Wakati tunajadili mishahara ya hawa watu tusisahau yafuatayo especially kwa hizi Urban Radios.
1. Approach vs Approached: Miaka ya nyuma nilikuwa nafanyia taasisi moja ya kifedha.
Sasa sijui ilikuwa ni uhaba wa Competitive Bankers au vipi lakini miaka ile haikuwa ajabu Staff wa Bank X kuwa approached na Bank Y kwamba ukafanye kazi kwao!
Ukishakuwa approached namna hii, unaahidiwa mambo mazuri including MSHAHARA NA BENEFITS.
So, kwenye media hapa Bongo, kuna layer fulani ya Watangazaji ambao mara nyingi wanakuwa approached na media zingine! Watu kama akina Kitenge, Edo Kumwembe, and the like huwa wanakuwa approached kujiunga na media fulani.
Hao wanalipwa vizuri sana!
2. Hao Watangazaji wanakuwa approached kwa sababu wana uwezo wa Kuvutia Advertisers kutokana na influence yao.
Kutokana na hilo, hao watu ni Mtaji Mzuri sana kwa redio. Aidha, kutokana na influence yao pia wanakuwa na fursa ya kuwa na connection na watu mbalimbali.
Connection hizi sio tu zinawasaidia kuleta deal mpya za matangazo kwenye redio bali pia ku-lobby pale ambapo hazipo.
Namba 2 hapo juu inawafanya wawe ni Ng'ombe Mzalisha Maziwa, na hivyo kuendelea kuwa na soko kubwa kwenye soko la ajira za Urban Radio.
3. Hizi media huwa zinatoa kamisheni kwa wale wanaofanikisha kuleta matangazo!
Sasa kwa sifa niliyotaja #2 hapo juu, unakuta mara nyingi wanakuwa miongoni mwa Staff wanaotandika kamisheni za kutosha!
NOTE: Usidhani watangazaji wote wapo sawa! Kama huna sifa nilizotaja hapo juu, na kwahiyo unategemea sana mshahara, basi Utangazji ni Kazi Iliyojaa Njaa!!
Aidha, sio kila mtangazi unayemsikia kwenye redio au kumuona kwenye tv ni Mwajiriwa!
Wapo wengi tu ambao wanapiga deiwaka kwa matarajio sooner or later ama watapata replacement hapo hapo au wataonekana na media zingine na hatimae akalamba ajira!
So, usimuone X aliye Wasafi au EFM analia njaa ndo ukadhani hapo Wasafi au EFM kuna njaa kali kihivyo... unaweza kukuta anapiga Deiwaka tu au ndo wale wasioleta cha ziada kwenye redio!