Tupe na ya kiislam si mnasema Yesu alikuwa Muislam.. tuelezee alisulubiwaje?
Bila kusahau ile story ya Suleiman na Jeshi lake la Kuku lenye kamanda wao pia... Huwa nacheka sana nikisoma Quran.
Muslim wanasema Yesu hajafa yupo Mbinguni lakini Koran Chapter 5 :75 isome kwa kiarabu maana kwa kiswahii na english wameichakachua hawa watumwa wa uongo kha.. inasema Messenger wote waliopita walikufa. kama Yesu ni Messenger alikufa nawaambieni Yesu ni Mungu na yupo Alive contradiction kwenye kuran kama zote..
5:75
مَّا ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌۭ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٌۭ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ ٱلطَّعَامَ ۗ ٱنظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ثُمَّ ٱنظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
The Messiah, son of Mary, was no more than a messenger. ˹Many˺ messengers had ˹come and˺ gone before him. His mother was a woman of truth. They both ate food.1 See how We make the signs clear to them, yet see how they are deluded ˹from the truth˺!
Ukitaka hakika ni kweli kuwa mtu ye yote anayesoma hizi hizi Injili ziliomo katika Biblia kwa uangalifu ataona ushahidi wa nguvu kuwa huyo aliyetundikwa msalabani hakufa hapo msalabani, bali alionekana tu kama amekufa.
Katika Injili hizo hizo upo ushahidi mzito wa kuonyesha kuwa yamkini sana kuwa huyo aliyetundikwa msalabani hakuwa Yesu Kristo kabisa, juu ya kuwa waandishi wa Injili walikuwa wakiamini kuwa ndiye Yesu.
Hebu natuuchungue ushahidi huo.
Ni wazi kuwa Yesu wakati ule hakuwa mtu maarufu katika mji wa Yerusalemu. Alikuwa ni mgeni kwa wale waliokuwa wakimsaka.
Yeye alikuwa mshamba, ametoka huko Galilaya. Tangu kuanza kuhubiri ni kiasi ya miaka miwili mitatu tu, naye akitanga tanga huku na huku bila ya kutulia, hata hakuwa na pahala pa kuweka kichwa chini. (
Mathayo 8.20).
Mnamo wakati huo hakupata kwenda Yerusalemu isipokuwa mara chache tu. Marko anasema alikwenda mara moja, na Yohana anasema mara nne. Jinsi ya kuwa hajuulikani vyema hata ikalazimu Yuda amtambulishe kwa kumbusu; alisema:
"
Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni." (
Mathayo 26.48).
The Interpreter's Bible kutafuta kijisibabu kwa huko kumuashiria kwa kumbusa inasema:
"
Yesu angejuulikana bila ya ishara, lakini wale waliokuja kumkamata hawakutaka kubahatisha kwa sababu makosa yaweza kutendeka kwa wepesi wakati wa usiku, na khasa pangetokea pata-shika."
Vyo vyote vile iwavyo, ikiwa ni kwa ugeni, ikiwa ni kwa giza la usiku, au ikiwa kwa ghasia na fujo lililokuwapo, ni jambo lilioelekea sana kumkosea Yesu akakamatwa mtu mwingine.
Wafuasi wake wote walimkataa, hata Petro naye ambaye alikuwa karibu mno na Yesu katika wanafunzi wake wote, naye pia alisema:
"
Simjui mtu huyu". (
Mathayo 26.74).
Basi je, tuukatae na kuutenga kando ushahidi wa wanafunzi wake wote wanaoitwa Watakatifu tuukubali wa khaini, msaliti mmoja, Yuda?
Tena hata yeye hakuutoa ushahidi wake mahkamani, baada ya kuapishwa, bali huko huko kwenye vurugu kizani, tena ni kwa ishara tu ya kumbusu, ambayo tunaambiwa na waandikaji kwamba walikubaliana baina yake Yuda na askari wa Kirumi faraghani, ambako bila ya shaka yo yote hao waandikaji au waliowasimulia hawakuwapo.
Hayo ni mambo ya dhana tu. Kuambiwa tena kuwa hayo nayo yalikuwa ni kutimiza bishara za Agano la Kale, au zake mwenyewe Yesu, ni hadi ya kuilazimisha imani ikubali lisilokubaliwa na akili.
Tena hebu tuzichungue jawabu alizozitoa mshtakiwa huko mahkamani. Hadi yake tunaweza kusema kuwa hizo jawabu ni za ubabaishi.
Injili tatu za mwanzo, nazo ndizo zenye kueleza maisha ya Yesu, zimeshindwa kutoa ushahidi hata mmoja kuthibitisha kuwa ni nani khasa huyo mshtakiwa.
Injili ya Luka inasimulia kuwa alipoulizwa barazani: "
Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie."
Akawaambia: "
Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa."
Na alipoambiwa: "
Basi wewe ndiwe Mwana wa Mungu?"
Akawaambia: "
Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye."
Maana ya kauli hiyo sio maana yake kukubali yasemwayo, bali ni kukanya na kumsukumia jukumu yule amuulizae na kumtuhumu kwa hayo - yeye hakimu pamoja na wote waliozua hayo mashtaka.
Na vyo vyote alisemalo hasadikiwi, kwani waliomkamata wamesha kata shauri kuwa yeye ndiye Yesu Kristo, na hali siye. Basi hapana haja ya kusema lo lote.
Katika Injili ya Marko tunasoma:
Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?
Akajibu, akamwambia: "
Wewe wasema." Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi.
Pilato akamwuliza tena akisema:
"
Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki!" Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu.
Kama alivyojibu kuwa yeye si Mfalme wa Wayahudi, hali kadhaalika si Mwana wa Mungu, wala si Kristo. Kwa suala zote tatu hizo mshtakiwa anasema kuwa hayo wanayasema wale wanaomshtaki, si yeye.
Kadhaalika Injili ya Mathayo inatwambia:
Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema,"Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?"
Yesu akamwambia: "
Wewe wasema."
Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno.
Ndipo Pilato akamwambia:
"
Husikii ni mambo mangapi wanayokushuhudia?"
asimjibu hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana. Na sote lazima tustaajabu. Ikiwa yeye ni Yesu, Kristo, Mwana wa Mungu, kama ilivyodaiwa kuwa anadai, kwa nini hakubali? Hapo mahakamani sipo hasa pa kueneza ujumbe wake?
Zingatia vyema kuwa hadithi hizi ziliandikwa miaka mingi baada ya kutokea hayo mambo, tena zimeandikwa na watu wenye kuamini kabisa kuwa huyo aliyekamatwa na kusalibiwa ni kweli Yesu Kristo, mwana wa Maryam.
Juu ya hivyo hata wao hawakuweza kuleta ushahidi wo wote wa kweli au wa kubuni usipokuwa ule wa Yuda, msaliti.
Huyo mshtakiwa hakukiri hata mara moja kuwa yeye ndiye Yesu anayetuhumiwa.
Na wanafunzi wake nao hawakumtambua wala hawakukiri kuwa wao wanamjua, bali walikataa kwa nguvu, na wakamkimbia.
Tukizingatia haya kwa usafi wa nia na kwa kutumia akili zetu bila ya kugubikwa na mawazo na imani tulizozoeshwa tangu utotoni, na pia tukatia maanani yale tuliyokwisha yasimulia yaliyomo katika Injili nyenginezo zisiokubaliwa na Kanisa, pamoja na nyaraka za kale zilizogundulikana karibuni zinazotufahamisha nini ilikuwa imani ya Wakristo wa asli ya kwamba Yesu hakufa msalabani, ukweli wa Qur'ani unathibiti kwa uwazi kabisa:
Na kwa kusema kwao (Mayahudi): Sisi tumemuua Masihi Isa mwana wa Maryam, Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala hawakumuua wala hakumsalibu, bali walifananishiwa. Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi juu yake, isipokuwa wanafuata dhana tu. Na hawakumuua kwa yakini.
(Qur'ani) An Nisaa 4.157