1. Kinyume cha UTU Huru wa MTU sio hali ya Unyama kama wengi wanavyotaka kutusadikisha. Si sahihi kumuita mtu aliyesaliti uasili wake ambao ni Utu wake kuwa, kwa kuukosa Utu sasa ana unyama. Mnyama hakusaliti uasili wake ili kuufikia Unyama ambao ndio asili yake, mnyama hajafanya kosa lolote ili kuwa mnyama. Mtu kuusaliti na kutelekeza uasili wake ambao ndio utu wake kafanya kosa, na sasa anathamani ya chini kabisa kuliko ya mnyama asiyefanyia mzaha uasili wake ambao ndio unyama wake. Kwa kuwa tunamuongelea MTU kujipambanisha na MAZINGIRA yake ili kujistawisha na kujiendeleza, lazima kuzingatia makundi haya mawali ambayo kwa muonekano wa machoni, watu wote wa makundi haya wanaonekana ni sawa, kumbe sio sahihi.
Kosa hili lilifanyika mwaka 1967 lisirudiwe tena. Itamkwe dhahiri kuwa kuna "MTU-MWENYE UTU" na "MTU-MPINGA UTU" ambao watakuwa na miingiliano na makabiliano TOFAUTI kwenye MAZINGIRA yao ili kujipatia Maendeleo.
2. Mtu mwenye UTU kwa mfano
akisukumwa na Utu wake, ataona kuwa tupambane na mazingira yetu kupitia Ardhi tufanye Kilimo, Ufugaji na kufanya kazi ili kupata rizki na ustawi wa jamii kama hatua ya mwanzo ya kujenga Taifa changa kwani ndicho kinachoweza kuwafikia wananchi wake wengi kwa wakati huo. Lakini Mpinga Utu atasukumwa Kibinafsi na Kupinga Hoja hiyo na kuona tufanye biashara nk ambayo si muafaka kwa wakati husika. Mpinga UTU anayetawaliwa na
ubinafsi ulio kithiri, kwani ndio utambulisho wake, anapopewa kundi la watu kuwaongoza ili kukabiliana na Mazingira yao, atapelekea madhara makubwa, hivyo lazima KU/Azimia namna ya kuwadhibiti Wapinga UTU kabla ya kuanza mchakato wowote kustawisha na kuendeleza jamii! Azimio La UTU lililoasisiwa Arusha, haliko ili likubalike kwa namna yeyote na wapinga UTU, bali liko
ili kuwakabili na kurejesha heshima na usawa wa utu kwenye Maendeleo ya Jamii HURU na yanye KUHESHIMIANA katika ujenzi wa Taifa.
3. UTU Huru wa MTU unahitaji kulindwa, kujengwa, kurutubishwa na kusimamiwa ili
kumsukuma MTU kikamilifu kujipambanisha na Mazingira yake ambayo ndio rasilimali, mali ya asili, mitaji, ardhi, bahari na kila lile lililoko kwenye mazingira yake ili kumjegea maendeleo yake. UTU wa MTU ni "RASILIMALI MAMA" na Mazingira yake yanakuwa ni "RASILIMALI MAZINGIRA" ambazo zote kwa pamoja vinatupelekea kwenye Maendeleo ya Mtu kwenye Mazingira yake.
4. Isipokuwa kwa Mpinga Utu peke yake, hakuna mtu mwingne asiyejua kuwa bila rasilimali mama, rasilimali mazingira peke yake hugeuka na kuwa vyanzo vya magonjwa, vita, ufukara, ukandamizaji, ufisadi nk. Bila rasilimali mama (Utu wa Mtu kushika hatamu ya Jamii/Taifa) ambao ni ujulma wa utu wa jamii,
"Mazingira yanabadilika na kuwa chombo cha kumuadhibu Mt". Ni Mpaka Mbegu ya utu kifamilia na Kitaifa, itawale jamii husika ndipo Mazingira na rasilimali zake zote zinaweza kumuendeleza na Kumneemesha Mtu. Rasilimali mazingira na Madini yote ya thamani chini ya Utawala Usiozingatia UTU ambayo ndio rasilimali mama, Madini hayo yanakuwa vyanzo vya kustawisha wachache na pengine kuzua machafuko na vita kati ya "walikowa nacho" na wale "waliodhulumiwa" hivyo kubomoa na kuangamiza maendeleo kwa kila hali. Kunahitajika Azimio La UTU lililo IMARA kabisa na "
linaloendana na wakati kila wakati" ili Kunusuru UTU WA TAIFA usifanyiwe mzaha na kuchezewa na wapinga Utu, katika michakato yote ya kijamii ili kufikia maendeleo na ustawi wa jamii ya Kitanzania.
5. Kuwadhibiti wapinga Utu, ambao wakifanikiwa "kusoma" na "kuhodhi fedha" wanaweza kabisa kusambaratisha UTU Huru wa mtu kwenye jamii, Lazmia SASA Katiba ya nchi, Sheria za nchi, Miiko ya nchi, Maadil na Elimu ya nchi vione ukweli huu na vitamke rasmi kwa kuazmia, kama Taifa kuwapinga na kuwachukulia hatua zote za kuwatokomeza Wapinga UTU wa Taifa, ili kusitiri na kustawisha Utu wa familia, jamii na Taifa kwa ujumla! Nani haoni kwa sasa UTU wa jamii ulivyoshuka na Wapinga UTU
(Magugu MTU) walivyoshika Hatamu? Taifa sasa liamke na kutambua kwa undani unapotoka msukumo hasi wa kijamii unaodiriki kupinga kwa hali na mali thamani ya Utu huru kwenye jamii! Hii itatoa mwanga wa kutokufanyia mzaha Azimio Lolote La Utu litakalokuwepo kwenye WAKATI HUSIKA!
6. UTU HURU wa MTU uliokuwa ndio lengo letu la mwaka 1961, haupitwi na wakati, Ulikuwepo, Upo na Utakuwepo wakati wowote atakapokuwepo Mtu na Mazingira yake Tanzania na duniani. Kwa kuwa UTU unajieleleza kupitia kauli, fikra na matendo ya mtu ili kijipamabanisha na mazingira yake, ni hakika basi
muoenekano wa nje wa dhana ya Utu utakuwa unabadilika kwa vipindi mbalimbali kama ilivyo kweli kwa mabadiliko ya fikra, kauli , matedo na mabadiko ya mazingira ya Mtu, LAKINI KATU UTU NA THAMNI YAKE KAMWE HAVITABADILIKA NI ULE ULE NA UNAHITAJI UANGALIZI makini kupitia azimio sahihi dhidi ya wapinga Utu wakati wote.
7. Ni wendawazimu kufikiri kuwa Azimio la Utu, utafika wakati likatapitwa na wakati na kutotahitajika kabisa huku magugu Mtu yapo wakati wote katika jamii hiyohiyo. Hiyo itakuwa ni kweli tu wakati mwanadamu atakuwa ametoweka duniani. Kama ilivyo mimea shambani inayoshambuliwa na magugu wakati wote na kuhitaji palizi la mara kwa mara, ndivyo Azimio La Utu litakavyohitajika wakati wote na kila wakati likija na makali yanayolingana na aina ya magugu yaliyopo, kwani magugu nayo pia ni viumbe vinavyopambana na mazingira yake ili kujisitiri na kunedeleza vizazi vyao na kutokukubali kushindwa na kutoweka kirahisi kwenye uso wa dunia.
8. Mchunguze kwa makini MTU mwenye msukomo wa kupinga UTU wake, wa wenzake na wataifa lake. Kwa kuwa utu ndio msingi wa Uhai na maisha ya mtu, katika kuishi yaani "LIVE" na mpinga UTU anapinga KUISHI basi aitwe jina hili hili la "LIVE" lakini, spell it backward and what do you get!? Yes you r right ant humans are not animals they are
"LIVE" spelled backwards! Ingawa wengi wanapenda kutumia neno Fisadi, lakini utagundua kuwa jina la hawa watu linakwenda na wakati au vipindi na mazingira yao! Wakiwa urusi watakuwa na jina lao, wakiwa Kenya jina lao, wakiwa Tanzania jina lao wakiwa uingereza jina lao na jina linaweza kubadilika kulingana na nyakati jamii inapojikuta na kupitia!
9. Mjadala huu hautatupatia muafaka wa pamoja ni hakika! Na sifikiri kuwa ndio lengo lake. ILA Utafanikiwa
kutupembulia Makundi haya mawili muhimu ambayo yako kwenye jamii wakati wote na ambayo KUSIGANA KWAKE ndiko kuna "define" ustawi na maendeleo ya jamii ya Tanzania. Na kiuwkeli kabisa yangetakiwa yawe ndio chimbuko la Vyama Vya Upinzani na michaato muhimu ya kijamii.
10. Ni vema tuwe wakweli kabisa na kuona hatari ya Wapinga UTU wanapozidi kushamiri kama uyoga na kuiteka jamii. Hivyo lazima tuazimie bila kubabaisha na hatua za haraka zichukuliwe na bila mzaha kurejesha UTU WA TAIFA kwenye mikono salama. Tunahitaji Azimio La Utu Huru wa Mtu katika kukabiliana na mazingira yake katika "mtizamo mpya" Kwani ni kweli halipingiki Ili kuipata Tanzania tunayoikusudia!!!