GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
"Kila Matokeo ya Mitihani yakitoka Wizara ya Elimu akina Mkenda huniletea Vitabu vikubwa pamoja na Flash hivyo nikiiweka tu katika Computer yangu Kwanza huanza Kuangalia Kwetu Mkoani Kusini Unguja kisha nikiona huwa nasema Mama yangu ni nini hiki? Yaani Mkoa anaotoka Rais ndiyo unaongoza kila mara kwa kufanya vibaya katika Mitihani nchi nzima? Sasa nimewaagiza tuanze kulifanyia Kazi ili Kuuinua huu Mkoa na Kuondoa Aibu hii" amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Chanzo: Nukuu ya Rais ya Redio One Leo.
Leo nimeyakumbuka maneno na Mafundisho ya Mhadhiri wangu Kipenzi wa Somo la Print Media, Critical and Logical Reasoning SAUT Mwanza 'Genius' Fr. Bishop. Dk. Bernadine F. Mfumbusa ( anayehudumu Kondoa kwa sasa ) tulipokuwa Darasani aliwahi kutuambia kuwa kabla ya kuanza Kumchambua Mtu Kimantiki ili tusisumbuke nae au asitupotezee sana muda tuanze Kuifuatilia Historia yake ya Kimaisha, Elimu na Uelewa ili tuweze kupata Hitimisho sahihi juu yake.
Hivyo nami GENTAMYCINE baada ya Leo kuisikia hii Nukuu Natangaza rasmi Kustaafu Kumjadili Mtu kwani nimegundua kuwa kumbe nilikuwa namuonea Mtu bure na tena huenda napaswa hata Kumuomba Radhi kwani kama tu Mkoa wake Umetukuka kwa kuwa Kinara wa Matokeo mabaya Tanzania nzima Mimi ni nani nimlaumu wakati nimeshajua Chanzo cha Tatizo ni nini?
Ngoja nami sasa nijiandae Kisaikolojia kuwa Mvumllivu kwa Tanzania ya 2021 hadi 2025 na ile ijayo ya 2025 hadi 2030.