Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

@W.J. Malecela. Azimio la Arusha bado lina mambo mazuri sana ya msingi kwa maendeleo ya taifa letu; ukitoa sehemu ya kwanza, sehemu za pili na tatu za azimio hilo bado zina mambo ambayo yana tija sana kwa taifa letu, mfano:

1. Suala la unyonyaji, azimio linasema hivi:

....... mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali hayapitani mno....uk.5

Sasa hapa mzee unataka kusema azimio ndio limetufikisha hapa, wakati lilisisitiza suala la kupinga unyonyaji?!

Pia...

......watu peke yao ambao huishi kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao, kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe...uk.5 (hii sehemu ya mwisho hata nchi zilizo kwenye mfumo wa ubepari, zina taratibu zenye elements kama hizo - mfano food stamps huko Marekani, na malipo ya kujikimu kwa nchi za Ulaya kama Uingereza)

2. Suala la kujitegemea.

Hapa azimio linasisitiza katika nchi kujitegemea na kuepuka kutegemea misaada kutoka mataifa mengine. Na mojawapo ya njia ya kufanikisha kujitegemea na kuongeza uwigo wa ukusanyi wa kodi..mfano azimio linasema:

Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi bila kutaka Ng’ombe akamuliwe tena...uk. 12-13

Azimio linasema kwa uwazi kabisa kwamba, serikali katika kujaribu kuepuka upanuzi wa ukusanyaji wa kodi, imejikita katika kutafuta na kupokea misaada ya kifedha toka ughaibuni (grants, unfairly conditioned loans and FDIs and aids). Azimio linasema kwa uwazi kabisa ni namna gani ilivyo ajabu na ujinga kutegemea fedha za nje kwa vile fedha hizo zinahatarisha uhuru wa kuamua mambo yetu (hii inajidhihirisha sasa hapa nchini; serikali haiwezi kufanya maamuzi bila kufikiri "wakubwa" watasemaje au watafikiriaje). Azimio linaongelea juu ya mikopo yenye masharti magumu ambayo licha ya kutokuwa na faida kwa taifa, pia inajenga mzigo mkubwa kwa watanzania wa sasa na wajao (hii pia inajidhihirisha sasa, kwani deni la taifa limekuwa kubwa kupita kiasi, huku serikali ikiendelea kukopa bila kufanya tathmini ya kina ya namna ya kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo ya taifa). Pia azimio linaongelea suala la uwekezaji wa watu kutoka nje (FDIs), uwekezaji ambao unaweka uchumi wa nchi mikononi mwa wageni, ambao wanapeleka faida za uwekezaji huo makwao (hii ni dhahiri kabisa hapa Tanzania, tunaona faida za uwekezaji katika madini, wanyamapori n.k. zikihamishwa kwenda kwenye nchi yanayotoka makampuni hayo. Na hakuna anayetaka kukumbuka mwongozo wa Azimio).

3. Suala la kumjali mkulima, azimio linasema

Ni dhahiri kwamba watanzania wengi wanaishi vijijini, ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo. Hivyo bila kuweka jitihada za kipekee katika kumjali mkulima hakika, maendeleo yatakuwa ndoto. Nchi zote zilizoendelea, zilisukumwa na kazi na shughuli za watu walioishi vijiji; maendeleo ya viwanda Ulaya licha ya kunufaika na ukoloni, watu wa vijijini na shughuli zao walikuwa driving forces za maendeleo hayo. Vivyo hivyo Marekani, watu walioishi vijijini pamoja na shughuli zao ndiyo walio sukuma maendeleo katika nchi hizo. Sasa kama taifa haliweki vipaumbele kwenye sehemu ambayo ndiyo moyo wa taifa, taifa litakuwa linapiga mark time tu.Ni ajabu na jambo la kusikitisha sana kwamba taifa halijafanikiwa katika hili, kwani sasa msisitizo upo katika diplomasia ya kiuchumi, ambapo uwekezaji mkubwa ndiyo unaotegemewa kusukuma gurudumu la maendeleo, huku wakulima wengi wakitegemewa kuwa outgrowers kupitia kwenye huo mfumo. Hii nayo imejidhihirisha hapa Tanzania, ambapo kuna wimbi la land grabbing linaondelea sasa, huku wimbo wa Kilimo Kwanza nao ukiimbwa!! Seriously, kwa utaratibu huo, watanzania wengi (wakulima) watanufaika kweli na Kilimo Kwanza?!

4. Suala la misingi ya maendeleo, azimio linatilia mkazo katika:

....ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora....uk. 28-31

Mzee hata katika hili unaona Azimio limetufikisha hapa? Seriuosly?

Ardhi na watu, taifa limejitosheleza katika hayo. Tatizo lipo kwenye siasa safi na uongozi bora (hapa ndipo miiko ya uongozi inapo-make sense). Siasa inayotawala sasa ni siasa uchwara; uongozi nao ni kama vile haupo. Kwani hakuna uwajibikaji, serikali haijali shida za wananchi, uongozi wa umma umekuwa sehemu ya kwenda kuchuma pesa na kujitajirisha, viongozi hawana tena morals zinakujivunia mbele ya wananchi. Sasa mtu ambaye hana hata ufahamu na uelewa wa nini maana ya kuwa kiongozi wa umma, wanachaguliwa na kupewa vyeo vikubwa. Tunaona mtu ambaye hana mbele wala nyuma katika mambo ya uongozi anaweza kuwa mbunge, waziri, mkuu wa mkoa/wilaya n.k. Viongozi wa umma wanaishi na kunufaika kwa jasho la walipa kodi, bila kujali kodi hizo zinaleta manufaa kwa watu wote. Pato la taifa linafaidiwa na wachache waliopo kwenye "mamlaka" n.k. Vijana wengi "wanazurura hovyo bila ajira" (vijana hawa wanajifariji kwa kujipa ajira zinazosemwa zisizo rasmi), viongozi wanatuma polisi wenye marungu na bomu ya machozi kuwanyanyasa vijana hao, badala ya kutafuta suluhisho la kudumu. Hali ya siasa na uongozi imekuwa mbaya kiasi kwamba raia nao sasa wanawaza "kupiga" tu popote pale walipo ili nao wajinufaishe na keki ya taifa, inayoliwa na watu wachache walio kwenye "mamlaka".

Sasa mkuu @W.J. Malecela, unapokuja na wazo kwamba Azimio la Arusha ndilo lililotufikisha hapa, bila kuzingatia yale mazuri ya azimio hilo, naamini unakosea mzee. Pengine ni kweli kwamba kuna vitu ambavyo haviko relevant na hali ya sasa ya Tanzania, lakini ni ajabu vile vile kulitupa azimio lote kwa kudai halina manufaa yoyote.

Na elewa kwamba toka taifa limeanzisha kuchanganya mambo ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar, ndipo mambo yalipoanza kwenda kombo. Serikali ikapuuzia yale mazuri ya Azimio la Arusha, "ikalichinjia baharini", na ikafikiria tu mabaya ya azimio hilo; mwisho wa siku mambo ndiyo yakaanza kwenda shaghalabaghala.

Lete hoja ya kujadili namna gani tuliboreshe azimio hilo (kwa kuweka mambo yaliyo na maana kwa sasa) kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Well, heshima mbele sana JF,

- Ninaomba kusema tena na tena, we were Dead wrong na idea za Azimio La Arusha, infact ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama hili taifa, hatujui tunakokwenda wala tulikotoka. Halafu wanatokea wasomi wanaodai eti turudi kwenye Azimio, hilo Azimio limetushinda mwanzoni kwa nini kuna wanaoamini tutaliweza sasa?

- Recently, nimeona wale wengi walioachwa kwenye uongozi wa juu yaani kwenye mlo, wakililia Azimio, halafu ninachukizwa sana ninapoona media inawapa free lunch hawa waliokosa mlo, sijawahi kuwasikia wakisema Azimio liliwahi kumfunga kiongozi gani wa juu mwizi, sijawasikia wakisema Azimio lilifanya nini cha maaana mpaka wanalilia!

- Mwalimu, yes was the greatest ever, lakini Mwalimu alikuwa na mapungufu makubwa mawili, hakujua;- !. Uchumi 2. Sheria, hivi vitu viwili Mwalimu simply hakuvijua kama alivijiua basi hakuvitilia maanani, na ndivyo vinavyolitafuna taifa letu sasa akiwa hayupo!

- WA-TANZANIA, KAMA TUNATAKA KUSONGA MBELE NA KIJIREKEBISHA TUACHANE NA MANENO YA AZIMIO LA ARUSHA, KWA SABABU NDILO HASA LIMETURUDISHA NYUMA SANA, LISIRUDI, LIENDE ZAKE, NA TUSILIJADILI MAANA NI SHETANI LILILOTURUDISHA NYUMA SANA, SASA TWENDE MBELE NA UBEPARI NA UTAWALA UNAOHESHIMU SHERIA NDIO THE BEST WAY MBELE!

RESPECT PEOPLE!

Mr. Willie @DSM City!

Naamini pasipo shaka mmoja wa walionufaika sana na azimio la arusha ni pamoja na Mzee Malecela. Yeye alitumia nguvu zake tena akiwa kijana kabisa kuhakikisha wanasimamisha vijiji vya ujamaa tena kwa gharama kubwa kabisa ya mali na hata maisha.
Kusema ukweli, kwangu mimi Mwalimu hakutakiwa kuwa mtaalamu wa kila kitu. Hata Azimio la Arusha alipolitangaza, wale walioamini katika siasa zile walitakiwa kuhakikisha wanatoa support ili lengo liweze kutimizwa. Badala yake mwalimu alikuwa na watu wenye agenda mbili. Huku kidumu chama cha mapinduzi na siasa zake, na upande mwingine kwanini tusiige mabepari.

Yes in 1990 we made a fundamental shift from Azimio la Arusha...hatukujua kila system lazima iwe na balance and check? Kwangu mimi tatizo sio Azimio la Arusha...tatizo ni double standard zetu ambazo hata tukipewa azimio kutoka popote pale katika ulimwengu huu hatutaweza kufanikiwa. Thinking is a process and we have to engage our minds in drafting dos and donts and stick hard to them.
Otherwise, kila kizazi na mambo yake...yetu ni ubabaishaji, double standards, deal na biashara zisizo na utaratibu, wizi wa mali ya umma...you name it.
 
@W.J. Malecela. Azimio la Arusha bado lina mambo mazuri sana ya msingi kwa maendeleo ya taifa letu; ukitoa sehemu ya kwanza, sehemu za pili na tatu za azimio hilo bado zina mambo ambayo yana tija sana kwa taifa letu, mfano:

1. Suala la unyonyaji, azimio linasema hivi:

....... mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali hayapitani mno....uk.5

Sasa hapa mzee unataka kusema azimio ndio limetufikisha hapa, wakati lilisisitiza suala la kupinga unyonyaji?!

Pia...

......watu peke yao ambao huishi kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao, kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe...uk.5 (hii sehemu ya mwisho hata nchi zilizo kwenye mfumo wa ubepari, zina taratibu zenye elements kama hizo - mfano food stamps huko Marekani, na malipo ya kujikimu kwa nchi za Ulaya kama Uingereza)

2. Suala la kujitegemea.

Hapa azimio linasisitiza katika nchi kujitegemea na kuepuka kutegemea misaada kutoka mataifa mengine. Na mojawapo ya njia ya kufanikisha kujitegemea na kuongeza uwigo wa ukusanyi wa kodi..mfano azimio linasema:

Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi bila kutaka Ng'ombe akamuliwe tena...uk. 12-13

Azimio linasema kwa uwazi kabisa kwamba, serikali katika kujaribu kuepuka upanuzi wa ukusanyaji wa kodi, imejikita katika kutafuta na kupokea misaada ya kifedha toka ughaibuni (grants, unfairly conditioned loans and FDIs and aids). Azimio linasema kwa uwazi kabisa ni namna gani ilivyo ajabu na ujinga kutegemea fedha za nje kwa vile fedha hizo zinahatarisha uhuru wa kuamua mambo yetu (hii inajidhihirisha sasa hapa nchini; serikali haiwezi kufanya maamuzi bila kufikiri "wakubwa" watasemaje au watafikiriaje). Azimio linaongelea juu ya mikopo yenye masharti magumu ambayo licha ya kutokuwa na faida kwa taifa, pia inajenga mzigo mkubwa kwa watanzania wa sasa na wajao (hii pia inajidhihirisha sasa, kwani deni la taifa limekuwa kubwa kupita kiasi, huku serikali ikiendelea kukopa bila kufanya tathmini ya kina ya namna ya kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo ya taifa). Pia azimio linaongelea suala la uwekezaji wa watu kutoka nje (FDIs), uwekezaji ambao unaweka uchumi wa nchi mikononi mwa wageni, ambao wanapeleka faida za uwekezaji huo makwao (hii ni dhahiri kabisa hapa Tanzania, tunaona faida za uwekezaji katika madini, wanyamapori n.k. zikihamishwa kwenda kwenye nchi yanayotoka makampuni hayo. Na hakuna anayetaka kukumbuka mwongozo wa Azimio).

3. Suala la kumjali mkulima, azimio linasema

Ni dhahiri kwamba watanzania wengi wanaishi vijijini, ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo. Hivyo bila kuweka jitihada za kipekee katika kumjali mkulima hakika, maendeleo yatakuwa ndoto. Nchi zote zilizoendelea, zilisukumwa na kazi na shughuli za watu walioishi vijiji; maendeleo ya viwanda Ulaya licha ya kunufaika na ukoloni, watu wa vijijini na shughuli zao walikuwa driving forces za maendeleo hayo. Vivyo hivyo Marekani, watu walioishi vijijini pamoja na shughuli zao ndiyo walio sukuma maendeleo katika nchi hizo. Sasa kama taifa haliweki vipaumbele kwenye sehemu ambayo ndiyo moyo wa taifa, taifa litakuwa linapiga mark time tu.Ni ajabu na jambo la kusikitisha sana kwamba taifa halijafanikiwa katika hili, kwani sasa msisitizo upo katika diplomasia ya kiuchumi, ambapo uwekezaji mkubwa ndiyo unaotegemewa kusukuma gurudumu la maendeleo, huku wakulima wengi wakitegemewa kuwa outgrowers kupitia kwenye huo mfumo. Hii nayo imejidhihirisha hapa Tanzania, ambapo kuna wimbi la land grabbing linaondelea sasa, huku wimbo wa Kilimo Kwanza nao ukiimbwa!! Seriously, kwa utaratibu huo, watanzania wengi (wakulima) watanufaika kweli na Kilimo Kwanza?!

4. Suala la misingi ya maendeleo, azimio linatilia mkazo katika:

....ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora....uk. 28-31

Mzee hata katika hili unaona Azimio limetufikisha hapa? Seriuosly?

Ardhi na watu, taifa limejitosheleza katika hayo. Tatizo lipo kwenye siasa safi na uongozi bora (hapa ndipo miiko ya uongozi inapo-make sense). Siasa inayotawala sasa ni siasa uchwara; uongozi nao ni kama vile haupo. Kwani hakuna uwajibikaji, serikali haijali shida za wananchi, uongozi wa umma umekuwa sehemu ya kwenda kuchuma pesa na kujitajirisha, viongozi hawana tena morals zinakujivunia mbele ya wananchi. Sasa mtu ambaye hana hata ufahamu na uelewa wa nini maana ya kuwa kiongozi wa umma, wanachaguliwa na kupewa vyeo vikubwa. Tunaona mtu ambaye hana mbele wala nyuma katika mambo ya uongozi anaweza kuwa mbunge, waziri, mkuu wa mkoa/wilaya n.k. Viongozi wa umma wanaishi na kunufaika kwa jasho la walipa kodi, bila kujali kodi hizo zinaleta manufaa kwa watu wote. Pato la taifa linafaidiwa na wachache waliopo kwenye "mamlaka" n.k. Vijana wengi "wanazurura hovyo bila ajira" (vijana hawa wanajifariji kwa kujipa ajira zinazosemwa zisizo rasmi), viongozi wanatuma polisi wenye marungu na bomu ya machozi kuwanyanyasa vijana hao, badala ya kutafuta suluhisho la kudumu. Hali ya siasa na uongozi imekuwa mbaya kiasi kwamba raia nao sasa wanawaza "kupiga" tu popote pale walipo ili nao wajinufaishe na keki ya taifa, inayoliwa na watu wachache walio kwenye "mamlaka".

Sasa mkuu @W.J. Malecela, unapokuja na wazo kwamba Azimio la Arusha ndilo lililotufikisha hapa, bila kuzingatia yale mazuri ya azimio hilo, naamini unakosea mzee. Pengine ni kweli kwamba kuna vitu ambavyo haviko relevant na hali ya sasa ya Tanzania, lakini ni ajabu vile vile kulitupa azimio lote kwa kudai halina manufaa yoyote.

Lete hoja ya kujadili namna gani tuliboreshe azimio hilo (kwa kuweka mambo yaliyo na maana kwa sasa) kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

SEHEMU YA KWANZA
Imani ya Tanu
SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA

IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII

Soma hapo juu. Azimio la Arusha ni Imani ya chama cha TANU. Chama hicho hakipo, na sisi wengine ni wanachama wa CHADEMA, CUF au TLP. Hivyo kwanini mnataka hoja ya chama kimoja iwe ya nchi zima?

Kamanda, jamaa huwa anchukua maneno bar na kwenye vijiwe na kuleta bila fact wala research

Muulize amelisoma azimio la arusha?? na chanzo ni document au implementation au change of our own policies??

Muhimu zaidi ange declare interest kwanza kwa mfano mzee malecela kutofautiana na Baba wa Taifa miaka ya hapo katikati nyuma, vinginevyo bila ya kujenga hoja, anajiweka katika wakati mgumu sana na ndio maana majibu ya wadau wengi juu ya hoja yake yanamhoji zaidi kuliko kujadili hoja aliyotoa.
 
- Mkuu ninaomba nikjibu kwa niaba ya wengine wote, hoja ikianza na baba au Mzeee Malecela, huwa nina tabia ya kuidharau kwamba hakuna hoja hapo, ninasema hivi Azimio la Arusha ndilo limetufikisha hapa tulipo, halikuwa na anything good in it zaidi tu ya kusadikika na majungu majungu ya kuwaonea wale waliokuwa hawalitaki na wana sababu za msingi, ni Azimio ndilo lililua viwanda vyetu na mashirika ya umma kwa sababu Azimio ndilo liliwa-empower wenyeviti wa chama kwenye viwanda na mashirika, na kuwaacha wataaalamu wakiwapigia magoti viongozi wa siasa kwenye uchumi, sihitaji research ya anything kujua kwamba under Azimio viwanda kama vya Sigara na bia vilikuwa vinaleta hasara!

- Now people unaweza kunishambulia as much as you want, lakini one thing is huwezi kupangua hoja kwamba Azimio was the waste of our time na hasa resources kwa sababu lilikuwa linashabikia sana majungu kuliko kazi, wananchi wengi kwa kulitumia Azimio wameishia kwua wavivu wa kusubiri Serikali iwafanyie kila kitu, sasa tumekwama sasa mnaanza kulilia turudi kwenye Azimio, mawazo ya kitumwa kwamba mpaka leo tumeshindwa kufikiria new ideas,

- Sina muda wa kusoma failing ideas za Azimio, ni waste of my time sasa ni wakati wa kusonga mbele na Ubepari, na utawala unaoheshimu sheria, hakuna Azimio tena wale wote mnaolilia Azimio ni smply hamuweziz kufikiria nje ya Maazimio ya Arusha, maana ndio hasa iliyokuwa nia na madhumuni yake yaani kuwafanya msifikirie nje ya Azimio,

- Mungu atunusuru sana hili taifa na mawazo mufilisi haya ya Azimio, maana yataishia kuturiudisha kwenye mwananchi kwua na pikipiki tu ni dhambi, I mean nashangaa great thinkers kulilia kwamba Azimio ni sawa na kuleta misahafu hapa na articles na kujifanya wasomi sana na failing ideas, please keep hizo artcile zenu, hilo Azimio lilishindwa then haliwezi sasa ni simply out of touch na maisha tuliyonayo sasa,

- Mimi nikivua nguo na wewe ukivua wote tunakuwa sawa, sasa nionyeshe kwamba wewe uliyevaa ni what you are kuliko kulia lia na hoja mufilisi, ninsema tena mambo ya Azimio la Arusha, ndio ymetufkisha hapa, hatujui tulikotoka wala tunakokwenda, ninawaomba tusirudie tena maneno ya Azimio la Arusha, kwa sababu hakuna popote penye ushahidi hata mmoja tu kwamba ulifaaa kila mahali Tanzania utajionea madhara yake, huzuni sana kwa mnaolilia Azimio ni simply kwamba hamuwezi kufikiria nje ya box la Azimio which was how it was design kwamba usiulize ubaya wake ukiuliza ni kuswekwa rumande, sasa mpaka leo tupo huru bado mnaogopa kuuliza ubaya wake na huku wote mnayo macho ya kuona madhara makubwa sana tuliyonayo!

William.
 
Mkuu ninaomba nikjibu kwa niaba ya wengine wote, hoja ikianza na baba au Mzeee Malecela, huwa nina tabia ya kuidharau kwamba hakuna hoja hapo, ninasema hivi Azimio la Arusha ndilo limetufikisha hapa tulipo, halikuwa na anything good in it zaidi tu ya kusadikika na majungu majungu ya kuwaonea wale waliokuwa hawalitaki na wana sababu za msingi, ni Azimio ndilo lililua viwanda vyetu na mashirika ya umma kwa sababu Azimio ndilo liliwa-empower wenyeviti wa chama kwenye viwanda na mashirika, na kuwaacha wataaalamu wakiwapigia magoti viongozi wa siasa kwenye uchumi, sihitaji research ya anything kujua kwamba under Azimio viwanda kama vya Sigara na bia vilikuwa vinaleta hasara!
.

Kaka yangu William,

Kwanza suala la majungu ni ‘timeless', lakini muhimu zaidi ni kwamba sio sahihi kuitumia kujadili suala muhimu kama azimio la arusha, kufanya hivyo ni kuishiwa hoja. Ni muhimu pia ukafahamu kwamba waliokuwa wanalikataa azimio la arusha ilikuwa ni viongozi ambao wao walitegemea kufaidika binafsi baada ya uhuru kwani walikuwa wanawakodolea macho wanzao nchi jirani kina njonjo n.k na kutaka kuiga tabia zao. Fanya utafiti, utagundua haraka sana kwamba Mwalimu embraced azimio la arusha baada ya kugundua kwamba wananchi walikuwa na hamu ya kuona matunda ya uhuru kwani walishapewa ahadi nyingi sana. Usikae na wazee kuadithiwa kuhusu nani alikuwa anapinga azimio la arusha na kwa sababu zipi, jaribu uwe na mtazamo wa kijamii zaidi, hasa kwa kuelewa historia ya nchi yetu.

Kuhusu suala la Mzee Malecela, hauwezi kutenganishwa na mzee wetu huyu kwa kumkwepa kiholela holela kama unavyofanya hivi sasa. Huyu ni mzee wetu muhimu na tunae mheshimu sana, kwani ni mmoja wa wazee walioijenga nchi yetu na Mwalimu bega kwa bega a pia katika awamu za baadae. Unachotakiwa kufanya ni ku declare interest na kuonyesha unasimamia wapi kwa hoja, na ukifanya hivyo mara moja tu, sidhani kama utahusishwa na Mzee Malecela tena katika mijadala.

Kusema kwamba hauitaji research ili kujua jinsi gani azimio la arusha liliua viwanda nadhani unajiweka katika wakati mgumu sana kujenga hoja yako kwani research ndogo tu itakuonyesha jinsi gani Tanzania ilifanikiwa kiuchumi kupitia viwanda chini ya azimio la arusha, na kama nchi, hatujawahi tena kufikikisha viwanda vyetu kwenye kiwango cha 12% ya GDP. Baada ya mwaka 1985, viwanda as a percentahe of GDP haijawahi kuvuka 10%. Na wewe kuchagua viwanda vya Sigara (TCC) na Bia (TBL) kama mfano inaonyesha jinsi gani usivyokuwa makini kwani hivyo ni viwanda pekee ambavyo vilikuwa vinaendeshwa kwa faida mpaka siku ya mwisho vilipo kuja binaifisishwa na Rais Mkapa.

Now people unaweza kunishambulia as much as you want, lakini one thing is huwezi kupangua hoja kwamba Azimio was the waste of our time na hasa resources kwa sababu lilikuwa linashabikia sana majungu kuliko kazi, wananchi wengi kwa kulitumia Azimio wameishia kwua wavivu wa kusubiri Serikali iwafanyie kila kitu, sasa tumekwama sasa mnaanza kulilia turudi kwenye Azimio, mawazo ya kitumwa kwamba mpaka leo tumeshindwa kufikiria new ideas

Sidhani kama kuna mtu anaye kushambulia. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba haujengi hoja juu ya kwanini ‘Azimio la Arusha' was a wrong move, na badala yake unatumia muda wako mwingi kutuona mazuzu sisi tunao amini kwamba azimio hili bado lina nafasi ya kutupeleka mbele iwapo litafanyiwa marekebisho. Nikuambie tu kwamba ili uweze ku ‘assess' how well Azimio la Arusha fared as a policy, ni muhimu uliweke side by side with comparative schemes, especially Structural Adjustment Programmes under the World Bank and the IMF. Tuwekee takwimu na jenga hoja kwanini unadhani mtanzania was 1967 – 1985 (miaka 18 ya ujamaa) alikuwa worse off ukimfananisha na mtanzania wa 1986 – 2012 (miaka 26 ya soko huria). Uchambuzi wako utajitosheleza zaidi iwapo utajikita kujadili trade-offs baina na ‘economic growth' na ‘social justice' katika vipindi hivi viwili. Nasubiri mawazo yako katika hili.

Sina muda wa kusoma failing ideas za Azimio, ni waste of my time sasa ni wakati wa kusonga mbele na Ubepari, na utawala unaoheshimu sheria, hakuna Azimio tena wale wote mnaolilia Azimio ni smply hamuweziz kufikiria nje ya Maazimio ya Arusha, maana ndio hasa iliyokuwa nia na madhumuni yake yaani kuwafanya msifikirie nje ya Azimio.

Nadhani hili ni tatizo la kifikra kwani wapo wengi wanaopingana na sehemu kubwa ya azimio la arusha pamoja kwamba wengine pia ni wajamaa, kwa mfano Prof. Shivji, lakini wanafanya hivyo kwa kujadili mapungufu yake from an objective point of view na kutuelewesha kwa hoja, sio kama wewe unavyofanya na kuwa subjective right from the let go na kutamka bila kufikiria mara mbili mbili kwamba "Sina muda wa kusoma failing ideas za Azimio la Arusha.' Ndio maana unapungukiwa hoja. Na kwa taarifa yako, Azimio la Arusha did not fail; Azimio la Arusha was ‘failed'.

Mungu atunusuru sana hili taifa na mawazo mufilisi haya ya Azimio, maana yataishia kuturiudisha kwenye mwananchi kwua na pikipiki tu ni dhambi, I mean nashangaa great thinkers kulilia kwamba Azimio ni sawa na kuleta misahafu hapa na articles na kujifanya wasomi sana na failing ideas, please keep hizo artcile zenu, hilo Azimio lilishindwa then haliwezi sasa ni simply out of touch na maisha tuliyonayo sasa
.

Nadhani watanzania wengi leo hii wanamhitaji Mungu kutunusuru zaidi na tunapokwenda kuliko tulipotoka, je unapingana na hoja hii? Ni muhimu ukaachana na mawazo kwamba maendeleo yetu ni ‘path dependent.' Kuna msemo unasema ‘usione vinaelea, ujue vimeundwa'. Unayo yaona Ulaya na Marekani hayaji kwa kuiga. Na usitazame nchi kama South Korea na wengine pale wanaoitwa ‘tigers' ukadhania na sisi tutafika huko just by embracing hayo unayo sisitiza ‘Ubeparia na Utawala unaofuata Sheria'. Ni muhimu ukatambua kwamba Development is not path dependent and Mwalimu aligundua hilo mapema kabisa.
Inaonyesha wewe ni muumini wa soko huria per se na kwa ushabiki zaidi kwani haujadili kabisa mapungufu ya mfumo huu ulioletwa kiholela relative to mfumo unaopingana nao. Kama unadhani mawazo ya azimio la arusha ni mufilisi, mawazo ya soko huria ni mawazo mufilisi zaidi, especially kwa vile ni mawazo ya kuiga. Sidhani kama ni sahihi kuita mawazo ya azimio la arusha kwamba ni mufilisi hasa ukizingatia kwamba Azimio hili lilitambua kwamba gifts and loans ilikuwa ni sumu ya uhuru wetu na vitu vya kudhoofisha na kuingilia juhudi zetu za kuwa taifa linalo lenga kujitegemea. Nini mufilisi katika lengo noble kama hili? Wanaotaka tulirudie azimio la arusha sio kwamba wanataka lirudiwe kama lilivyo bali kwa kufanyiwa marekebisho.

Mimi nikivua nguo na wewe ukivua wote tunakuwa sawa, sasa nionyeshe kwamba wewe uliyevaa ni what you are kuliko kulia lia na hoja mufilisi, ninsema tena mambo ya Azimio la Arusha, ndio ymetufkisha hapa, hatujui tulikotoka wala tunakokwenda, ninawaomba tusirudie tena maneno ya Azimio la Arusha, kwa sababu hakuna popote penye ushahidi hata mmoja tu kwamba ulifaaa kila mahali Tanzania utajionea madhara yake, huzuni sana kwa mnaolilia Azimio ni simply kwamba hamuwezi kufikiria nje ya box la Azimio which was how it was design kwamba usiulize ubaya wake ukiuliza ni kuswekwa rumande, sasa mpaka leo tupo huru bado mnaogopa kuuliza ubaya wake na huku wote mnayo macho ya kuona madhara makubwa sana tuliyonayo!

Katika mabaya ya azimio la arusha wewe ulicho ona ni suala la watu kuwekwa rumande peke yake? Wangapi leo hii wanawekwa ndani leo kwa kuiba kuku wakati walioiba mali ya umma bado wanapeta mitaani huku wakilindwa na usalama unaolipwa posho na mishahara ya wenye mali zilizoibwa (walipa kodi)? Nini mtazamo wako kuhusu madhara ya soko huria leo hii ambapo imekuwa ni jambo la kawaida kwa mamilioni ya watanzania kushindwa kujipatia mlo zaidi ya mmoja kwa siku? Je, una maoni gani juu ya ufisadi unao litafuna taifa hivi sasa chini ya Azimio la Zanzibar ambalo majizi ndani ya CCM yalilipitisha ili kuhalalisha mali za umma walizoiba? Uchwara huu haukupewa nafasi chini ya Azimio la Arusha na hilo unalitambua fika.

Kwa kauli kama hizi, binafsi nadhani upeo wako juu ya Tumetoka Wapi, Tupo Wapi, na Twende Wapi kama taifa umefikia tamati. Na nadhani vijana wenzako wengi watakubaliana na mimi. Binafsi nadhani unakabiliwa na mambo mawili: Aidha hauna uelewo wa taifa lako au hauna uzalendo na taifa lako. Otherwise, please prove me wrong.
 
Well, heshima mbele sana JF,

- Ninaomba kusema tena na tena, we were Dead wrong na idea za Azimio La Arusha, infact ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama hili taifa, hatujui tunakokwenda wala tulikotoka. Halafu wanatokea wasomi wanaodai eti turudi kwenye Azimio, hilo Azimio limetushinda mwanzoni kwa nini kuna wanaoamini tutaliweza sasa?

- Recently, nimeona wale wengi walioachwa kwenye uongozi wa juu yaani kwenye mlo, wakililia Azimio, halafu ninachukizwa sana ninapoona media inawapa free lunch hawa waliokosa mlo, sijawahi kuwasikia wakisema Azimio liliwahi kumfunga kiongozi gani wa juu mwizi, sijawasikia wakisema Azimio lilifanya nini cha maaana mpaka wanalilia!

- Mwalimu, yes was the greatest ever, lakini Mwalimu alikuwa na mapungufu makubwa mawili, hakujua;- !. Uchumi 2. Sheria, hivi vitu viwili Mwalimu simply hakuvijua kama alivijiua basi hakuvitilia maanani, na ndivyo vinavyolitafuna taifa letu sasa akiwa hayupo!

- WA-TANZANIA, KAMA TUNATAKA KUSONGA MBELE NA KIJIREKEBISHA TUACHANE NA MANENO YA AZIMIO LA ARUSHA, KWA SABABU NDILO HASA LIMETURUDISHA NYUMA SANA, LISIRUDI, LIENDE ZAKE, NA TUSILIJADILI MAANA NI SHETANI LILILOTURUDISHA NYUMA SANA, SASA TWENDE MBELE NA UBEPARI NA UTAWALA UNAOHESHIMU SHERIA NDIO THE BEST WAY MBELE!

RESPECT PEOPLE!

Mr. Willie @DSM City!

Mkuu Willie,

Kwa yale niliyonayo Azimio la Arusha lilikuja kwa sababu za kisiasa. Lakini kwa mtanzania yoyote mwenye upeo mzuri na akili timamu hawezi kukaa na kulitetea Azimio hilo.

Tanganyika ilipokuwa inapigania uhuru, kulikuwa na mambo mengi ambayo TANU ilitoa ahadi kuyafanya mara baada ya kupata uhuru. Lakini mambo hayo yaliitaji pesa na viongozi wa TANU walikuwa hawajui kuendesha nchi wala bajeti.

Uhuru ulipopatikana, wananchi wakaanza kusubiri kutimiziwa ahadi zao. Lakini kutokana na uhaba wa pesa, TANU ilikuwa nyuma kutekeleza ahadi hizo. Lakini wakati huo huo TANU inashindwa kutimiza ahadi zake, viongozi wa juu walikuwa wanaishi maisha ya kifahari kama wakoloni.

Hivyo TANU kurudisha umaarufu wake kama ule uliopata wakati wa uhuru ilihamua kutangaza Azimio hili. Na vilevile hili serikali ya TANU ipate pesa ya kutimiza ahadi zake, ulihamua kutaifisha mali za wawekezaji. Mfano huu uliigwa kutoka nchi kama Misri iliyoweza kutaifisha Suez Canal hili kujiongezea mapato yake. Hivyo hakuna jipya ambalo Azimio la Arusha lilileta.

Kwenye vipengere vya haki za binadamu, hizo ni haki zilizopo kwenye Tangazo la umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu. Viongozi wa TANU hawakutoa chochote kipya zaidi ya ku-copy and paste.

Na wameshindwa vibaya kwenye haki hizo. Azimio linatoa haki ya kutoa mawazo. Haki za kumiliki mali. Haki ya kushiriki kwenye shughuli za kisiasa. Wakati huo huo viongozi waliotunga Azimio hilo walilazimisha watu kuhamia kwenye vijiji vya Ujamaa bila mapenzi yao na kupoteza mali zao.

Tukurudi kwenye mafanikio ya Azimio la Arusha. Ukweli data zote zinaonyesha kuwa halikuwa na mafanikio yoyote yale. Rasimali zilizotaifishwa kama vile mashamba ya mkonge yalishindwa kuendelea.

Mfanikio ya elimu, afya, na maji hayakuletwa na Azimio la Arusha. Ni mipango ya World Bank, IMF, and donor countries. Hata nchi ambazo hazikuwa na Azimio la Arusha zilipata misaada hiyo. Mojawapo Zambia.

Kuhusiana na viwanda vilivyomilikiwa na serikali, vilevile ni mipangoa ya World Bank, IMF, and donor countries. Zaire, Zambia, Kenya n.k zilikuwa na viwanda vinavyomilikiwa na serikali.

Azimio la Arusha ni beneficiary tu wa siasa za kidunia zilizokuwepo miaka ya 60, 70, mwanzoni mwa 80. Na bila kuwepo siasa hizi za kiduani, Azimio la Arusha lisingeweza kuendesha hata kiwanda cha miswaki ya vijiti. Na nashangaa msomi kama Shivji anatoa mfano wa kiwanda cha Urafiki kuonyesha mafanikio ya Azimio la Arusha. Wachina walijenga kiwanda hicho kueneza siasa zao za mambo ya nje. Na matokeo yake wamepata kiti katika baraza la umoja wa mataifa na kura ya veto.
 
.

Kaka yangu William,

Kwanza suala la majungu ni ‘timeless', lakini muhimu zaidi ni kwamba sio sahihi kuitumia kujadili suala muhimu kama azimio la arusha, kufanya hivyo ni kuishiwa hoja. Ni muhimu pia ukafahamu kwamba waliokuwa wanalikataa azimio la arusha ilikuwa ni viongozi ambao wao walitegemea kufaidika binafsi baada ya uhuru kwani walikuwa wanawakodolea macho wanzao nchi jirani kina njonjo n.k na kutaka kuiga tabia zao. Fanya utafiti, utagundua haraka sana kwamba Mwalimu embraced azimio la arusha baada ya kugundua kwamba wananchi walikuwa na hamu ya kuona matunda ya uhuru kwani walishapewa ahadi nyingi sana. Usikae na wazee kuadithiwa kuhusu nani alikuwa anapinga azimio la arusha na kwa sababu zipi, jaribu uwe na mtazamo wa kijamii zaidi, hasa kwa kuelewa historia ya nchi yetu.

Kuhusu suala la Mzee Malecela, hauwezi kutenganishwa na mzee wetu huyu kwa kumkwepa kiholela holela kama unavyofanya hivi sasa. Huyu ni mzee wetu muhimu na tunae mheshimu sana, kwani ni mmoja wa wazee walioijenga nchi yetu na Mwalimu bega kwa bega a pia katika awamu za baadae. Unachotakiwa kufanya ni ku declare interest na kuonyesha unasimamia wapi kwa hoja, na ukifanya hivyo mara moja tu, sidhani kama utahusishwa na Mzee Malecela tena katika mijadala.

Kusema kwamba hauitaji research ili kujua jinsi gani azimio la arusha liliua viwanda nadhani unajiweka katika wakati mgumu sana kujenga hoja yako kwani research ndogo tu itakuonyesha jinsi gani Tanzania ilifanikiwa kiuchumi kupitia viwanda chini ya azimio la arusha, na kama nchi, hatujawahi tena kufikikisha viwanda vyetu kwenye kiwango cha 12% ya GDP. Baada ya mwaka 1985, viwanda as a percentahe of GDP haijawahi kuvuka 10%. Na wewe kuchagua viwanda vya Sigara (TCC) na Bia (TBL) kama mfano inaonyesha jinsi gani usivyokuwa makini kwani hivyo ni viwanda pekee ambavyo vilikuwa vinaendeshwa kwa faida mpaka siku ya mwisho vilipo kuja binaifisishwa na Rais Mkapa.

Sidhani kama kuna mtu anaye kushambulia. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba haujengi hoja juu ya kwanini ‘Azimio la Arusha' was a wrong move, na badala yake unatumia muda wako mwingi kutuona mazuzu sisi tunao amini kwamba azimio hili bado lina nafasi ya kutupeleka mbele iwapo litafanyiwa marekebisho. Nikuambie tu kwamba ili uweze ku ‘assess' how well Azimio la Arusha fared as a policy, ni muhimu uliweke side by side with comparative schemes, especially Structural Adjustment Programmes under the World Bank and the IMF. Tuwekee takwimu na jenga hoja kwanini unadhani mtanzania was 1967 – 1985 (miaka 18 ya ujamaa) alikuwa worse off ukimfananisha na mtanzania wa 1986 – 2012 (miaka 26 ya soko huria). Uchambuzi wako utajitosheleza zaidi iwapo utajikita kujadili trade-offs baina na ‘economic growth' na ‘social justice' katika vipindi hivi viwili. Nasubiri mawazo yako katika hili.

Nadhani hili ni tatizo la kifikra kwani wapo wengi wanaopingana na sehemu kubwa ya azimio la arusha pamoja kwamba wengine pia ni wajamaa, kwa mfano Prof. Shivji, lakini wanafanya hivyo kwa kujadili mapungufu yake from an objective point of view na kutuelewesha kwa hoja, sio kama wewe unavyofanya na kuwa subjective right from the let go na kutamka bila kufikiria mara mbili mbili kwamba "Sina muda wa kusoma failing ideas za Azimio la Arusha.' Ndio maana unapungukiwa hoja. Na kwa taarifa yako, Azimio la Arusha did not fail; Azimio la Arusha was ‘failed'.

.

Nadhani watanzania wengi leo hii wanamhitaji Mungu kutunusuru zaidi na tunapokwenda kuliko tulipotoka, je unapingana na hoja hii? Ni muhimu ukaachana na mawazo kwamba maendeleo yetu ni ‘path dependent.' Kuna msemo unasema ‘usione vinaelea, ujue vimeundwa'. Unayo yaona Ulaya na Marekani hayaji kwa kuiga. Na usitazame nchi kama South Korea na wengine pale wanaoitwa ‘tigers' ukadhania na sisi tutafika huko just by embracing hayo unayo sisitiza ‘Ubeparia na Utawala unaofuata Sheria'. Ni muhimu ukatambua kwamba Development is not path dependent and Mwalimu aligundua hilo mapema kabisa.
Inaonyesha wewe ni muumini wa soko huria per se na kwa ushabiki zaidi kwani haujadili kabisa mapungufu ya mfumo huu ulioletwa kiholela relative to mfumo unaopingana nao. Kama unadhani mawazo ya azimio la arusha ni mufilisi, mawazo ya soko huria ni mawazo mufilisi zaidi, especially kwa vile ni mawazo ya kuiga. Sidhani kama ni sahihi kuita mawazo ya azimio la arusha kwamba ni mufilisi hasa ukizingatia kwamba Azimio hili lilitambua kwamba gifts and loans ilikuwa ni sumu ya uhuru wetu na vitu vya kudhoofisha na kuingilia juhudi zetu za kuwa taifa linalo lenga kujitegemea. Nini mufilisi katika lengo noble kama hili? Wanaotaka tulirudie azimio la arusha sio kwamba wanataka lirudiwe kama lilivyo bali kwa kufanyiwa marekebisho.

Katika mabaya ya azimio la arusha wewe ulicho ona ni suala la watu kuwekwa rumande peke yake? Wangapi leo hii wanawekwa ndani leo kwa kuiba kuku wakati walioiba mali ya umma bado wanapeta mitaani huku wakilindwa na usalama unaolipwa posho na mishahara ya wenye mali zilizoibwa (walipa kodi)? Nini mtazamo wako kuhusu madhara ya soko huria leo hii ambapo imekuwa ni jambo la kawaida kwa mamilioni ya watanzania kushindwa kujipatia mlo zaidi ya mmoja kwa siku? Je, una maoni gani juu ya ufisadi unao litafuna taifa hivi sasa chini ya Azimio la Zanzibar ambalo majizi ndani ya CCM yalilipitisha ili kuhalalisha mali za umma walizoiba? Uchwara huu haukupewa nafasi chini ya Azimio la Arusha na hilo unalitambua fika.

Kwa kauli kama hizi, binafsi nadhani upeo wako juu ya Tumetoka Wapi, Tupo Wapi, na Twende Wapi kama taifa umefikia tamati. Na nadhani vijana wenzako wengi watakubaliana na mimi. Binafsi nadhani unakabiliwa na mambo mawili: Aidha hauna uelewo wa taifa lako au hauna uzalendo na taifa lako. Otherwise, please prove me wrong.

Mchambuzi... umeshawahi kumpigia mBuzi gitaa???

Basi leo kazi unayo... the boy operates like a robot... cant change his mind coz he is not open minded
 
- Mkuu Zakumi, thaanks kwa kunipinguzia kazi ya kumjibu Mkuu Mchambuzi, ingawa najua kwa hawa maa-apologists wa Mwalimu na Maazimio ya Arusha ni kama unampigia mbuzi gitaa, lakini leo tunao hapa mpaka kieleweke!

MUCH RESPECT!, MCHAMBUZI HII NDIO LUGHA UNAYOITAKA YA NDIO MMEITUMIA MIAKA NENDA MIAKA RUDI, MATOKEO HAKUNA MANENO MENGI KWENYE MAA-ARTICLE NCHI INAKWISHA!

William.
 
Mchambuzi... umeshawahi kumpigia mBuzi gitaa???

Basi leo kazi unayo... the boy operates like a robot... cant change his mind coz he is not open minded

- Sasa mkuu hii yako unaita ni open mind? duh haya bana mimi siiitaki tena open mind! kwamba usipokumbatia Azimio la Arusha basi huna open mind. haya mkuu na wewe umesikika sana!

William.
 
.

Kaka yangu William,

Kwanza suala la majungu ni ‘timeless’, lakini muhimu zaidi ni kwamba sio sahihi kuitumia kujadili suala muhimu kama azimio la arusha, kufanya hivyo ni kuishiwa hoja. Ni muhimu pia ukafahamu kwamba waliokuwa wanalikataa azimio la arusha ilikuwa ni viongozi ambao wao walitegemea kufaidika binafsi baada ya uhuru kwani walikuwa wanawakodolea macho wanzao nchi jirani kina njonjo n.k na kutaka kuiga tabia zao. Fanya utafiti, utagundua haraka sana kwamba Mwalimu embraced azimio la arusha baada ya kugundua kwamba wananchi walikuwa na hamu ya kuona matunda ya uhuru kwani walishapewa ahadi nyingi sana. Usikae na wazee kuadithiwa kuhusu nani alikuwa anapinga azimio la arusha na kwa sababu zipi, jaribu uwe na mtazamo wa kijamii zaidi, hasa kwa kuelewa historia ya nchi yetu.

Kuhusu suala la Mzee Malecela, hauwezi kutenganishwa na mzee wetu huyu kwa kumkwepa kiholela holela kama unavyofanya hivi sasa. Huyu ni mzee wetu muhimu na tunae mheshimu sana, kwani ni mmoja wa wazee walioijenga nchi yetu na Mwalimu bega kwa bega a pia katika awamu za baadae. Unachotakiwa kufanya ni ku declare interest na kuonyesha unasimamia wapi kwa hoja, na ukifanya hivyo mara moja tu, sidhani kama utahusishwa na Mzee Malecela tena katika mijadala.

Kusema kwamba hauitaji research ili kujua jinsi gani azimio la arusha liliua viwanda nadhani unajiweka katika wakati mgumu sana kujenga hoja yako kwani research ndogo tu itakuonyesha jinsi gani Tanzania ilifanikiwa kiuchumi kupitia viwanda chini ya azimio la arusha, na kama nchi, hatujawahi tena kufikikisha viwanda vyetu kwenye kiwango cha 12% ya GDP. Baada ya mwaka 1985, viwanda as a percentahe of GDP haijawahi kuvuka 10%. Na wewe kuchagua viwanda vya Sigara (TCC) na Bia (TBL) kama mfano inaonyesha jinsi gani usivyokuwa makini kwani hivyo ni viwanda pekee ambavyo vilikuwa vinaendeshwa kwa faida mpaka siku ya mwisho vilipo kuja binaifisishwa na Rais Mkapa.

Sidhani kama kuna mtu anaye kushambulia. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba haujengi hoja juu ya kwanini ‘Azimio la Arusha’ was a wrong move, na badala yake unatumia muda wako mwingi kutuona mazuzu sisi tunao amini kwamba azimio hili bado lina nafasi ya kutupeleka mbele iwapo litafanyiwa marekebisho. Nikuambie tu kwamba ili uweze ku ‘assess’ how well Azimio la Arusha fared as a policy, ni muhimu uliweke side by side with comparative schemes, especially Structural Adjustment Programmes under the World Bank and the IMF. Tuwekee takwimu na jenga hoja kwanini unadhani mtanzania was 1967 – 1985 (miaka 18 ya ujamaa) alikuwa worse off ukimfananisha na mtanzania wa 1986 – 2012 (miaka 26 ya soko huria). Uchambuzi wako utajitosheleza zaidi iwapo utajikita kujadili trade-offs baina na ‘economic growth’ na ‘social justice’ katika vipindi hivi viwili. Nasubiri mawazo yako katika hili.

Nadhani hili ni tatizo la kifikra kwani wapo wengi wanaopingana na sehemu kubwa ya azimio la arusha pamoja kwamba wengine pia ni wajamaa, kwa mfano Prof. Shivji, lakini wanafanya hivyo kwa kujadili mapungufu yake from an objective point of view na kutuelewesha kwa hoja, sio kama wewe unavyofanya na kuwa subjective right from the let go na kutamka bila kufikiria mara mbili mbili kwamba “Sina muda wa kusoma failing ideas za Azimio la Arusha.’ Ndio maana unapungukiwa hoja. Na kwa taarifa yako, Azimio la Arusha did not fail; Azimio la Arusha was ‘failed’.

.

Nadhani watanzania wengi leo hii wanamhitaji Mungu kutunusuru zaidi na tunapokwenda kuliko tulipotoka, je unapingana na hoja hii? Ni muhimu ukaachana na mawazo kwamba maendeleo yetu ni ‘path dependent.’ Kuna msemo unasema ‘usione vinaelea, ujue vimeundwa’. Unayo yaona Ulaya na Marekani hayaji kwa kuiga. Na usitazame nchi kama South Korea na wengine pale wanaoitwa ‘tigers’ ukadhania na sisi tutafika huko just by embracing hayo unayo sisitiza ‘Ubeparia na Utawala unaofuata Sheria’. Ni muhimu ukatambua kwamba Development is not path dependent and Mwalimu aligundua hilo mapema kabisa.
Inaonyesha wewe ni muumini wa soko huria per se na kwa ushabiki zaidi kwani haujadili kabisa mapungufu ya mfumo huu ulioletwa kiholela relative to mfumo unaopingana nao. Kama unadhani mawazo ya azimio la arusha ni mufilisi, mawazo ya soko huria ni mawazo mufilisi zaidi, especially kwa vile ni mawazo ya kuiga. Sidhani kama ni sahihi kuita mawazo ya azimio la arusha kwamba ni mufilisi hasa ukizingatia kwamba Azimio hili lilitambua kwamba gifts and loans ilikuwa ni sumu ya uhuru wetu na vitu vya kudhoofisha na kuingilia juhudi zetu za kuwa taifa linalo lenga kujitegemea. Nini mufilisi katika lengo noble kama hili? Wanaotaka tulirudie azimio la arusha sio kwamba wanataka lirudiwe kama lilivyo bali kwa kufanyiwa marekebisho.

Katika mabaya ya azimio la arusha wewe ulicho ona ni suala la watu kuwekwa rumande peke yake? Wangapi leo hii wanawekwa ndani leo kwa kuiba kuku wakati walioiba mali ya umma bado wanapeta mitaani huku wakilindwa na usalama unaolipwa posho na mishahara ya wenye mali zilizoibwa (walipa kodi)? Nini mtazamo wako kuhusu madhara ya soko huria leo hii ambapo imekuwa ni jambo la kawaida kwa mamilioni ya watanzania kushindwa kujipatia mlo zaidi ya mmoja kwa siku? Je, una maoni gani juu ya ufisadi unao litafuna taifa hivi sasa chini ya Azimio la Zanzibar ambalo majizi ndani ya CCM yalilipitisha ili kuhalalisha mali za umma walizoiba? Uchwara huu haukupewa nafasi chini ya Azimio la Arusha na hilo unalitambua fika.

Kwa kauli kama hizi, binafsi nadhani upeo wako juu ya Tumetoka Wapi, Tupo Wapi, na Twende Wapi kama taifa umefikia tamati. Na nadhani vijana wenzako wengi watakubaliana na mimi. Binafsi nadhani unakabiliwa na mambo mawili: Aidha hauna uelewo wa taifa lako au hauna uzalendo na taifa lako. Otherwise, please prove me wrong.

- Mchambuzi nilikuwa nakuheshimu sana lakini kama nilivyosema ukishaanza maneno ya baba yako na mama yako kwenye hoja muhimu ya taifa, pale pale huwa ninaacha kusoma mpaka mwisho maana ninaamini huna hoja ila unajaribu kutumia nguvu kulazmisha hoja na kujaribu kuwavuta watu wengine wakushangilie kama yanga na simba.

- Bingwa wa hoja Mkulu Mwanakijiji sijawahi kuona akiweka hoja za baba na mama za watu, yeye hupiga hoja kwa hoja tu na Dunia nzima inaelewa anachosema bila kugusa baba wala mama wa mtu, hizo namba ulizoandika ndio mmezitumia sana kuwadanganya wananchi huku viwanda vinaanguka, mashirika yanaleta hasara nyinyin mmeshika hizo namba na asilimia nyingi sana kumbe uongo mtupu, nimesema huwa sisomi empty theory au any theory iliyoshindwa kama Azimio la Arusha, ni simply a failed theory na dead hata klabla hijaaanza na ndio imetufikisha hapa hili taifa tumedumaa na kubaki kulaumiana kama wendawazimu,

- Azimio was wrong, kwa sababu halijawahi kuafnikiwa mahali popote Duniani, na ndio maana waanzilishi wa maazimio ya ujmaaa jamaa kule Soviet wali-collapse, kwa sababu zilikuwa ni unrealistic theories za kuwadanganya wananchi kwamba Soviet ni Super Power kumbe hawana uchumi, mwendo wa kwenda ambele sasa ni ubepari tu hakuna njia nyingine!

- Mchambuzi great class, ila next time dont waste your time na mtu asiye na hoja nzito kama zako maana wanaojua vizuri watashindwa kutofautisha! ha! ha! ha! ha! ha! ha!

William.
 
- Joka Kuu, heshima yako sana mkuu, mataifa yote yaliyoendelea Duniani hayaishi kwa miiko ya uongozi, yanaishi kwa utawala unaoheshimu sheria tu! Ukishaanza maneno ya miiiko automatically, unatoka kwenye mkondo wa sheria na ku-establish alternative ya sheria matokeo yake ndiop haya tumekwama, kiongozi mwizi kwenda kujadiliwa kwenye vikao vya chama, nonsense!

- Mawaziri wezi, mnaenda kubishana bungeni, bdala ya kwenda kwenye sheria, Mataifa yote yaliyoendelea Duniani, kamati yao ya bunge inaangalia ishu ikiona waziri ni mwizi anaitwa mbele ya kamati na kuhojiwa, akishindwa kuridhisha kamati hoja inapelekwa kwenye full bunge, inapigwa kura ili aende mahakamani au aadhibishwe na kamati ya bunge, kama kura hazitoshi kama ilivyo bunge letu ni kazi ya upinzani kuichukua kesi kwa wananchi! Wananchi wataamua tena in a very good way kwa kuwafundisha viongozi kwenye kura,

- Sisi tumekalia kulia lia tu, Azimio! hivi lile Azimio gani lililokuwa dead hata kabla halijaanza?

Willie!
Marekani ni nchi ya kibepari lakini ina miiko ya uongozi. Bila miiko ya uongozi taifa linakuwa kama meli inayoyumba baharini bila kepteni kujua inakoelekea. Kwa mfano, Obama hawezi kumuajiri mkewe, mwanae, au ndugu yake katika serikali. Huo ni mwiko. Obama hawezi kuendesha kampuni ya biashara akiwa White House. Huo ni mwiko. Obama hawezi kumpigia mkuu wa polisi na kumtaka amwachie mhalifu fulani kwa sababu ni rafiki au ndugu yake Obama. Huo ni mwiko. Azimio la Arusha liliweka miiko ya uongozi ambayo ilifutwa na Mwinyi na Mzee Malecela pale Zanzibar na matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona. Kulaumu Azimio kwa matatizo tuliyo nayo Tanzania ni kuwa myopic. Kenya wamekuwa mabepari tangu walipopata uhuru. Tena wao viongozi wao walijinyakulia ardhi na mali za serikali bila aibu tangu enzi za Kenyatta, lakini ukienda mashambani Wakenya wanaishi maisha ya dhiki kuliko hata sisi Watanzania. Azimio la Arusha lilitoa matumaini ya maisha bora kwa Watanzania waliokuwa wanaishi vijijini ambao ni zaidi ya 80% ya population yetu. Mnaoshangilia kufa kwa azimio hamna lolote la kuonyesha ila tu kukithiri kwa wizi wa viongozi na ndiyo sababu kila mtu anakimbilia sasa kuwa mbunge ili ama achaguliwe kuwa waziri, atajirike kwa muda mfupi, au awe na maisha mazuri ya haraka kuliko Mtanzania wa kawaida.
 
- Mkuu Jasusi, heshima yako sana America kuna sheria, hakuna miiko ya uongozi you know better huko taifa huongozwa kwa sheria, matatizo ya Clinton na Monica yalitatuliwa na sheria sio miiiko ya uongozi, hapana!

- Kenya wamekwua mabepari kwa muda mrefu kuliko sisi, ndio maana wana viwanda vingi kuliko sisi na pesa yao ni kubwa kuliko yetu, na pia Watalii wanawajali wao kuliko sisi, yaaani haya hata bila shule yanaeleweka sana kuwa ni matunda ya ubepari!

William.
 
- Sasa mkuu hii yako unaita ni open mind? duh haya bana mimi siiitaki tena open mind! kwamba usipokumbatia Azimio la Arusha basi huna open mind. haya mkuu na wewe umesikika sana!

William.
Thanks William

Actually my post ilimaanisha kuwa open minded ni kuwa flexible with your ideas, kukubali kusoma na kujifunza through azimio au hata other similar references zinazolingana na situation yetu na azimio la arusha... na hii ilitokana na jibu lako la kwamba huna muda wa kusoma

Tukirudi kwenye mada.. naomba kujua, what motivate you as a successful nation??? ni watu well being au numbers in the financial journals??

what would be your performance marker if you are given a chance kufanya ratings za economic performance yetu??

Na unaweza kunipa mwongozo na mimi nijifunze... if Azimio la arusha was not there miaka hiyo, can you guess what system we would be operating??
 
SEHEMU YA KWANZA
Imani ya Tanu
SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA

IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII

Soma hapo juu. Azimio la Arusha ni Imani ya chama cha TANU. Chama hicho hakipo, na sisi wengine ni wanachama wa CHADEMA, CUF au TLP. Hivyo kwanini mnataka hoja ya chama kimoja iwe ya nchi zima?

It disturbs me to see we dont want to confront the fundamental and thorny issues that affects us today, without referring to Nyerere and his term in the office. The nature of the problems that we face today have got nothing to do with Nyerere. Kwa mfano, ningeona tatizo kama Nyerere angesaini mkataba wa miaka mia mbili na nchi au kampuni fulani ya nje ili kuiendesha bandari yetu au mbuga zetu za wanyama au hata migodi yetu.
Nyerere hakufanya hivyo ila sisi tunafanya. Tukiulizwa tunasema tatizo ni kwasababu ya Nyerere na siasa zake. Tuache kuzidanganya nafsi zetu wenyewe. Tupambane na vizingiti vinavyoikabili Tanzania ya leo kwa ubunifu zaidi na matumizi sahihi ya vichwa vyetu.
Naona tulio wengi nia ni kuwa viongozi wa wananchi bila hata kujua hao wananchi tutawafanyia nini. Anyway, labda like father like son. Who knows???!!!
 
.

Kaka yangu William,

Kwanza suala la majungu ni ‘timeless', lakini muhimu zaidi ni kwamba sio sahihi kuitumia kujadili suala muhimu kama azimio la arusha, kufanya hivyo ni kuishiwa hoja. Ni muhimu pia ukafahamu kwamba waliokuwa wanalikataa azimio la arusha ilikuwa ni viongozi ambao wao walitegemea kufaidika binafsi baada ya uhuru kwani walikuwa wanawakodolea macho wanzao nchi jirani kina njonjo n.k na kutaka kuiga tabia zao. Fanya utafiti, utagundua haraka sana kwamba Mwalimu embraced azimio la arusha baada ya kugundua kwamba wananchi walikuwa na hamu ya kuona matunda ya uhuru kwani walishapewa ahadi nyingi sana. Usikae na wazee kuadithiwa kuhusu nani alikuwa anapinga azimio la arusha na kwa sababu zipi, jaribu uwe na mtazamo wa kijamii zaidi, hasa kwa kuelewa historia ya nchi yetu.

Kuhusu suala la Mzee Malecela, hauwezi kutenganishwa na mzee wetu huyu kwa kumkwepa kiholela holela kama unavyofanya hivi sasa. Huyu ni mzee wetu muhimu na tunae mheshimu sana, kwani ni mmoja wa wazee walioijenga nchi yetu na Mwalimu bega kwa bega a pia katika awamu za baadae. Unachotakiwa kufanya ni ku declare interest na kuonyesha unasimamia wapi kwa hoja, na ukifanya hivyo mara moja tu, sidhani kama utahusishwa na Mzee Malecela tena katika mijadala.

Kusema kwamba hauitaji research ili kujua jinsi gani azimio la arusha liliua viwanda nadhani unajiweka katika wakati mgumu sana kujenga hoja yako kwani research ndogo tu itakuonyesha jinsi gani Tanzania ilifanikiwa kiuchumi kupitia viwanda chini ya azimio la arusha, na kama nchi, hatujawahi tena kufikikisha viwanda vyetu kwenye kiwango cha 12% ya GDP. Baada ya mwaka 1985, viwanda as a percentahe of GDP haijawahi kuvuka 10%. Na wewe kuchagua viwanda vya Sigara (TCC) na Bia (TBL) kama mfano inaonyesha jinsi gani usivyokuwa makini kwani hivyo ni viwanda pekee ambavyo vilikuwa vinaendeshwa kwa faida mpaka siku ya mwisho vilipo kuja binaifisishwa na Rais Mkapa.

Sidhani kama kuna mtu anaye kushambulia. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba haujengi hoja juu ya kwanini ‘Azimio la Arusha' was a wrong move, na badala yake unatumia muda wako mwingi kutuona mazuzu sisi tunao amini kwamba azimio hili bado lina nafasi ya kutupeleka mbele iwapo litafanyiwa marekebisho. Nikuambie tu kwamba ili uweze ku ‘assess' how well Azimio la Arusha fared as a policy, ni muhimu uliweke side by side with comparative schemes, especially Structural Adjustment Programmes under the World Bank and the IMF. Tuwekee takwimu na jenga hoja kwanini unadhani mtanzania was 1967 – 1985 (miaka 18 ya ujamaa) alikuwa worse off ukimfananisha na mtanzania wa 1986 – 2012 (miaka 26 ya soko huria). Uchambuzi wako utajitosheleza zaidi iwapo utajikita kujadili trade-offs baina na ‘economic growth' na ‘social justice' katika vipindi hivi viwili. Nasubiri mawazo yako katika hili.

Nadhani hili ni tatizo la kifikra kwani wapo wengi wanaopingana na sehemu kubwa ya azimio la arusha pamoja kwamba wengine pia ni wajamaa, kwa mfano Prof. Shivji, lakini wanafanya hivyo kwa kujadili mapungufu yake from an objective point of view na kutuelewesha kwa hoja, sio kama wewe unavyofanya na kuwa subjective right from the let go na kutamka bila kufikiria mara mbili mbili kwamba "Sina muda wa kusoma failing ideas za Azimio la Arusha.' Ndio maana unapungukiwa hoja. Na kwa taarifa yako, Azimio la Arusha did not fail; Azimio la Arusha was ‘failed'.

.

Nadhani watanzania wengi leo hii wanamhitaji Mungu kutunusuru zaidi na tunapokwenda kuliko tulipotoka, je unapingana na hoja hii? Ni muhimu ukaachana na mawazo kwamba maendeleo yetu ni ‘path dependent.' Kuna msemo unasema ‘usione vinaelea, ujue vimeundwa'. Unayo yaona Ulaya na Marekani hayaji kwa kuiga. Na usitazame nchi kama South Korea na wengine pale wanaoitwa ‘tigers' ukadhania na sisi tutafika huko just by embracing hayo unayo sisitiza ‘Ubeparia na Utawala unaofuata Sheria'. Ni muhimu ukatambua kwamba Development is not path dependent and Mwalimu aligundua hilo mapema kabisa.
Inaonyesha wewe ni muumini wa soko huria per se na kwa ushabiki zaidi kwani haujadili kabisa mapungufu ya mfumo huu ulioletwa kiholela relative to mfumo unaopingana nao. Kama unadhani mawazo ya azimio la arusha ni mufilisi, mawazo ya soko huria ni mawazo mufilisi zaidi, especially kwa vile ni mawazo ya kuiga. Sidhani kama ni sahihi kuita mawazo ya azimio la arusha kwamba ni mufilisi hasa ukizingatia kwamba Azimio hili lilitambua kwamba gifts and loans ilikuwa ni sumu ya uhuru wetu na vitu vya kudhoofisha na kuingilia juhudi zetu za kuwa taifa linalo lenga kujitegemea. Nini mufilisi katika lengo noble kama hili? Wanaotaka tulirudie azimio la arusha sio kwamba wanataka lirudiwe kama lilivyo bali kwa kufanyiwa marekebisho.

Katika mabaya ya azimio la arusha wewe ulicho ona ni suala la watu kuwekwa rumande peke yake? Wangapi leo hii wanawekwa ndani leo kwa kuiba kuku wakati walioiba mali ya umma bado wanapeta mitaani huku wakilindwa na usalama unaolipwa posho na mishahara ya wenye mali zilizoibwa (walipa kodi)? Nini mtazamo wako kuhusu madhara ya soko huria leo hii ambapo imekuwa ni jambo la kawaida kwa mamilioni ya watanzania kushindwa kujipatia mlo zaidi ya mmoja kwa siku? Je, una maoni gani juu ya ufisadi unao litafuna taifa hivi sasa chini ya Azimio la Zanzibar ambalo majizi ndani ya CCM yalilipitisha ili kuhalalisha mali za umma walizoiba? Uchwara huu haukupewa nafasi chini ya Azimio la Arusha na hilo unalitambua fika.

Kwa kauli kama hizi, binafsi nadhani upeo wako juu ya Tumetoka Wapi, Tupo Wapi, na Twende Wapi kama taifa umefikia tamati. Na nadhani vijana wenzako wengi watakubaliana na mimi. Binafsi nadhani unakabiliwa na mambo mawili: Aidha hauna uelewo wa taifa lako au hauna uzalendo na taifa lako. Otherwise, please prove me wrong.

kaka

nashukuru sana kwa uchambuzi wako makini
kiukweli kabisa huyu bwana william hana hoja,hawezi kujenga wala kutetea hoja zake alizoziweka,na anashangaza sana pale anapokuja na usemi kuwa HAWEZI POTEZA MUDA KWA KUSOMA HOJA ZIHUSUYO AZIMIO LA ARUSHA ikimaanisha tayari anamajibu yake kichwani na hataki kubadirika wala kueleweshwa,sasa ulileta hoja mezani ya nini?

kwa sisi tuliosomea saikolojia tunaelewa kuwa,ili uweze kumpa ushauri mtu ni lazima kwanza yeye mwenyewe akubari kushauriwa na usimlazimishe kumshauri,kwa maana hiyo basi bwana william hayupo tayari kupata nini watu wanansema kwakuwa tayari ameweka post akiwa na vyake kichwani,

hulazimishwi kukubaliana nasi lakini ukweli ndio huo

walivunja azimio la arusha na kuunda azimio la zanzibar kwa maslahi yao binafsi,uroho wa kumiliki mali na kuuza uchumi wetu kwa wawekezaji

unanishangaza sana tena sana,pele unaposema kuwa azimio la arusha ndilo lililouwa viwanda vyetu,nadhani husomi historia na hata kama unaisoma huielewi

kwani viwanda vyote tulivyokuwa navyo mpaka sasa vingine vimegeuka ni majumba ya kufugia mbuzi vilianzishwa na hilo azimio la arusha,lakini baada ya kuanzisha azimio la zanzibar viwanda vyote viliuzwa na hakuna kiwanda kipya kilichojengwa ktk kipindi hiki cha utandawazi zaidi ya kukarabati vile vya azimio la arusha

tunaelezwa enzi za azimio la arusha Tanzania ilikuwa inamiliki zaidi ya ndege 18,lakini ktk kipindi hiki cha utandawazi na wizi Tanzania hususani shirika la ndege halina hata ndege moja.

Please mkuu,rudi kajipange upya,ktk hili huna la kuongea zaidi ya kuwa na majibu yako usiyotaka yabadirishwe hata kama ni false
 
- Mchambuzi nilikuwa nakuheshimu sana lakini kama nilivyosema ukishaanza maneno ya baba yako na mama yako kwenye hoja muhimu ya taifa, pale pale huwa ninaacha kusoma mpaka mwisho maana ninaamini huna hoja ila unajaribu kutumia nguvu kulazmisha hoja na kujaribu kuwavuta watu wengine wakushangilie kama yanga na simba.

- Bingwa wa hoja Mkulu Mwanakijiji sijawahi kuona akiweka hoja za baba na mama za watu, yeye hupiga hoja kwa hoja tu na Dunia nzima inaelewa anachosema bila kugusa baba wala mama wa mtu, hizo namba ulizoandika ndio mmezitumia sana kuwadanganya wananchi huku viwanda vinaanguka, mashirika yanaleta hasara nyinyin mmeshika hizo namba na asilimia nyingi sana kumbe uongo mtupu, nimesema huwa sisomi empty theory au any theory iliyoshindwa kama Azimio la Arusha, ni simply a failed theory na dead hata klabla hijaaanza na ndio imetufikisha hapa hili taifa tumedumaa na kubaki kulaumiana kama wendawazimu,

- Azimio was wrong, kwa sababu halijawahi kuafnikiwa mahali popote Duniani, na ndio maana waanzilishi wa maazimio ya ujmaaa jamaa kule Soviet wali-collapse, kwa sababu zilikuwa ni unrealistic theories za kuwadanganya wananchi kwamba Soviet ni Super Power kumbe hawana uchumi, mwendo wa kwenda ambele sasa ni ubepari tu hakuna njia nyingine!

- Mchambuzi great class, ila next time dont waste your time na mtu asiye na hoja nzito kama zako maana wanaojua vizuri watashindwa kutofautisha! ha! ha! ha! ha! ha! ha!

William.

nadhani hiimada tuachane nayo,kwa sasa tupo na azimio la zanzibar na tunaona mambo yalivyo

nawakubali sana wachina,wao wapo wazi sana na siasa zao nini zinafuata,uchina ni nchi ya kijamaa hutaki unaacha,inaongozwa na sheria za kijamaa hutaki unaacha na haijayumbishwa na mabebari kwa kulazimishwa kuuza njia kuu za uchumi.

azimio la zanzibar ndilo limewapa kiburi viongozi wa sasa,kutumia uongozi kwa maslahi yao binafsi,kumiliki makampuni kama wanahisa namba 2,kutolipa kodi

hakika tutakuja sikumoja tukiwa hai kulikemea azimio la zanzibar kama tunavyo pigia kelele azimio la arusha.

nchi hii inahitaji uwajibikaji,wananchi wanafanya kazi sana tena sana,lakini viko vikundi vya watu wachache ndivyo vyenye haki ktk chi hii,

tunahitaji kubadilika na tuwatendee mema wananchi kama tunavyotaka kutendewa sisi

JIFINYE KWA VIDOLE VIWILI,MAUMIVU UTAKAYOYAPATA WEWE,NDIVYO HIVYO WANANCHI WANAVYOJISIKIA
 
SEHEMU YA KWANZA
Imani ya Tanu
SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA

IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII

Soma hapo juu. Azimio la Arusha ni Imani ya chama cha TANU. Chama hicho hakipo, na sisi wengine ni wanachama wa CHADEMA, CUF au TLP. Hivyo kwanini mnataka hoja ya chama kimoja iwe ya nchi zima?

Zakumi. That is too low mzee. Read between the lines in my post.

Nimesema ukitoa sura ya kwanza,azimio bado lina mambo mengi ya msingi kwa taifa letu. Sasa unapokuja na hoja ya nisome sura ya kwanza,nakushangaa.

Hakika nakwambia,licha ya mapungufu ya azimio hilo,lina mambo mazuri. Jambo la msingi kwetu ni kujadili namna gani tuliboreshe. Tuchukue mazuri yake tuchanganye na mazuri ya ubepari,then tunakua na mfumo mchanganyiko ambao unakuwa na manufaa kwa taifa nzima.
 
Last edited by a moderator:
Well, heshima mbele sana JF,

- Ninaomba kusema tena na tena, we were Dead wrong na idea za Azimio La Arusha, infact ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama hili taifa, hatujui tunakokwenda wala tulikotoka. Halafu wanatokea wasomi wanaodai eti turudi kwenye Azimio, hilo Azimio limetushinda mwanzoni kwa nini kuna wanaoamini tutaliweza sasa?

- Recently, nimeona wale wengi walioachwa kwenye uongozi wa juu yaani kwenye mlo, wakililia Azimio, halafu ninachukizwa sana ninapoona media inawapa free lunch hawa waliokosa mlo, sijawahi kuwasikia wakisema Azimio liliwahi kumfunga kiongozi gani wa juu mwizi, sijawasikia wakisema Azimio lilifanya nini cha maaana mpaka wanalilia!

- Mwalimu, yes was the greatest ever, lakini Mwalimu alikuwa na mapungufu makubwa mawili, hakujua;- !. Uchumi 2. Sheria, hivi vitu viwili Mwalimu simply hakuvijua kama alivijiua basi hakuvitilia maanani, na ndivyo vinavyolitafuna taifa letu sasa akiwa hayupo!

- WA-TANZANIA, KAMA TUNATAKA KUSONGA MBELE NA KIJIREKEBISHA TUACHANE NA MANENO YA AZIMIO LA ARUSHA, KWA SABABU NDILO HASA LIMETURUDISHA NYUMA SANA, LISIRUDI, LIENDE ZAKE, NA TUSILIJADILI MAANA NI SHETANI LILILOTURUDISHA NYUMA SANA, SASA TWENDE MBELE NA UBEPARI NA UTAWALA UNAOHESHIMU SHERIA NDIO THE BEST WAY MBELE!

RESPECT PEOPLE!

Mr. Willie @DSM City!

Hoja zako hapa ni nyepesi sana Le Mutuz. Umeshindwa kuelezea ni vipo Azimio la Arusha limepelekea tuzidi kuwa masikini mpaka leo hii, ili hali tulitakiwa tuwe tumepiga hatua za kimaendeleo.Elezea kitakwimu ni kwa vipi kabla ya Azimio la Arusha uchumi ulikuwa unakuwa na ukioanisha na ustawi wa maendeleo ya jamii.Pia uweze kuweka baya baada ya Azimio la Arusha kuanza kutekelezwa uchumi ulikuwa unakuwa kwa kiwango gani sambamba na ustawi wa maendeleo ya Jamii .Mwisho uelezee baada ya azimio la Arusha kufa nini kilitokea mpaka sasa.

Sio mfuasi wa Unyerere ila sijaweza kumlinganisha na viongozi baada ya yeye kwa kuwa mambo mengi ambayo yeye aliyafanya kwa vitendo hawa viongozi wetu wa sasa ndio wanataka kudanganya uma kuwa wanaanza michakato(kama wanavyopenda kutamka). Raisi wako JK amekuja na hoja ya kilimo kwanza anahutubia maswaala ya kuongeza thamani kwenye mazao ya wakulima,akitumia makabrasha.Je unajua Mwl. alishafanya kwa vitendo hizo hatua?.Leo tunauza korosho ghafi,ila enzi za Mwl alijenga viwanda vya kubangiua Korosho (kuongeza thamani kwenye mazao).Nenda Mtwara -Newala, Mtwara mjini na Lindi leo uone hivyo viwanda vimefanywaje.Vyote vimegeuzwa maghala.

Kama Great thinker sinzani kama ni sahihi kukosoa mfumo fulani wa utawala/sera bila kuelezea njia mbadala ukiainisha mapungufu ya ufumo wa awali, sambamba na kuoanisha na mfumo/sera mbadala na zenye kutekelezeka kwa mifano huo unaouna ni sahihi.

Le mutuz nilikupa ushauri kabla ya siku ya kinyang'anyiro cha kura za ubunge wa Afrika Mashariki,jitahidi sana kujifunza mengi kutoka kwa wataalamu wa fani mbalimbali.Wewe kuzunguka dunia nzima 90% sio tija kama huwezi deliver.Kwa hoja kama hii (Sio kwamba nashabikia turudi kwenye azimio la Arusha) ila haina ushawishi imekaa kama post ya Facebook.Jifunze kujenga hoja kitafiti,hii ni kama unandoto za kuwa kiongozi.Kwa hoja kama hii sinzani kama unaweza pambana na vijana wenzako kama kina J.Mnyika,J.Makamba(Japo amejisahau),Zitto Kabwe.Jipange sana Le Baharia.
 
Back
Top Bottom