Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Uamuzi wa Hamas kulitetea taifa la Palestina unaendelea kuzaa matunda kwa mataifa mengi zaidi kuendelea kulitambua taifa hilo katika ngazi ya Umoja wa mataifa.
Katika kura zilizopigwa jana kwenye baraza kuu la UN jumla ya kura 143 ziliunga mkono,Tisa tu ndizo zilizokataa na 25 wakaamua kutopiga kura.
Baada ya hatua hiyo ambayo inaitambua Palestina kwa mipaka yake ya 1967 azimio hilo linatarajiwa kupelekwa kwenye baraza la usalama la jumuiya hiyo ambako nchi moja kati ya tano ikipiga kura ya veto basi azimio hilo halitopita. Nchi inayohofiwa zaidi na ambayo imeshafanya hivyo mara nyingi dhidi ya haki za Palestina ni Marekani pekee.
Baada ya azimio hilo kupata uungwaji mkono mkubwa kiasi hicho ,balozi wa Israel katika umoja wa mataifa alifoka na kuushutumu umoja wa mataifa kuwa umekubali kuruhusu taifa la kigaidi kujiunga na umoja huo.