Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Nenda kaharishe huo uvundo hizo pesa ulizopewa na mafisadi zimekufanya uvimbiwe
 
Watu wa aina ya huyu mleta mada ndio wanaowajengea ujinga watanzania mpaka wanachelewa kuona mantiki pana ya mabadiliko ya uendeshaji wa bandari yetu.

Ni watu hawana kabisa mahusiano na biashara ya bandari, yeye anapiga siasa tu za kina Mangungo ili kuteka akili za wengine wasio na biashara yoyote ile na masuala ya bandari.

Rwanda, Congo wameshasaini mkataba wa uwekezaji, watu wa dunia ya karne ya sasa wanaangalia zaidi fursa za kutengeneza pesa kama nchi.

Huyu bwana Jilala yeye kaamua kubakia katika karne ya zamani, anakuja na hoja zilizopitwa na wakati za machifu walioishi zaidi ya miaka mia moja iliyopita, this is rubbish.
 
Hiyo mentality hakuna hata mmoja anayeweza kuiongelea, watanzania wa miaka ya sasa wanachojua ni wizi, kupata pesa za kutumia mwisho wa wiki, za kulewa mapombe makali mpaka saa kumi na mbili asubuhi.

Watanzania wanafikiria pesa za chap chap, za kuiba kila inapowezekana ili akaufanye ufalme wa bandia club fulani.

DPW pale bandarini wanakuja na nidhamu mpya ya ufanisi wa kazi, hakuna tena pesa za mkupuo za kutanua kila ijumaa na jumamosi, watanzania wanaona chaka lao la pesa za bure bure linakwenda kuzimwa jumla. Hizi kelele hazishangazi hata kidogo.
 
Hakuna ukweli wowote. Hakuna mkataba wa miaka 100 unaokwenda kusainiwa.
 
Ndio hapo utajua majizi ndio yanaponda uwekezaji
Hakuna utamaduni wa kufanya kazi kwa nidhamu

Kuna wakati sijui waziri gani alienda kufunga gate la kazini ili waliochelewa wasiingie
Lakini kwa kuwa na yeye alikuwa ni mvivu wa kuwahi ilibidi suala Zima life

Hawana ari ya kazi wala kujituma wao wanataka shortcuts tu

Kulala sana, hongo kwa wingi na wizi, utapeli na rushwa ndio imo kwenye akili za wengi mpaka viongozi
Hapo usitegemee maendeleo
 
Huu ujinga hatuwezi kukubali!! Eti tumekubali kabla ya mkataba!! Kilichopitishwa ndio mkataba mama na mingine ya kiutekelezaji itapitishwa!! Wizi mtupu!! HATUKUBALI!!
 
Huu ujinga hatuwezi kukubali!! Eti tumekubali kabla ya mkataba!! Kilichopitishwa ndio mkataba mama na mingine ya kiutekelezaji itapitishwa!! Wizi mtupu!! HATUKUBALI!!
Hakuna unachokijua, tulia uelimishwe mambo mengi. Mikataba haijasainiwa bado, na itakuwa kadhaa kulingana na sekta husika ya bandari.

Hakuna mkataba mama mpaka dakika hii uliyosainiwa kwenye hii biashara, kuna agreement ya IGA, ambayo ni kifupisho tu cha mengi yanayokwenda kujadiliwa katika michakato wa uandishi wa hiyo mikataba.
 

Bado una msimamo huu?
 
Bado una msimamo huu?
Bado ninao na siku zote nitakuwa nao. DPW yupo bandarini na Adani pia kaanza kazi.

Tulidanganyana kwamba IGA ya DPW itazuia shughuli zote za bandarini kwa maana ya wao kuwa na utawala wa sekta nzima ya bandari. Hili ni jambo wengi wetu tulikuwa hatuna ufahamu nalo.

Ukisikia bandari ya Mtwara au Mbinga inataka uwekezaji tafuta mwekezaji na uende nae pale TPA, kama anakidhi vigezo mtapewa kazi ya kuendesha hizo bandari bila ya kuitazama IGA ya DPW inasema nini.
 
Dunia haitusubiri tuamke yenyewe inakwenda kasi tu. Ni juu yetu kuliwahi basi lisilo na muda wa kumsubiri abiria ajivute wakati wa kupanda.

Sekta yetu ya bandari bado ipo chini, nguvu kazi pale TPA bado haina uelewa wa masuala mengi ya bandari na ufanyaji kazi wa kisasa, sisi tulitakiwa kuchangamkia hizi fursa za uwekezaji kuliko kuja na kejeli za Chief Mangungo.

Ni aidha tuitafute elimu kwa kasi na nguvu au tuendelee kuja na uzi wa malalamiko kama huu wenye kuwajaza ujinga wasomaji wengi kana kwamba tunaibiwa.

India wamempa DPW fursa ya uwekezaji, sisi na wao nani wapo juu kiuchumi na kimaarifa?.
 

Faida yao ni ipi?
 
Faida yao ni ipi?
Gawio la hazina kuongezeka ni faida kubwa sana kwenye uchumi wa nchi.

Haraka ya ushushaji na upakiaji wa makasha pale bandarini yanafanya kazi nyingi ifanyike ndani ya muda mfupi.

Bandari yetu kuwa kimbilio na chaguo la waingizaji na watoaji wa bidhaa pia ni heshima kwa Tanzania.

Elimu ya masuala ya bandari inayotolewa na DPW kwa mujibu wa vipengele vya mkataba wa DPW, kwa wale wafanyakazi wanaopewa mafunzo ni faida kwa taifa letu katika suala zima la kuongeza wataalam.
 
kama itafanya vyema ningefurahi kama wangeipa hiyo kampuni hata miaka 100. shida ni whether itakuwa bora. hata ukimpa miaka michache kama anafanya vibaya kuna faida gani?
 
kama itafanya vyema ningefurahi kama wangeipa hiyo kampuni hata miaka 100. shida ni whether itakuwa bora. hata ukimpa miaka michache kama anafanya vibaya kuna faida gani?

Faida yake unafanya mabadiliko haraka
 

Umeshaipata sasa hiyo haraka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…