Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

sheikh Mohamed Said wewe ni mwandishi mzuri sana ila katika maandiko yako hasa ya uhuru wa Tanganyika unataka kutuonesha waliopigania uhuru walikua na mlengo wa kiislam zaidi kuliko misimamo yao ya kiaflika kupinga ukoloni!
 
Kleist Sykes asili yake huyo babu alikuwa adopted na wazungu na alikuja kuwa mwanajeshi.
Kleist na Sykes yote ni majina ya Kijerumani. Kwa hiyo Kleist siyo Mtanzania? Kama aliletwa na Jeshi la mkolono je tumwite naye mkoloni? Alikuwa ni Mkatoliki au Mwislamu. Ilikuwaje aishi Kiputa Street asokae Oysterbay na Wazungu wenziye?
 
Kleist na Sykes yote ni majina ya Kijerumani. Kwa hiyo Kleist siyo Mtanzania? Kama aliletwa na Jeshi la mkolono je tumwite naye mkoloni? Alikuwa ni Mkatoliki au Mwislamu. Ilikuwaje aishi Kiputa Street asokae Oysterbay na Wazungu wenziye?

William Marconi,
Soma haya kutoka kitabu cha Abdul Sykes:



Kleist Sykes, Muasisi wa Harakati na Mtu wa Fikra: 1894 - 1949

''Historia ya ukoo wa akina Sykes inarudi nyuma kiasa cha zaidi ya miaka mia moja hivi. Katika miaka hiyo yote ukoo huu umeweza kuhifadhi historia yake kupitia kwa Kleist Sykes mwenyewe ambae yeye alijifunza historia ya kabila lao kutoka kwa mlezi wake, Affande Plantan. Kleist akawa ndiyo mtu wa kwanza katika ukoo huo kuandika asili yao na yote aliyoyatenda katika uwanja wa siasa. Affande Plantan alimlea Kleist katika nyumba yake baada ya kifo cha baba yake Sykes Mbuwane kutokea huko Ruaha wakati wakirudi vitani baada ya kumshinda Chifu Mkwawa. Sykes Mbuwane aliona ngímbe wakivuka Mto Ruaha na akadhani maji hayakuwa na kina kirefu. Akihisi kuwa angeliweza kuvuka, shujaa huyu wa Kizulu na wenzake wakajaribu kuvuka na wote wakasombwa na maji na kuzama.

Ukoo wa Mbuwane asili yake ni Afrika Kusini. Kabila hilo lilikuwa chini ya utawala wa Chaka mfalme mashuhuri wa Wazulu. Kutokana na vita vya mara kwa mara ukoo huo ulikimbia Afrika Kusini kuelekea kaskazini Msumbiji kukimbia vita vya kikabila vilivyokuwa vikitokea mara kwa mara. Ndani ya Msumbiji Wazulu katika Inhambane hawakupata amani ya kudumu na walipambana na Wareno katika vita iliyodumu miaka mingi. Mwishowe Wazulu walishindwa kutokana na mkataba ambao mmoja wa watoto wa chifu aliwekeana na Wareno. Inasemekana kulikuwa na ghilba katika mkataba ule, kwa kuwa Wareno hawakutimiza masharti ya makubaliano, Wazulu wakajikuta wamejiweka pabaya. Hii ikasababisha kuanguka kwao na hatimae kushindwa vita. Haikuwezekana kufahamika kwa uhakikani makubalino gani ambayo mataifa hayo mawili yalikuwa yamekubaliana, lakini itoshe tu kujua kuwa kushindwa kwa Wazulu hakukutokana na nguvu za kijeshi za Wareno kuwazidi Wazulu.

Wajerumani kwa kuwa walikuwa ni watu wanye kuusudu sana mambo ya vita na ujasiri waliwaona Wazulu kama watu ambao wangeliweza kuwatumia katika majeshi yao ili kusaidia kuja kuiteka Tanganyika. Wakati ule Wajerumani walikuwa wameelemewa na vita kutoka kwa Abushuri bin Salim bin Harith akiwa Pangani na Chifu Mkwawa kutoka Kalenga, Iringa. Wajerumani walihisi kuwa ikiwa Wazulu walikuwa walikuwa wamewasimamisha Wareno katika vita wakashindwa kupata ushindi kwa urahisi ëwashenzií wa Tanganyika hawataweza kufua dafu mbele ya mbinu za Wazulu za vita. Kwa ajili hii Sykes Mbuwane, Affande Plantan na Wazulu wengine walichukuliwa na Wajerumani waje kuongeza nguvu majeshi ya Wajerumani ambayo yalikuwa yanapambana na Chifu Mkwawa wa Uhehe na Abushiri bin Salim Mwarabu kutoka Pangani ambae alikuwa anapinga utawala wa Kijerumani katika Pwani ya Tanganyika.

Efffendi Plantan, Sykes Mbuwane na mamluki wengine wa Kizulu walikuja Tanganyika katika meli ya kivita ya Wajerumani iliyotia nanga Pangani mwaka 1894. Wazulu hawa walitokea Inhambane, Msumbiji iliyokuwa ikitawaliwa na Wareno. Kijiji chao kilikuwa kinajulikana kama Kwa Likunyi. Mjerumani alyewaleta toka huko alikuwa na sifa ya kuwa mwanajeshi na mvumbuzi, Harmine von Wissman.''
 
Huyu mzee sykes alikuwa mtu mkubwa mbona shulen hatukumsoma
 
Nyakageni,
Baba yangu hakuwa na mchango wowote katika siasa.
Akina Sykes ni Wazulu.

Dully ni mjukuu wa Abdul Sykes.
Na dully ni Abdull kumbe kalithi jina la babu yake ,hakika walikuwa watu wakubwa ila sijui kwa nini hatuwasomi mashuleni
 
We kweli Duduwasha,,,povu jingi utumbo mtupu unaandika. Kitabu chako kiko wapi au chuki na wanywa kahawa?


Nimekudharau uliposema amesubiri wazee wafe ndio aandike kitabu. Hujui kaa kimya
 
Shukran Sheikh...ila nikuulize vipi mbona huyo mtoto wa Hamza aliitwa "Rose" ilhal rose ni jina la kikristo?
 
CDG,
Hiyo picha niko Azam TV angaalia kitabu nilichoandika miaka 19 iliyopita.

Nilishasoma vitabu vyako viwili mwaka 2014-2015 nlipewa Magomeni Dsm...kuna contents nyingi nzuri ambazo kwingine sijawahi kuzisoma.

Big up, ila kwanini huwataji wakristo walioshiriki kupigania uhuru?

Au unataka tuanzishe ile mijadala ya zamani...eeh!
 
Yamagashi ningechukia ungeona lugha kali.

Mimi nakujibu nakufahamisha kuwa ondoa hasad, kejeli nk. hiyo ni historia hata kama huipendi haiwezi kubadilika.
Sawa...ila hebu tuambie leo hii hakuna Wakristo pia waliohusika katika kupigania uhuru?

Au walipigania ila hukuwafanyia wao utafiti?
 
Napinga hilo la aina ya kujibu swali kupitia swali.

Hapo utakuwa umeuliza kwani hujatoa jibu.
 
We kweli Duduwasha,,,povu jingi utumbo mtupu unaandika. Kitabu chako kiko wapi au chuki na wanywa kahawa?


Nimekudharau uliposema amesubiri wazee wafe ndio aandike kitabu. Hujui kaa kimya
Wewe hata ukidharau kwangu your too young kuweka ligi na Mimi... Namaanisha wewe hay exist kabisa... Mimi narekebisha waongo.. Hivyo tulia usome na ujifunze... Uujue ukweli.... Historia sio movie au hadithi ujaze uongo ili unoge...
 
Na dully ni Abdull kumbe kalithi jina la babu yake ,hakika walikuwa watu wakubwa ila sijui kwa nini hatuwasomi mashuleni
Ukubwa wao ni katika kufanya nini?

Wayajua au wewe shabiki?

Hebu tupe darsa bibie....!
 
Nice History
Wanamajlis,
Ukweli ni kuwa historia hii niliyoandika na kitabu kuchapwa Uingereza mwaka 1998,
''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924- 1968)The Untold Story of the Muslim
Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, Londn ilichoma na
kuwastua wengi sana.

Kwa nini iliwashtua wengi ni kuwa wanahistoria takriban wote waliaanza kwa kusema
kuwa harakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika zilianza na Mwalimu
Nyerere
1954.

Mimi nilirudi nyuma sana nikaanza na historia ya African Association na nikitumia kile
kinachoitwa, ''biographical approach,'' na kwa kusoma nyaraka za ukoo wa Sykes nikaja na
historia mpya kabisa kwa wengi.

Lakini kubwa ni kuwa wengi katika mashujaa wa uhuru wa Tanganyika walikuwa ni wazee
wangu hapa Dar es Salaam na wakifahamika kwa sifa hiyo.

Hili nimelisema mara kadhaa hapa jamvini.
Sina haja ya kurudia.

Wengi walipoona majina yale ya Waislam sijui kwa nini hawakupenda.

Lakini ukweli ni kuwa hawa ndiyo walokuwa wameachwa kutajwa katika historia rasmi ya
TANU iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni mwaka wa 1981.

Kuhusu Wakristo katika kupigania uhuru wa Tanganyika walikuwapo na ukipitia faharasa
(index) ya kitabu utakuta majina yao.
 
shikamoo mzee Mohamed Said.

wakati unaendelea kutuelimisha kuhusu historia isiyo na shaka ya aziz ally, abdulwahid sykes na wazee wengine mashuhuri wa dar es salaam wa wakati huo walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika harakati za kudai uhuru,naomba kufahamu ushiriki wa waswahili waliokuwa na asili ya kinubi toka sudani.

inasimuliwa kwamba wengi wa hawa askari shupavu wa kinubi,waliletwa tanganyika ama na muingereza au mjerumani kusaidia ktk harakati zao za kusambaza ukoloni.

pia inasimuliwa,baada ya miaka mingi kupita wakiwa ktk ardhi ya tanganyika,hawa wanubi walioa wanawake wa kiswahili na kuzaa nao watoto,pia walishiriki kikamilifu ktk vuguvugu la kudai Uhuru.

wengi wao walikuwa na makazi kariakoo na mji wa kilwa.

kama hutojali,naomba kufahamu majina yao na mchango wao ktk kudai Uhuru.

nimewahi simuliwa kuwa,wakati nyerere alipokuwa anatafuta uungwaji mkono miongoni mwa watanganyika ili awaunganishe kudai uhuru,alipokuwa anaenda kilwa,alikuwa anafikia ktk nyumba ya mzee mmoja mashuhuri wa wakati huo mwenye asili ya kinubi,mzee huyo pia alikuwa na makazi ya kudumu kariakoo.naomba kufahamu jina lake na ushiriki wake ktk kudai uhuru.
natanguliza shukrani.
 
Wewe hata ukidharau kwangu your too young kuweka ligi na Mimi... Namaanisha wewe hay exist kabisa... Mimi narekebisha waongo.. Hivyo tulia usome na ujifunze... Uujue ukweli.... Historia sio movie au hadithi ujaze uongo ili unoge...
Mkuu hebu jaribu kupinga hicho unachosema ni uongo kwa kuweka wewe ukweli wako, bila hivyo tutakutafsiri kua una chuki fulani tu na wivu usio na maana,huwezi kusifiwa kwa kukashifu watu humu bali tutakusifu kama utajenga hoja ili ueleweke kuliko kukashifu watu usiowajua kisa tu coz upo nyuma ya keyboard,ustaarabu hauuzwi dukani,tujenge kuheshimiana ili tuelimike sote,

One love.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…