Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,210
- Mkuu waliolitupa Azimo, walifanya hivyo kwa sababu hawakuona likiwanufaisha wengi ndio wakaamua kuweka njia itakayowanufaisha wengi nayo ni Ubepari tulionao sasa. Sio kazi ya Serikali kuona kila mwananchi anakuwa sawa na mwingine kimaisha hapana kazi ya Serikali ni kutoa nafasi sawa kwa wote tu na kusimamia sheria.
- Wakati linavunjwa Azimo, lilikuwa na miaka karibu 25, sasa na Ubepari upewe nafasi kwanza kabla ya hukumu, tuliwapa nafasi na Azimo, limetuletea maafa ya ajabu sana, sasa na Ubepari uachiwe kwanza ndio tutoe hukumu!
William.
Mkuu Malecela, kama lengo lilikuwa ni kutafuta njia ya kuwanufaisha wengi lilikuwa ni jambo jema sana. Lakini kilichopo ni kwamba njia aliyokuja nayo imewadunusha wengi zaidi kuliko wakati za azimio la Arusha na kuwaneemesha wachache sana, na kuwa matajiri wa kupindukia na kuufanya utawala na uongozi wa nchi kama ufalme.
Ukiangalia sasa hivi naweza kusema kuna maafa makubwa zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa azimio la Arusha. Angalia afya, elimu, maji. Hovyo zaidi kuliko wakati wa azimio la Arusha.
Sina maana kuwa azimio la Arusha was 100% perfect, tunatakiwa kuchukua yale ya msingi na yale mabaya tuyaweke pembeni, na tusifute mazuri kama tulivyofanya kule Zanzibar na kuweka mengine ya ovyo. Mkuu, tataizo la Azimio la Zanzibar sio kuleta ubepari, bali ni kuondoa miiko ya uongozi na kuruhusu viongozi kuwa wezi, na kutowafanya accountablem