Baada ya CCM kuondolewa madarakani Watetezi wake mitandaoni watakimbia na kutoweka ama watajificha

Baada ya CCM kuondolewa madarakani Watetezi wake mitandaoni watakimbia na kutoweka ama watajificha

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Hili jambo ndilo litakalotokea. Hawa wote mnaowasoma humu JF na kwingine wakitoka jasho la kwapa kutetea maovu ya CCM bila kujali utu wa binadamu, hawataonekana tena baada ya CCM kuondoka.

Hawa si watetezi wa bure, bila shaka wanalipwa. Hii ni kwa sababu hakuna binadamu yeyote mwenye akili timamu anayeweza kutoka mshipa wa shingo kwa ajili ya kutetea unyama, haitawezekana!

Hawa wanahangaika kwa vile wao wenyewe wanalipwa ama wazazi wao wanalipwa.

Hakuna mtu yeyote wa CCM katika hawa wanatoka povu humu atakayekubali kutetea uchafu wa CCM bila kulipwa, tena katika kipindi ambacho jumuiya ya kimataifa inatafuta majina ya wanaCCM ili washtakiwe, yaani hawa watetezi wa CCM hawawezi kufanya kazi iliyotukuka kama wanayofanya Wapinzani kama sisi bila malipo ya kukosoa utawala wa mabavu na kutetea Katiba ya nchi huku tukikwepa mishale ya sumu ukiwemo utekaji, risasi na wakati mwingine uchawi.

Hawa wote unaowafahamu hapa wanaojiita watetezi wa uzalendo ni wachumia tumbo wenye njaa kali sana, ambao kwao njaa ya tumboni ni muhimu kuliko utu.

Utetezi wa CCM ndiyo ajira yao ya kujikimu, hawana uwezo wa kutetea CCM nje ya madaraka na wengi watabadili ID ama watakimbia kujificha.
 
Watetezi wa wauza madawa ya kulevya mwisho 2020
Screenshot_20200215-062753.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • Screenshot_20200215-062826.jpeg
    Screenshot_20200215-062826.jpeg
    30.2 KB · Views: 16
Mi jambo linaloniuma kwa sasa,serikal ya ccm imebana uhuru wa kujieleza,na democrasia,ni aibu sana maamuzi kufanywa na mtu mmoja na kuathir nchi nzima.utekwaji na kukamwatwa na ubambikiwaji wa kesi,kwel maendeleo tunahitaj ila si kwa style ya udikteta.

Rais wetu anapaswa afaham haya...we need changes ila si kwa mabavu,smooth gradual change is possible
 
Hata ndoto ya mchana nayo pia ni ndoto kwa mjinga!

Nakumbuka kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, Freeman Mbowe alijiapiza baada ya kuota ndoto ya mchana kuwa kama CHADEMA haitaingia Ikulu katika Uchaguzi huo basi yeye atastaafu siasa! Leo hii bado yupo kwenye siasa na wale waliojaribu kumtingisha kwenye kiti Uenyekiti mwaka jana wamekiona cha ''mtema kuni'' huku ''Nyumbu wake'' wakiendelea kumshangilia!
 
Mi jambo linaloniuma kwa sasa,serikal ya ccm imebana uhuru wa kujieleza,na democrasia,ni aibu sana maamuzi kufanywa na mtu mmoja na kuathir nchi nzima.utekwaji na kukamwatwa na ubambikiwaji wa kesi,kwel maendeleo tunahitaj ila si kwa style ya udikteta..
Rais wetu anapaswa afaham haya...we need changes ila si kwa mabavu,smooth gradual change is possible
Weee hapa mbona unajieleza? Pumbavu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom