Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,345
- 10,885
@W.J. Malecela. Azimio la Arusha bado lina mambo mazuri sana ya msingi kwa maendeleo ya taifa letu; ukitoa sehemu ya kwanza, sehemu za pili na tatu za azimio hilo bado zina mambo ambayo yana tija sana kwa taifa letu, mfano:
1. Suala la unyonyaji, azimio linasema hivi:
....... mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali hayapitani mno....uk.5
Sasa hapa mzee unataka kusema azimio ndio limetufikisha hapa, wakati lilisisitiza suala la kupinga unyonyaji?!
Pia...
......watu peke yao ambao huishi kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao, kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe...uk.5 (hii sehemu ya mwisho hata nchi zilizo kwenye mfumo wa ubepari, zina taratibu zenye elements kama hizo - mfano food stamps huko Marekani, na malipo ya kujikimu kwa nchi za Ulaya kama Uingereza)
2. Suala la kujitegemea.
Hapa azimio linasisitiza katika nchi kujitegemea na kuepuka kutegemea misaada kutoka mataifa mengine. Na mojawapo ya njia ya kufanikisha kujitegemea na kuongeza uwigo wa ukusanyi wa kodi..mfano azimio linasema:
Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi bila kutaka Ngombe akamuliwe tena...uk. 12-13
Azimio linasema kwa uwazi kabisa kwamba, serikali katika kujaribu kuepuka upanuzi wa ukusanyaji wa kodi, imejikita katika kutafuta na kupokea misaada ya kifedha toka ughaibuni (grants, unfairly conditioned loans and FDIs and aids). Azimio linasema kwa uwazi kabisa ni namna gani ilivyo ajabu na ujinga kutegemea fedha za nje kwa vile fedha hizo zinahatarisha uhuru wa kuamua mambo yetu (hii inajidhihirisha sasa hapa nchini; serikali haiwezi kufanya maamuzi bila kufikiri "wakubwa" watasemaje au watafikiriaje). Azimio linaongelea juu ya mikopo yenye masharti magumu ambayo licha ya kutokuwa na faida kwa taifa, pia inajenga mzigo mkubwa kwa watanzania wa sasa na wajao (hii pia inajidhihirisha sasa, kwani deni la taifa limekuwa kubwa kupita kiasi, huku serikali ikiendelea kukopa bila kufanya tathmini ya kina ya namna ya kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo ya taifa). Pia azimio linaongelea suala la uwekezaji wa watu kutoka nje (FDIs), uwekezaji ambao unaweka uchumi wa nchi mikononi mwa wageni, ambao wanapeleka faida za uwekezaji huo makwao (hii ni dhahiri kabisa hapa Tanzania, tunaona faida za uwekezaji katika madini, wanyamapori n.k. zikihamishwa kwenda kwenye nchi yanayotoka makampuni hayo. Na hakuna anayetaka kukumbuka mwongozo wa Azimio).
3. Suala la kumjali mkulima, azimio linasema
Ni dhahiri kwamba watanzania wengi wanaishi vijijini, ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo. Hivyo bila kuweka jitihada za kipekee katika kumjali mkulima hakika, maendeleo yatakuwa ndoto. Nchi zote zilizoendelea, zilisukumwa na kazi na shughuli za watu walioishi vijiji; maendeleo ya viwanda Ulaya licha ya kunufaika na ukoloni, watu wa vijijini na shughuli zao walikuwa driving forces za maendeleo hayo. Vivyo hivyo Marekani, watu walioishi vijijini pamoja na shughuli zao ndiyo walio sukuma maendeleo katika nchi hizo. Sasa kama taifa haliweki vipaumbele kwenye sehemu ambayo ndiyo moyo wa taifa, taifa litakuwa linapiga mark time tu.Ni ajabu na jambo la kusikitisha sana kwamba taifa halijafanikiwa katika hili, kwani sasa msisitizo upo katika diplomasia ya kiuchumi, ambapo uwekezaji mkubwa ndiyo unaotegemewa kusukuma gurudumu la maendeleo, huku wakulima wengi wakitegemewa kuwa outgrowers kupitia kwenye huo mfumo. Hii nayo imejidhihirisha hapa Tanzania, ambapo kuna wimbi la land grabbing linaondelea sasa, huku wimbo wa Kilimo Kwanza nao ukiimbwa!! Seriously, kwa utaratibu huo, watanzania wengi (wakulima) watanufaika kweli na Kilimo Kwanza?!
4. Suala la misingi ya maendeleo, azimio linatilia mkazo katika:
....ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora....uk. 28-31
Mzee hata katika hili unaona Azimio limetufikisha hapa? Seriuosly?
Ardhi na watu, taifa limejitosheleza katika hayo. Tatizo lipo kwenye siasa safi na uongozi bora (hapa ndipo miiko ya uongozi inapo-make sense). Siasa inayotawala sasa ni siasa uchwara; uongozi nao ni kama vile haupo. Kwani hakuna uwajibikaji, serikali haijali shida za wananchi, uongozi wa umma umekuwa sehemu ya kwenda kuchuma pesa na kujitajirisha, viongozi hawana tena morals zinakujivunia mbele ya wananchi. Sasa mtu ambaye hana hata ufahamu na uelewa wa nini maana ya kuwa kiongozi wa umma, wanachaguliwa na kupewa vyeo vikubwa. Tunaona mtu ambaye hana mbele wala nyuma katika mambo ya uongozi anaweza kuwa mbunge, waziri, mkuu wa mkoa/wilaya n.k. Viongozi wa umma wanaishi na kunufaika kwa jasho la walipa kodi, bila kujali kodi hizo zinaleta manufaa kwa watu wote. Pato la taifa linafaidiwa na wachache waliopo kwenye "mamlaka" n.k. Vijana wengi "wanazurura hovyo bila ajira" (vijana hawa wanajifariji kwa kujipa ajira zinazosemwa zisizo rasmi), viongozi wanatuma polisi wenye marungu na bomu ya machozi kuwanyanyasa vijana hao, badala ya kutafuta suluhisho la kudumu. Hali ya siasa na uongozi imekuwa mbaya kiasi kwamba raia nao sasa wanawaza "kupiga" tu popote pale walipo ili nao wajinufaishe na keki ya taifa, inayoliwa na watu wachache walio kwenye "mamlaka".
Sasa mkuu @W.J. Malecela, unapokuja na wazo kwamba Azimio la Arusha ndilo lililotufikisha hapa, bila kuzingatia yale mazuri ya azimio hilo, naamini unakosea mzee. Pengine ni kweli kwamba kuna vitu ambavyo haviko relevant na hali ya sasa ya Tanzania, lakini ni ajabu vile vile kulitupa azimio lote kwa kudai halina manufaa yoyote.
Na elewa kwamba toka taifa limeanzisha kuchanganya mambo ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar, ndipo mambo yalipoanza kwenda kombo. Serikali ikapuuzia yale mazuri ya Azimio la Arusha, "ikalichinjia baharini", na ikafikiria tu mabaya ya azimio hilo; mwisho wa siku mambo ndiyo yakaanza kwenda shaghalabaghala.
Lete hoja ya kujadili namna gani tuliboreshe azimio hilo (kwa kuweka mambo yaliyo na maana kwa sasa) kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.