Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!


Mkandara,

Hivi una matatizo gani ya kutoelewa. Azimio la Arusha lilipitishwa na Halmashauri kuu ya TANU. Azimio la Zanzibar lilipitiswa na Halmashauri ya CCM. Maazimio yote haya ni mali ya Chama cha Mapinduzi. Ni wanachama wa Chama hicho wenye kuhamua jinsi ya kuyafuata na sio Taifa.

Hata sherehe za kuzaliwa kwa CCM na kutangazwa kwa Azimio la Arusha sio sherehe za kitaifa. Hivyo unachotakiwa kutambua ni kuwa ujio wa vyama vingi ulifuta baadhi ya mambo kuwa ya kitaifa. Mojawapo ya hayo mambo ni hayo maazimio.
 

I agree with what you say. However, that doesn't change what I have said before: Nyerere didn't grasp principals of finance and economics.
 
Of course the current government and everybody in a good position is molesting the country. However, there's a surprising fact. The majority in the government grew up reciting Azimio la Arusha, like an altar boy gone bad.
Tatizo nadhani pro-Azimio wanajaribu kuchanganya itikadi kama mwongozo wa kutunga sera (which is the case) na itikadi kama mwongozo wa kutunga sheria (which is not appropriate in our times). The former is practical but then not through a failed declaration such as 'the Arusha Declaration' blueprint, and the later is not accepted in today's world kwa sababu hizo hizo za mifano yao ya dini walioileta.

Mfano the West until a century a go most of the laws were a result of Christianity doctrine, and most of those laws were centered around morals. People have come to understand morals evolve, what was unaccepted in the early 20's might no longer carry the same reasoning lines in the future. Therefore the emphasis of making new laws shifted from doctrines to understanding (rationale approach).

Na pale bado kunako tumia doctrines (especially religion) ndipo kwenye conflict nyingi, kwa hivyo si kweli kwamba mzungu ana haribu huko middle east kila kitu. Ndio anatumia upenyo uliopo kati ya wale wanaotaka secular state na wale wanaotaka muongozo wa dini to advance his economical goals (but then dini si kila mtu anaamini kila kitu these days) therefore it wrong to assume the west is intervening in their ways of lives.

Tukirudi kwenye ma-azimio haya hayana tofauti kubwa na dini (except these are political doctrines), kwa maana hiyo kusema eti tutunge sheria kupitia maazimio ni yale yale tu, kwa mfano kwenye hii thread pekee kuna makundi mawili pro and anti Azimio, kuweka sheria za nchi kupitia Azimio tayari umeshawachagulia wengine namna ya kuongozwa ki maisha kupitia Azimio Uchwara. Ndio sababu popote pale duniani kwenye kutaka kuweka misingi ambayo ni impractical only to suit megalomaniac leaders egos kuna haya mambo, na kote huko kuna one thing in common heavily police states. Ndio effects hizo hizo bado zipo na kwetu kupitia azimio, maana kuna watu waliotokea kwenye maazimio bado wana amini ndio special breed kutokana na previleges walizokuwa nazo zama hizo na excessive usalama wa taifa kwa nchi maskini kama yetu.

Ndio maana Azimio kwa kweli litupwe na makarabsha ya chomwe moto yote huwezi kutunga sheria kupitia itikadi. Maana ya sheria ni kutoa sanctions inapovunjwa, sasa mntaka tuweke sheria kupitia aspects za azimio wakati kuna watu tayari hawalitaki. Kuna namna nyingine za kuweka accountability lakini si kupitia Azimio la Arusha.

By the way kugawa ardhi yetu kijinga kwa kisingizio cha uwekezaji ni upuuzi, that doesnt mean I am anti capitalism too. The state has a role in many things.....oops the argument i want to bring is not valid in this stance.
 
It' actually based on Hammourabi's code and Magna Carta/ Napoleonic laws.
Christianity has its base or it's grounded on "The Eucarist"
Constitrutional legitimacy is grounded on the foundation of the concept of the "Rule of Law"
And the rule of law can either be a "Process" or "Substantive"
Sasa kutokana na hayo, ndiyo unaweza labda kuniambia kwanini itikadi isiwe kama mwongozo wa kutunga sheria. Ninaamini kuwa itikadi (like in China) inaweza kuwa ni mwongozo wa kutunga sheria. Not neccessarily Morals au Norms au Moral norms.
 
Hitimisho la Mjadala ..?

1. Kinyume cha UTU Huru wa MTU sio hali ya Unyama kama wengi wanavyotaka kutusadikisha. Si sahihi kumuita mtu aliyesaliti uasili wake ambao ni Utu wake kuwa, kwa kuukosa Utu sasa ana unyama. Mnyama hakusaliti uasili wake ili kuufikia Unyama ambao ndio asili yake, mnyama hajafanya kosa lolote ili kuwa mnyama. Mtu kuusaliti na kutelekeza uasili wake ambao ndio utu wake kafanya kosa, na sasa anathamani ya chini kabisa kuliko ya mnyama asiyefanyia mzaha uasili wake ambao ndio unyama wake. Kwa kuwa tunamuongelea MTU kujipambanisha na MAZINGIRA yake ili kujistawisha na kujiendeleza, lazima kuzingatia makundi haya mawali ambayo kwa muonekano wa machoni, watu wote wa makundi haya wanaonekana ni sawa, kumbe sio sahihi. Kosa hili lilifanyika mwaka 1967 lisirudiwe tena. Itamkwe dhahiri kuwa kuna "MTU-MWENYE UTU" na "MTU-MPINGA UTU" ambao watakuwa na miingiliano na makabiliano TOFAUTI kwenye MAZINGIRA yao ili kujipatia Maendeleo.

2. Mtu mwenye UTU kwa mfano akisukumwa na Utu wake, ataona kuwa tupambane na mazingira yetu kupitia Ardhi tufanye Kilimo, Ufugaji na kufanya kazi ili kupata rizki na ustawi wa jamii kama hatua ya mwanzo ya kujenga Taifa changa kwani ndicho kinachoweza kuwafikia wananchi wake wengi kwa wakati huo. Lakini Mpinga Utu atasukumwa Kibinafsi na Kupinga Hoja hiyo na kuona tufanye biashara nk ambayo si muafaka kwa wakati husika. Mpinga UTU anayetawaliwa na ubinafsi ulio kithiri, kwani ndio utambulisho wake, anapopewa kundi la watu kuwaongoza ili kukabiliana na Mazingira yao, atapelekea madhara makubwa, hivyo lazima KU/Azimia namna ya kuwadhibiti Wapinga UTU kabla ya kuanza mchakato wowote kustawisha na kuendeleza jamii! Azimio La UTU lililoasisiwa Arusha, haliko ili likubalike kwa namna yeyote na wapinga UTU, bali liko ili kuwakabili na kurejesha heshima na usawa wa utu kwenye Maendeleo ya Jamii HURU na yanye KUHESHIMIANA katika ujenzi wa Taifa.

3. UTU Huru wa MTU unahitaji kulindwa, kujengwa, kurutubishwa na kusimamiwa ili kumsukuma MTU kikamilifu kujipambanisha na Mazingira yake ambayo ndio rasilimali, mali ya asili, mitaji, ardhi, bahari na kila lile lililoko kwenye mazingira yake ili kumjegea maendeleo yake. UTU wa MTU ni "RASILIMALI MAMA" na Mazingira yake yanakuwa ni "RASILIMALI MAZINGIRA" ambazo zote kwa pamoja vinatupelekea kwenye Maendeleo ya Mtu kwenye Mazingira yake.

4. Isipokuwa kwa Mpinga Utu peke yake, hakuna mtu mwingne asiyejua kuwa bila rasilimali mama, rasilimali mazingira peke yake hugeuka na kuwa vyanzo vya magonjwa, vita, ufukara, ukandamizaji, ufisadi nk. Bila rasilimali mama (Utu wa Mtu kushika hatamu ya Jamii/Taifa) ambao ni ujulma wa utu wa jamii, "Mazingira yanabadilika na kuwa chombo cha kumuadhibu Mt". Ni Mpaka Mbegu ya utu kifamilia na Kitaifa, itawale jamii husika ndipo Mazingira na rasilimali zake zote zinaweza kumuendeleza na Kumneemesha Mtu. Rasilimali mazingira na Madini yote ya thamani chini ya Utawala Usiozingatia UTU ambayo ndio rasilimali mama, Madini hayo yanakuwa vyanzo vya kustawisha wachache na pengine kuzua machafuko na vita kati ya "walikowa nacho" na wale "waliodhulumiwa" hivyo kubomoa na kuangamiza maendeleo kwa kila hali. Kunahitajika Azimio La UTU lililo IMARA kabisa na "linaloendana na wakati kila wakati" ili Kunusuru UTU WA TAIFA usifanyiwe mzaha na kuchezewa na wapinga Utu, katika michakato yote ya kijamii ili kufikia maendeleo na ustawi wa jamii ya Kitanzania.

5. Kuwadhibiti wapinga Utu, ambao wakifanikiwa "kusoma" na "kuhodhi fedha" wanaweza kabisa kusambaratisha UTU Huru wa mtu kwenye jamii, Lazmia SASA Katiba ya nchi, Sheria za nchi, Miiko ya nchi, Maadil na Elimu ya nchi vione ukweli huu na vitamke rasmi kwa kuazmia, kama Taifa kuwapinga na kuwachukulia hatua zote za kuwatokomeza Wapinga UTU wa Taifa, ili kusitiri na kustawisha Utu wa familia, jamii na Taifa kwa ujumla! Nani haoni kwa sasa UTU wa jamii ulivyoshuka na Wapinga UTU (Magugu MTU) walivyoshika Hatamu? Taifa sasa liamke na kutambua kwa undani unapotoka msukumo hasi wa kijamii unaodiriki kupinga kwa hali na mali thamani ya Utu huru kwenye jamii! Hii itatoa mwanga wa kutokufanyia mzaha Azimio Lolote La Utu litakalokuwepo kwenye WAKATI HUSIKA!

6. UTU HURU wa MTU uliokuwa ndio lengo letu la mwaka 1961, haupitwi na wakati, Ulikuwepo, Upo na Utakuwepo wakati wowote atakapokuwepo Mtu na Mazingira yake Tanzania na duniani. Kwa kuwa UTU unajieleleza kupitia kauli, fikra na matendo ya mtu ili kijipamabanisha na mazingira yake, ni hakika basi muoenekano wa nje wa dhana ya Utu utakuwa unabadilika kwa vipindi mbalimbali kama ilivyo kweli kwa mabadiliko ya fikra, kauli , matedo na mabadiko ya mazingira ya Mtu, LAKINI KATU UTU NA THAMNI YAKE KAMWE HAVITABADILIKA NI ULE ULE NA UNAHITAJI UANGALIZI makini kupitia azimio sahihi dhidi ya wapinga Utu wakati wote.

7. Ni wendawazimu kufikiri kuwa Azimio la Utu, utafika wakati likatapitwa na wakati na kutotahitajika kabisa huku magugu Mtu yapo wakati wote katika jamii hiyohiyo. Hiyo itakuwa ni kweli tu wakati mwanadamu atakuwa ametoweka duniani. Kama ilivyo mimea shambani inayoshambuliwa na magugu wakati wote na kuhitaji palizi la mara kwa mara, ndivyo Azimio La Utu litakavyohitajika wakati wote na kila wakati likija na makali yanayolingana na aina ya magugu yaliyopo, kwani magugu nayo pia ni viumbe vinavyopambana na mazingira yake ili kujisitiri na kunedeleza vizazi vyao na kutokukubali kushindwa na kutoweka kirahisi kwenye uso wa dunia.

8. Mchunguze kwa makini MTU mwenye msukomo wa kupinga UTU wake, wa wenzake na wataifa lake. Kwa kuwa utu ndio msingi wa Uhai na maisha ya mtu, katika kuishi yaani "LIVE" na mpinga UTU anapinga KUISHI basi aitwe jina hili hili la "LIVE" lakini, spell it backward and what do you get!? Yes you r right ant humans are not animals they are "LIVE" spelled backwards! Ingawa wengi wanapenda kutumia neno Fisadi, lakini utagundua kuwa jina la hawa watu linakwenda na wakati au vipindi na mazingira yao! Wakiwa urusi watakuwa na jina lao, wakiwa Kenya jina lao, wakiwa Tanzania jina lao wakiwa uingereza jina lao na jina linaweza kubadilika kulingana na nyakati jamii inapojikuta na kupitia!

9. Mjadala huu hautatupatia muafaka wa pamoja ni hakika! Na sifikiri kuwa ndio lengo lake. ILA Utafanikiwa kutupembulia Makundi haya mawili muhimu ambayo yako kwenye jamii wakati wote na ambayo KUSIGANA KWAKE ndiko kuna "define" ustawi na maendeleo ya jamii ya Tanzania. Na kiuwkeli kabisa yangetakiwa yawe ndio chimbuko la Vyama Vya Upinzani na michaato muhimu ya kijamii.

10. Ni vema tuwe wakweli kabisa na kuona hatari ya Wapinga UTU wanapozidi kushamiri kama uyoga na kuiteka jamii. Hivyo lazima tuazimie bila kubabaisha na hatua za haraka zichukuliwe na bila mzaha kurejesha UTU WA TAIFA kwenye mikono salama. Tunahitaji Azimio La Utu Huru wa Mtu katika kukabiliana na mazingira yake katika "mtizamo mpya" Kwani ni kweli halipingiki Ili kuipata Tanzania tunayoikusudia!!!
 
It' actually based on Hammourabi's code and Magna Carta/ Napoleonic laws.
Christianity has its base or it's grounded on "The Eucarist"
Constitrutional legitimacy is grounded on the foundation of the concept of the "Rule of Law"
If that is the case what was the bases of King Henry departure from Catholism to Church of England? what are the bases of abortion laws and many moral issues today in the west and also why many of these morals laws are being challenged in human rights courts?

The Magna carta introduced new ways of thinking outside the church and monarchy ideas which were dominant of the time lakini hayo mambo yako mengine ya 'Hammourabis code' sijui umeyatolea wapi and how they fit in modern political discussions.

Becuause the 'rule of the law' in modern times is based on democratic ideas. The values of democracy are freedom of choice (ndio maana hata nchi nyingi duniani zinashinikizwa kuwa na vyama vingi) to name a few, sasa kama utaweka ideologies za chama na kuzifanya sheria ya nchi tayari umeshavunja misingi ya democracy na mbele your bound to violate human rights acts, kawaulize huko 'North Korea' imefikia hatua through propaganda kuna watu wana amini Kim Jong alikuwa kama mungu, lakini hivi si ndio kama tanzania baadhi wanavyoamini kuhusu Mwalimu coming to think of it wengi ni ndio washabiki wa azimio today.
 


mkuu
kiongozi bora ni yule anayeshirikisha watu wake katika kufanya maamuzi(participatory leadership)lakini endapo watu hao umewazidi sana elimu amahawana kabisa uelewa juu ya mambo mbalimbali kiongozi hutakiwa kudectate kutoaorder na watu kufuata kwa sababu utawashirikisha utajadiliana nao nini amawatakusumbua ama hamtafikia muafaka wa kile unachotaka kifikiwe ila jambo hiloliwe kwa manufaa ya hao unaowaongoza.
mwalimu alikuwa na wakati mgumu sana kwani asilimia kuwa ya watu wakati huohawakuwa na elimu na hawakuelewa yaliyokuwa yanaendelea na namna ganiwatajikwamua ilibidi mwalimu kutumia hiyo hali unayoona ya kidikteta and he wasright.
ni kama una mtoto ambaye inabidi umfanyie maamuzi ili kumsaidia kufanikiwakwake.
lakini sina hakika kabisa kuwa mwalimu hakushirikisha watu wake.
nakubaliana na wewe kabisa kuwa leadership is an art napenda kukuhakikishiakuwa mwalimu kuja na azimio la arusha was an art in his leadeship. kwa sababuile namna unayotawala zile mbinu unazofanya zile strategies unazotumia ni art.mchunguze mwalimu then angalia viongozi wa sasa nani kaja na chochote kipyaamebaki mwalimu pekeyake kuwa kiongozi wa pekee aliyekuja na kitu cha kufanywakwa maendeleo ya taifa. iwe imefeli au kufaulu ilikuwa ni creativity ya ainayake. na kwangu ilifanikiwa kwa baadhi ya mambo na ninamsifu kwa hayo.

 
Mkuu wangu naona mimi nawewe hatutaweza kuelewana. Hakuna mahala nimesema Azimio la Arusha na Zanzibar sio zao la CCM lakini unachoshindwa kuelewa ni CCM hyo hiyo inayoongoza nchi hii kwa miaka yote, ni CCM hii ndio iliyotunga Katiba na Sheria zilizopo sasa sielewi tunabishana ju ya kitu gani. Ujio wa vyama vingi haukubalisha sheria yoyote inayohusu WATU zaidi ya demokrasia ya chaguzi lakini mamlaka ni yale yale, isipokuwa kuna tofauti kubwa kati ya wakati wa Azimio a Arusha na Azimio la Zanzibar.

Jamani hizi sheria na Katiba hata Hitler alikuwanazo ambazo ukizisoma hutaona makosa ila utawala bora, maana Hitler mwenyewe alitangaza AMANI (peace) ktk kila speach zake, sheria na mkazo mkubwa wa uwajibikaji na naweza kusema hakuna kiongozi aliyewahi kupendwa na wananchi wake hapa duniani kama Hitler - Hakuna!. Lakini unapotazama Azimio lake, walitaka kujenga Ujarumani ipi, ile kutaka kuitawala Ulaya kama Napoleon, Kuudhihirishia ulimwengu kwamba wao ndi Taifa bora kuliko yote, superdupa, kuutaka Ushujaa na kisasi cha kupambana na Wayahudi kwa imani kwamba ndio waliomuua Yesu...Hapa ndipo tunapo kwazwa na Azimio hilo na kuwaona ukoma.

Mtazame Ghadaffi yeye, pia alikuwa Azimio la kitaifa la Ujamaa pia ambalo walilipenda wote, katiba na sheria zikatungwa akitangaza demokrasia ya aina yake, akiwapa wananchi wake kila kitu toka Elimu hadi welfare kila mwezi hata kama huna kazi, lakini sii kitu walichokitaka wananchi kwa sababu alikuwa na nia ya kuitawala Libya hadi kifo kitakapo mkuta na pengine kuwarithisha wanawe, kumbe ndio ikawa sababu ya mwisho wake. Maazimio haya ndio yaliyowaangusha Watawala hawa tofauti na CCM ambao hadi leo hii wametawala kupitia maazimio mawili kwa nyakati mbili tofauti.

Hivyo mkuu wangu nakubaliana nayi sana mnaposema Azimio la Arusha halikuwa zuri na mkazieleza athari zake lakini na ubishi ukabakia ktk uzuri au ubaya lakini sii kusema Utawala wowote hautakiwi kuwa na Azimio ama wananchi kujua umuhimu wa Azimio maana hapa tunatawaliwa na Azimio la Zanzibar na wewe kama mtanzania lazima ufahamu CCM walitaka kulijenga Taifa la aina gani na haya madudu yote ya Ufisadi ni mavuno ya Azimio hilo.

Pili, Nachokataa mimi ktk mjadala huu ni wazo la kwamba ni Azimio la Arusha lililotufikisha hapa, tunachosema sisi haya sii kweli kabisa kwa sababu Azimio hilo tuliliacha na halipo tena na mnasema halifai hata kuwepo isipokuwa tunatakiwa kufuata sheria tu, sasa tunachoshangaa iweje kitu ambacho hakina mumuhimu kiwe ndio sababu ya kutufikisha hapa tuipo hata baada ya miaka 20 tulipokiacha?.

Je, Azimio ni muhimu au sio muhimu?. Kama sio muhimu kwa nini mnalilaumu Azimio la Arusha kuwa sababu, kama ni Muhimu je Azimio letu leo hii ni lipi?.. haya ndio maswali nilokuwa nayo toka mwanzo sema tunapigana chenga tu...Hadi leo tunatawaliwa na Azimio la Zanzibar ambalo wewe kwa fikra zako unasema halipo wakati unakubaliana na maamuzi yote ya Azimio la Zanzibar ambayo yanafanya kazi hadi leo chini ya katiba na sheria mpya ambazo zimeondoa miiko na maadili kwa viongozi wetu. Halafu vichekesho mnamtaka JK awawajibishe mawaziri na viongozi wanaohujumu Uchumi kwa sheria, sheria gani ikiwa sheria zilizopo zimetungwa kutokana na Azimio?. Kuhujumu Uchumi sii lazima iwe makosa ya jinai ndio maana ya Fisadi huyu kwa ufasaha huitwa Mharibifu, iwe hata sawa na ng'ombe aloingia shambani kwako akala mahindi huyu huwezi kumhukumu kwa kutazama njaa yake ama sheria za mwizi ila hufungwa kamba shingoni.
 

Mkandara,

The fact that you have mentioned Hitler and Ghadafi in this post tells a lot why you need Azimio la Arusha. You want a dictator who shouts from the mountain top.
 
HODI WANAJAMVI! Ni mwanaafrika mwenzenu, ni tayari kujifunza na kuishi maarifa mapya kutoka kwenu, naomba mnipokee!

Nirudi kwenye mada...
Naamini kuwa maisha ya mwanadamu hutegemea sana mambo mawili,
1. MAZINGIRA, yaani anaishi wapi na nani.
2. NYAKATI, anaishije, yaani mahusihano baina ya mtu na mtu na mazingira yao (tamaduni, itikadi, imani, mitazamo, mifumo, taratibu, falsafa, nk.).
Katika hili, napenda kujitambua kwamba sisi ni waafrika, wenye mazingira mahususi kwetu, yafahayo kuongoza mahusiano yetu kati ya mtu na mtu, na mazingira yenyewe! Mambo hayo ndiyo yaongozayo wajibu wa mtu kwa jamii yake! Upi ni wajibu wa mwanaafrika?
Mungu alipotuumba, alituumba na kutuwekea msingi mkuu wa maisha nafsini mwetu, UTU! Mantiki ya UTU i nafsini mwake mtu, kutoiishi ni kujisaliti na kujinafiki, ni kujikataa. MANTIKI hii imo kwa kila mtu, haibadiliki, kumbe kila mtu angeiishi maisha yangekuwa ni furaha, kwasababu ya MANTIKI ya UTU ndaniye. HAKIKA, kwangu "MAISHA NI FURAHA, KAMA HAIPO NI UPUUZI TUPU". Na hakuna furaha ya MTU ila WATU! Nitatoa mifano miwili midogo...
"...fikiria furaha ya simba mawindoni amuonapo mwanaswala mnono, mate humtoka na mkia kutotulia....furaha yake ni juu ya mnofu wa swala "
Fikiria tena hili "...mtu mwenye kufurahia mali zake na familia yake ndani mwao "ni shangwe na kumshukuru Mungu kwa kumjalia", hali jirani kuna yule aliyekosa uji siku mbili, nondo mkononi anavunja geti kumjeruhi mwenye mali, walau apate hata kile kidondokacho mezani mwa mwenye mali" je hakuvuruga furaha huyo, utafurahije kuwa na 3 kwa mwenye 0? Furaha ya simba na tajiri zimekosa MANTIKI, yaani UWIANO SAWA. Simba ni unyama alioumbwa nao, lakini mwanadamu ni kwa kupindishiwa MANTIKI , kulikofanywa na nyakati alizonazo. Kumbe wajibu wetu ni kuuishi UTU kama waafrika, japo umepindishwa nafsini mwa watu, tunaweza kuuimarisha kwa kutumia mfumo ulioundwa kwa MANTIKI ya nyakati na mazingira yetu.
Azimio Jipya, saluti...
Wanajamvi mnastahili kwa kweli.
Mungu wetu anaita!
 


Let me assume that you are correct. Nyerere entitled to take some actions on our behalves because he was leading the nation of illiterates and semi-illiterates. My question is: Should Azimio la Arusha have been a temporary or permanent solution?

Your post implies that it should have been a temporary solution because the country evolves. New people with better education than Nyerere are graduating each year and they should have a chance to decide their own future.

Additionally, you have just proved that colonists were right to decide the fate of our lives because they were educated, and they were entitled, just like Nyerere, to take tough decision on our behalves. Please correct me if I am wrong.
 


Jinga La Falsafa and Azimio la Arusha,

Tanzania is a signatory of universal Declaration of human rights which includes almost everything you have started above. In addition, some amendments were made in order to accommodate human rights in our constitution. If I am not mistaken that was 1984.

So the main problem isn’t to declare or define what human rights are, but to put them into practice. Take for example the issue of ownership. The constitution clearly indicates that we have the right to own properties. However, in practice, government officials can easily take pieces of land from poor people.
 
There's no private ownership of land in Tanzania. And the president is the trustee.
 

- Sawa sawa!

William.
 

Hizi demokrasia za Ku-copy......na za Kushinikizwa inabidi tuziangalie kwa umakini mkubwa na relevance yake kwenye culture yetu/zetu.........demokrasia zinazoshinikizwa kwetu sie na wengine inabidi tuzi-mould tu suit our interest........

Mnaweza kuwa na chuki za binafsi dhidi ya azimio la arusha...........however mjue ya kwamba si kila jambo ndani ya azimio la arusha ni baya........ilibidi tuliimarishe kwa kuondoa vipengele ambavyo si relevant........

siku hizi kuna models mbali mbali za kisiasa na kiuchumi ambazo.......watu hufikiria ku-copy na ku-paste.......again we will be very wrong..........we need our own ideas that will work for us/our nation.........Tanzania yetu mambo ya ujanja ujanja/mishe mishe.......ndio yametifikisha hapa tulipo na wala si Azimio la Arusha......tulili-abuse Azimio la Arusha.....badala ya kuliboresha...........
 
Mkandara,

The fact that you have mentioned Hitler and Ghadafi in this post tells a lot why you need Azimio la Arusha. You want a dictator who shouts from the mountain top.
U chose to ignore! it's all gud...
 
My brother please. Land ownership is not a Universal human right, here in Canada we only hold land permit from the sovereign monarch. as to say Wananchi ni wapangaji tu. The land permit signify agreement between land owner and the crown, not between land owner rights to own the land. As to Tanzania, it's the government who owns the land we are just tenants.
 

Mkuu Zakumi.....waweza kutudadavulia hiyo?.......na kwamba ipo katika sheria zetu?
 

Asante sana Mkuu........ hivi jamani ni nchi gani iliyoendelea duniani isiyo na miiko/maadili kwa viongozi wake.........
 
I disagree with you. It's not democracy to our liking. But you can't denie that pluralism is taking shape. The number of opposition MPs has increased, and CCM aren't sure that they will hold power forever.

tuna demokrasia yenye ugonjwa ambao kila mmoja wetu/vyama vyetu a/vinaufumbia macho...........i mean kwa demokrasia tuliyonayo.......kila atakayeingia madarakani atalia "faulo" kwa mwenzake.........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…