Azzan Zungu ataka mazungumzo Bandari ya Bagamoyo kunusuru tatizo la ajira

Azzan Zungu ataka mazungumzo Bandari ya Bagamoyo kunusuru tatizo la ajira

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mbunge wa Ilala ameomba muongozo leo Bungeni Dodoma kuhusu mpango wa Serikali kuanzisha mazungumzo tena ya bandari ya Bagamoyo kutokana bandari ya Dar es Salaam kuzidiwa na kutokuwa na uwezo wa kuingiza meli kubwa. Zungu amesema bandari ya Bagamoyo itapelekea kuanzisha viwanda, kuleta ajira na gateway kwa Bagamoyo.

Zungu amesema ulikuwa mpango wa Serikali kuanzisha Industrial Park Bagamoyo lakini wakapata mgogoro wa kimkataba.

 
Bandari hii ni muhimu sana lakini tu alimradi usiingilie utendaji kazi wa bandari zingine wala mamlaka zetu za mapato zisiwekewe vikwazo za ukusanyaji mapato katika bandari hii mpya ya Bagamoyo aidha ni bora tukaziuza ndege zote tukabaki na mbili tu na fedha zote zikaingizwa katika mradi wa BAGAMOYO.
 
Zungu ulionelsna ukigawa fedha uchaguzi mkuu 2020. Sasa unatafuta 10% huko bagamoyo. Au ulinunua viwanja 1000 sasa unatafuta mji uhamie huko
Kuna watu weengi sana waliwekeza kwenye ardhi huko Bagamoyo sasa JPM akawapiga chenga kama alivyofanya maeneo ya Nala Dodom

saivi wanataka wakaiuzie Serikali ardhi yao ikiwa mraji utaanza
 
Kuna watu weengi sana waliwekeza kwenye ardhi huko Bagamoyo sasa JPM akawapiga chenga kama alivyofanya maeneo ya Nala Dodom

saivi wanataka wakaiuzie Serikali ardhi yao ikiwa mraji utaanza
Wabunge wetu ni mbumbu, how we vote for imbeciles, I just can’t understand. Funga bunge na Pima akili zao, 99% ni vichaa, they have serious mental issues!
 
Bandari hii ni muhimu sana lakini tu alimradi usiingilie utendaji kazi wa bandari zingine wala mamlaka zetu za mapato zisiwekewe vikwazo za ukusanyaji mapato katika bandari hii mpya ya bagamoyo aidha ni bora tukaziuza ndege zote tukabaki na mbili tu na fedha zote zikaingizwa katika mradi wa BAGAMOYO.

Jambo la msingi ni kuboresha bandari zilizopo za dar, Tanga na Mtwara... Bandari ya bagamoyo ni ufisadi na mwiba kwa bandari zilizopo...

Kuboresha bandari ya tanga ni vizuri ukizingatia bomba la mafuta kutoka Uganda litaishia pale...
 
Siungi mkono Kujenga hii Bandari.

Na sijui kwa nini inashikiwa bango bila maelezo ya kutosha kuhusu Bandari ya Dar, Tanga na Mtwara.

Hivi uhitaji wa hii Bandari ni mkubwa kiasi hicho hata tuache shughuli nyingine tuweke nguvu hapo?.
Uchumi wa Singapore na Malaysia wanategemea bandari mkuu,kwa hiyo bandari ni mojawapo ya vyanzo vya mapato kwa asilimia kubwa vyenye uhakika kwa mwaka
 
Ni yaleyale kama ya ujenzi wa viwanja viwili vya michezo sehemu moja, Uwanja wa Benjamin Mkapa na ule Uhuru.

Kuna faida nyingi za kiuchumi tutazipata kama nchi endapo bandari za Mtwara na Tanga zitakapopanuliwa na kuweza kupokea shehena kubwa za mizigo badala ya kung'ang'ania ujenzi mpya wa bandari ya Bagamoyo ambayo ipo karibu sana kijografia na bandari ya Dar es Salaam.
 
Kuna watu weengi sana waliwekeza kwenye ardhi huko Bagamoyo sasa JPM akawapiga chenga kama alivyofanya maeneo ya Nala Dodom

saivi wanataka wakaiuzie Serikali ardhi yao ikiwa mraji utaanza
Mchezo Kama huo aliuufanya pia Manji huko Kigamboni, baada ya kustuliwa na watu wa ndani kuhusu Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kupita,yeye Manji akawafuata Wakazi wa pale kwenye mradi na kuwarubuni kununua Viwanja vyao kwa M7 kwa kila mwenye kipande chake Cha Aridhi na kweli wengi walimuuzia maana walikuwa hawajui kuwa mradi tayari unakuja, na wale wachache waliojuwa walitishwa kuwa watanyanganywa Aridhi yao na Serekali,basi kwa haraka haraka nao wakakubali kumuuzia manji, japokua kuna wachache sana wao walichukua pesa kwa Manji na bado wakamkatalia, hao wengi wao walikua Wanajeshi wastaafu,

Sasa Mradi ulivyo kuja tu,ukakuta tajiri Manji ndiyo mmiliki wa eneo lile, Sasa ndiyo ikabidi wakae na Manji awauzie,Sasa hizo bei zilizopigwa hapo! Manji alipiga pesa ndefu sana,na ndiyo maana itachukua muda mrefu sana lile Daraja la Kigamboni kurudisha pesa zote za Mradi!! Matajiri wengi ni Wapigaji!!
 
Ngoja tuunge dot....

  • Ndugai
  • Zungu
  • Bagamoyo sugar
  • Singh
  • Msofe
  • Kutosikika/kung'aa kwa PM
  • VP kupotea kwenye medani
  • Katiba mpya kukataliwa
  • Kufuta mashitaka na kuachiwa tycoons
  • Manji kurudi
  • Kusafisha Kamati kuu
  • Wateule wa awamu ya nne kurudi
  • Raisi kusisitiza ulazima wa Industrial park bila kuweka bayana nini ilikuwa mbaya na nini imeboreshwa, kwa kutuwekea bayana tuchambue wenyewe.
  • Bandari zote 3 zinapanuliwa kwa gharama kubwa, udogo huo unatoka wapi?
  • Znz kuchomoza kwenye picha ya Tanganyika
  • Mikopo lukuki ndani ya siku 100
  • Kuongea na Jin(Bandari ya bagamoyo itahusika)
  • Rais wa Botswana na BFM
  • Znz, Dar, Dom cylce
  • Kulipa malimbikizo na kupandisha madaraja

Mungu nisaidie niione TZ ijayo, maana nimeikutia kati, sijui ilipotoka, sijui inapokwenda, ila najua ilipo kwa sasa; Kazi iendelee.
 
Hivi ni lazima mumtukane mtu ndiyo mutafanikiwa kwenye kutoa hoja zenu kwenye mitandao?

Nauliza tu jamani.
 
Back
Top Bottom