Sasa bandugu hasira za nini,naona mnakuwa waongo sana sana kupita maelezo,mimi nipo kijiji kimoja Tanzania kinaitwa Murutunguru ni kisiwa kadogo tu,najivunia maendeleo yaliopo na ninaendelea kuridhika.
Tatizo jingine nimeligundua muda mfupi hamridhiki na kidogo kinachoanza kuongezeka,maendeleo hayaji kwa kasi mnayoiota,hayo sio maendeleo ni wizi ,na ndio maana mnababaika sana, sana katika uongozi wa Mheshimiwa Magufuli maana mirija yote ameikata, Mlisahau moja ya lengo la kupata UHURU ni kuikata na kuiondoa mirija, tulifanikisha lakini watanzania mlianzisha mirija ya kienyeji na mliizoe vibaya sana.
Chauchau,tuzungumze,usiwe na wasi,zungumza basi,wewe subiri ,utaona kama hongo au rushwa lakini misamiati ya mirija,tumia kidogo zinazobaki weka kando.
Na hii shida iliyopo ni ya muda na ndio nikasema kwa kuandika tuvumilie, ni suala litakalopita ,infrastructure inayoanza kuboreka itaongeza maendeleo kwa wananchi wa Tanzania nzima zikiwemo nchi za jirani nazo zitafaidika.