Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

Badala ya kupendekeza wafutiwe posho za kukaa Bungeni ili kuipunguziwa serikali mzigo, anapendekeza aina nyingine ya kodi wakati kuingia tu mtandaoni tunakuwa tumelipa kodi kupitia vifurushi!!
Hapo Zungu kwa ushairi huu anajipendelea mwenyewe kwa vile hiyo kodi inaliwa moja kwa moja na yeye kama mbunge. Bila shaka anahofia uwezo wa serikali kulipa posho zake. Ubinafsi gani huu!
 
Atakubali akatwe huyu mjinga?

Hii compliment ya "mheshimiwa" nadhani ifikiriwe upya, kuna watu wanadhalilisha sana hii title.
Yamejazana mule ndani,kazi yao ni kupiga makelele na kugonga meza tu,kwa kuwa yana uhakika ya kuchota mihela bure bila kuifanyia kazi, yanakera sana hayo majinga
 
Hivi kwanini asingeshauri hata namba za wabunge zipunguzwe, anagalau tuwe na majimbo machache, pocho ya bungeni ifutwe wabaki wakitegemea mshahara tu kwa sababu kuingia bungeni ni kama mfanyakazi mwingine ameingia kazini, hivi kwanini asingesema gharama za uchaguzi zifutwe, anyway, wanyonge watalipishwa, wanyongaji watafaidi.
 
Serikali ifanyie kazi Ushauri huu Mzuri sana. Hata isipoitwa kodi ya Uzalendo lakini HAKIKA HIKI NI CHANZO KIZURI SANA CHA MAPATO/KODI KWASABABU TANZANIA HII MTU YUPO RADHI AKOSE VINGINE LAKINI SIO KUKOSA BANDO LA KUCHATI KWENYE GROUP NA TWITTER KUFUATIA MANGE, KIGOGO, KAJALA NA PAULA
Kuna ya kuhuisha fikra. Simu sio anasa kwa zama tulizonazo. Gharana za vifurushi vya simu ilipaswa vilegezwe zaidi, kwa sababu soko la kidigiti ni sehemu nyingine ya ajira kwa vijana, tusirudishane nyuma.
Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi. Watunza sera waongeze ubunifu tu ambao hauleti kero kwa wananchi.
 
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533
Hakuna sheria kama hiyo, hivyo pendekezo halitekelezeki. Kwani kinachokatwa kwa sasa kinahesabiwa kama nini kutoka kwa mtumiaji wa mtandao (vifurushi vya maongezi, vifurushi vya meseji, vifurushi vya data, kila shilingi mia unayoingiza kwenye simu inakatwa shilingi kumi na nane.

Uzalendo ni hiari ya raia sio shurutisho. Tatizo wawakilishi wa wananchi hamjui namna bora ya kuibua vyanzo vipya vya kodi visivyo kero. Au wanafikiri kufanya hivyo kuwaadhibu watumiaji waachache kuhoji mambo?

This man has to step down, he failed to generate grand tax collection from his constituency despite being the leading host of all milionnaires and billionnaires invested at the city center-ILALA.
 
Inaumiza sana kumtegemea kama mwakilishi wako wa jimbo...pia itaumiza zaidi kama 2025 atachaguliwa kurudi bungeni...

Lazima ifike wakati tutambue wawakilishi wetu wananchi wakishapata shavu wanawaza matumbo yao na familia zao..
 
Gharama za mawasiliano zipo juu sana hapa tanzania ukilinganisha na nchi nyingine wengi tunatamani zipungue ili wengi waweze kuzimudu halafu anatokea mjinga mmoja anataka tena tuanze kukatana hela.Ama kweli wabunge wa ccm hawaishiwi vimbwanga.CCM mnataka tutembee na chupi kichwani ndio mjue sisi tu wazalendo?
 
Yani kwa hesabu hiyo anamaanisha kila siku kila mtu akatwe Tshs. 18,000 kwa siku, ndio ipatikane hiyo bilioni 540 kwa siku. Hii ni kauli ya aliyevimbewa madaraka na ukwasi.
 
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758533

Kwa nini wao hawaoni wakilipia kodi mapato yao yote tu kama tunavyolipa sisi, pesa nyingi na hata zaidi ya anazosema zitapatikana?

Uzalendo kwao ni kutokulipa kodi?

Wakileta kodi hii ya zungu simu tunapiga chini. Bila ya minimum force hawa jamaa watatupeleka puta sana.

Hiiiiii bagosha!
 
Kila muamala wa simu tunalipa kodi. Yeye aseme tu wanatafuta njia ya kurudisha kodi ya kichwa pengine mambo ni magumu huko kwenye chungu kikuu. Tumeona kwenye yatokanayo na bei za miamala.
 
Back
Top Bottom