kuchambia kopo haina maana umeshindwa maisha hata kidogo ni lazima ujiandae wewe nafsi yako na sii kutegemea kuyabadilisha mazingira ya Bongo yakidhi mahitaji ya ndugu yetu William. Ni william anayetakiwa kujiandaa, kujiwekea taratibu, sheria, miiko na kadhalika kulingana na maisha ya Bongo akiwa na lengo ya kubadilisha maisha yake yeye na sii vitu au watu around him..
Bro, William utanisamehe kwa hili kukutolea mfano, lakini najaribu tu kuiweka hoja yangu wazi.
Sasa kafika Tanzania kajaribu ubunge wa EA, inawezekana ilikuwa sii wazo zuri kwa wengine maana kaukosa ubunge, lakini kibinadamu sidhani kama ana plan moja tu, zipo nyingi tu na hakika hapo alipo tayari kisha gundua ni nidhamu ipi anatakiwa kwa nayo. Kimaisha tayari kesha jenga mwongozo wa jinsi atakavyoishi hapo bongo, kajipangia utaratibu na sheria iwe kwenda kanisani au kujimwaga Karibu lounge yote haya ni ktk mipango ya kutafuta maisha mapya Tanzania. Aidha uyaone makosa ktk baadhi ya maamuzi yake lakini nina hakika ana miiko na maadili hafuati tu sheria za nchi bali nafsi yake inamsuta ktk mengine ambayo yanaweza mkwamisha.
Kwa hiyo wazo lake la kuondoka USA na kurudi Tanzania huambatana na DIRA, yaani kesha visionalize maisha yake akiwa Tanzania, na hata kama hatafanikiwa leo ama kesho haina maana wazo la yeye kurudi Tanzania ilikuwa kosa - Hapana. Pia wazo la kina sisi kubakia nchi hizi haiwezi kupimwa kutokana na mafanikio yetu bali maisha tuishio ndio yanayotazamwa makosa ndani yake ambayo ndio sababu ya kutofanikiwa kwetu maana wapo watu wengine wamefanikiwa aidha kwa kuishi Marekani au kurudi Bongo.
Na hata kama akijaribu siasa kwa miaka 10 ijayo asifanikiwe haiwezi kuwa sababu kwamba William alifanya kosa kujiingiza ktk siasa, isipokuwa muhimu ni tutazame makosa yake yalikuwa yapi kiasi kwamba akashindwa kufanikiwa ktk siasa na sii kulaumu kuondoka kwake Marekani pengine he had no choice ya kubakia Marekani kama sisi tulivyoshindwa kubakia ktk Usosialisti, ati mbona Wachina na Vietnam walibakia na leo hii wanatisha!. We are who we are tutafute muda wa kujitambua sisi kwanza na mabadiliko gani ya kifikra tunayahitaji.