Baada ya barua ya kujiuzulu, Polepole atambue kwamba Press Conference ina jambo moja kwake, akisimama nchale akikimbia nchale

Wengi wetu, walio na wasio wanachama au mashabiki wa CCM, tumeiona barua ya kujiuzulu ya Polepole, na sababu za yeye kujiuzulu. Kuna waliompongeza na kumwona shujaa wa Tanzania, na kuna waliomlaani na kumwona msaliti na mnafiki kwa CCM na Tanzania.

Na ni wazi kwamba CCM watakuwa wamemfikia kwa kila katika namna ya kujaribu kuzima moto aliouwasha. Kina Makala, kina Nchimbi, huenda hata kina Kikwete, watakuwa wameambiwa wajaribu kuongea nae, wajaribu kumpooza. Na wengine wengi watakuwa wamemfikia kusema piga zaidi kwenye mshono, piga, tuko nyuma yako mzee baba!

Sasa je, Press Conference ya Polepole ni matokeo ya hizi jitihada za kumfikia Polepole ili alegeze au kukaza uzi juu ya barua yake ya kujiuzulu? Polepole atambue hadi sasa amejiweka kati ya makundi mawili - lile la CCM linalomtaka apooze moto aliouwasha, na lile la wanaomuona kuwa shujaa wa Tanzania na linamtaka achochee hata zaidi moto aliouwasha!

Haitakuwa rahisi kwa Polepole kuyaridhisha makundi yote mawili kwa kutumia Press Conference hii. Lazima kuna kundi mojawapo ataliacha lina hasira nae sana baada ya Press Conference yake - hatujui kundi lipi. Najua Polepole anajua, a man gotta do what a man gotta do!

Ndio maana ninasema kwa Polepole, Press Conference uliyoitisha ina jambo moja kwako; ukichimama nchale, ukikimbia nchale!
Slow slow atanywea tu. Kama Gwaji boy kanywea kama mkate kwenye chai itakuwa huyo slow slow?.
 
Kwa nini unadhani kuwa mtu mzima na akili zake, tena kiongozi, anaweza kuandika barua ya kujiuzulu huku akitoa sababu bila kuwa na uhakika na afanyacho? Kwangu mimi nadhani anataka kwenda kwa undani zaidi kuhusu sababu zake za kujiuzulu na ikiwezekana ajibu maswali. Barua na press ni vitu viwili tofauti.
 
Ndivyo tulivyodhani itakuwa kwenye press conference ya Gwajima. Kaishia kuongea utopolo mtupu
 
Gwajima hajaongea upotolo au niseme kwangu mimi naona hajaongea upotolo. Kwa mfano ujumbe alioutoa wa CCM kukubali ifanye marekebisho kwenye sheria za uchaguzi ni maoni muhimu sana sana hasa ikizingatiwa yeye ni CCM ambayo wengi hawataki.
 
Basi asiongee kwa namna ambayo anafanya CCM kufanya hivyo ni kutoa favor kwa Chadema. Chadema hawajaomba Reforms kwa CCM, kwa nini yeye analifanya sualahili kuwa la CCM?
 
Back
Top Bottom