Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Wandugu,

Mtakumbuka kuwa wakati zoezi la uhakiki vyeti linaanza, wengi tulitoa maoni tangu awali ya kuwa hili suala halina tija kwa sasa zaidi litaleta uhasama baina ya makundi ya wenye mamlaka na wasio na mamlaka. Wakabisha badala yake wakaongeza kasi zaidi. Watumishi wengi hasa wa kada ya chini wameishi kwa mashaka na hofu kuu kipindi hiki huku wengine wakitumbuliwa hadahrani na wengine wakiwekwa viporo.

Ni hofu kila mahali mori ya kazi imeshuka kila kona ya nchi. Hili likiendelea, yakaibuka kwa kasi sana madai ya kugushi umri na jina la Mwigulu Nchemba hadi alipojitokeza mwenyewe kujibu japo ni kama alichochea moto zaidi kwani alichojibu kiliibua maswali zaidi ambayo hayana majibu hadi leo hii. Hili halijaisha, zikawepo fununu kuwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda anatumia jina lisilo lake bali la mtangazji wa kituo cha radio huko Tabora Ndugu Paul Christian.

Uvumi huu umekolezwa zaidi baada ya kuona kujikanganya kwa majibu alipohojiwa huyo anayedaiwa kutoa cheti cha form four kwa Bwana Daud ambaye ilibidi alazimike kujiita Paul ili kwenda samabamba na jina la mtoa cheti. Umma wa Watanzania ulitegea kuwa Bwana Paul Makonda atajitokeza na kujibu tuhuma hizi kwa uwazi na kupokea maswali kisha kuyajibu, lakini hili halijafanyika.

Sasa hoja iliyopo na ndicho wananchi wengi wanjiuliza, ikiwa watumishi wengi wametumbuliwa hadharani kwa madai ya kughushi vyeti, iweje Paul Makonda aendelee kudunda tu katika ofisi kuu ya umma kama Mkuu wa Mkoa? Utawala bora unahitaji huyu bwana awekwe kando kisha uchunguzi ufanyike na majibu ya uchunguzi huo yawekwe hadharani. Hakuna aliye juu ya sheria.

Serikali yetu sikivu ina kigugumizi gani kumweka kando Ndugu Paul Makonda?

Karibuni kwa michango.
 
hawezi kumtumbua kwasabab hata yeye kafoji PhD (kwa madai ya Ben). Yaangalie tu yalivyokuwa yanabihave yalivyokuwa wanamtumbua Wilson Kabwe yani waziwazi ilionyesha hawa watu ni vilazer.
 
Kwenye Utawala Wala Serikali Haitakuwa Na Kigugumizi Nimeshangaa Na Kucheka Sana
*Kigugumizi Kimetoka Wapi
Wameonewa Sana Watu Wa Kada NYINGINE Huyu Jamaa @Anatucheka Kwa Dharau Tu
 
Wandugu,

Mtakumbuka kuwa wakati zoezi la uhakiki vyeti linaanza, wengi tulitoa maoni tangu awali ya kuwa hili suala halina tija kwa sasa zaidi litaleta uhasama baina ya makundi ya wenye mamlaka na wasio na mamlaka. Wakabisha badala yake wakaongeza kasi zaidi. Watumishi wengi hasa wa kada ya chini wameishi kwa mashaka na hofu kuu kipindi hiki huku wengine wakitumbuliwa hadahrani na wengine wakiwekwa viporo.

Ni hofu kila mahali mori ya kazi imeshuka kila kona ya nchi. Hili likiendelea, yakaibuka kwa kasi sana madai ya kugushi umri na jina la Mwigulu Nchemba hadi alipojitokeza mwenyewe kujibu japo ni kama alichochea moto zaidi kwani alichojibu kiliibua maswali zaidi ambayo hayana majibu hadi leo hii. Hili halijaisha, zikawepo fununu kuwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda anatumia jina lisilo lake bali la mtangazji wa kituo cha radio huko Tabora Ndugu Paul Christian.

Uvumi huu umekolezwa zaidi baada ya kuona kujikanganya kwa majibu alipohojiwa huyo anayedaiwa kutoa cheti cha form four kwa Bwana Daud ambaye ilibidi alazimike kujiita Paul ili kwenda samabamba na jina la mtoa cheti. Umma wa Watanzania ulitegea kuwa Bwana Paul Makonda atajitokeza na kujibu tuhuma hizi kwa uwazi na kupokea maswali kisha kuyajibu, lakini hili halijafanyika.

Sasa hoja iliyopo na ndicho wananchi wengi wanjiuliza, ikiwa watumishi wengi wametumbuliwa hadharani kwa madai ya kughushi vyeti, iweje Paul Makonda aendelee kudunda tu katika ofisi kuu ya umma kama Mkuu wa Mkoa? Utawala bora unahitaji huyu bwana awekwe kando kisha uchunguzi ufanyike na majibu ya uchunguzi huo yawekwe hadharani. Hakuna aliye juu ya sheria.

Serikali yetu sikivu ina kigugumizi gani kumweka kando Ndugu Paul Makonda?

Karibuni kwa michango.

- Kwani Rais Magufuli alimteua RC lini kwamba hakupata muda wa kuhakiki vyeti vyake? Katiba inasema ni Rais tu lazima awe na angalau Degree moja wengine haisemi kitu hata darasa la Saba anaweza, cha msingi ni nyinyi kumfikisha RC mahakamani kuwa amefoji vyeti ama sivyo mnatupigia kelele za kitoto sana

le Mutuz
 
Hao Watumishi Wengine Waliohakikiwa Mbona Wameonewa Jamaa
Mamlaka Iliyomteua Iombe Vyeti Vya Daudi Bashite Makonda Paul Christian Makonda

Najiuliza Imeshindikana Kumpata Yule Mtangazaji Wa Tabora Ukweli Uwe Wazi
 
Japo sijasoma ulichopovika, nahisi wewe pia ni mnufaika wa madawa.
 
Haina haja ya kupiga makelele mkoa Dar ni mkubwa mkuu anaangalia kwasasa nani anaweza kufaa ingawa karata inamuangukia mkuu wa wilaya ya kinondoni tumpe muda kidogo atafanya mabadiliko muda wowote kuanzia sasa ingawa kumtoa madereva kwake ngumu kumeza ila hana jinsi kufoji cheti ni jambo la aibu na linapaswa kukemewa vikali.
 
- Kwani Rais Magufuli alimteua RC lini kwamba hakupata muda wa kuhakiki vyeti vyake? Katiba inasema ni Rais tu lazima awe na angalau Degree moja wengine haisemi kitu hata darasa la Saba anaweza, cha msingi ni nyinyi kumfikisha RC mahakamani kuwa amefoji vyeti ama sivyo mnatupigia kelele za kitoto sana

le Mutuz

Babu ishu si kiwango cha elimu bali ni uhalali wa vyeti, mbona ni somo jepesi tu hilo, "KUGUSHI VYETI NDIYO MJADALA ULIOPO MEZANI"
 
- Safi sana kagushi vyeti mna uhakika si mtangulie mahakamani au Social MEdia ndiyo mahakama ya Tanzania? hahahahahahahha

le Mutuz
 
Wanabodi,
Declaration of interest. Mimi Paskali Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo wa kufanya investigative story kuhusu jambo looted, ila nimeamua kujikita kwenye kuandika developmental news only zenye maslahi kwa taifa, hivyo hii hoja kwenye uzi huu haina maslahi yoyote kwa taifa hivyo siifanyii uchunguzi, ila ina maslahi kwa usafi wa mtu, truthfulness na the audacity kunyooshea watu vidole kumbe. ..

Uwongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli.

Kuna tuhuma za wanafunzi waliokuwa vibonde darasani wakafeli, kisha wakachukua majina ya vipanga wakaendelea na masomo na hatimaye kufanikiwa.

Tuhuma kama hii ilianzia kwa Mae. Dr. Hamisi Kigwangala akaikanusha. Jina la Said Nassor Bogoile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla?

Kisha ikaja kwa Mhe. Mwigulu Nchemba naye akaikanusha,

Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina

sasa tuhuma kama hii imeibukia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito

Jee kuna ukweli wowote juu ya hili au ni wivu tuu na wazushi wanaomuonea kijicho kijana kuwa the 2i/c (two I .C) baada ya top, hivyo wanamzushia na kumzulia ili kutaka kumshusha? !.

Jee tuhuma hii iliwahi kukanushwa?. Tuhuma ikitolewa isipo kanushwa, hata kama ni kwa ku ignore tuu, inamaanisha ni silence which means yes!.

Hii kitu inaweza kuwa kweli?!.
Nauliza tuu! .
NB.Kwa msio jua uteuzi wa mtu kuwa RC hauhitaji sifa wala vigezo, hivyo hata kama mtu aliishia darasa la 7 anaweza kuwa RC mzuri teu, au mtu aliyepata Div 0 anaweza kuwa kiongozi mzuri kuliko Ph.D holder, hivyo bandiko hili has nothing to do with u RC wa Makonda, it has to usafi binafsi wa kiongozi if honestly and truthfulness ni miongoni mwa sifa za kiongozi bora. Hii inaitwa
Academic Dishonesty , kwa mtumishi wa umma ni serious allegation
Paskali.

- Cha msingi kama mna ushahidi mngemshitaki RC Mahakamani kuliko kuhangaika namna hii inasikitisha, yaani badala ya kuongelea njia za kupambana na madawa ya kulevya sasa ni vyeti? huzuni sana hii

le Mutuz
 
- Kwani Rais Magufuli alimteua RC lini kwamba hakupata muda wa kuhakiki vyeti vyake? Katiba inasema ni Rais tu lazima awe na angalau Degree moja wengine haisemi kitu hata darasa la Saba anaweza, cha msingi ni nyinyi kumfikisha RC mahakamani kuwa amefoji vyeti ama sivyo mnatupigia kelele za kitoto sana

le Mutuz
Naona umeibuka toka mafichoni, mmejiandaa lakini? angalia usije kumkimbia mtu hapa. Haya sasa tuleteeni cheti tu cha form four cha huyo Bwana anayewalipa kumtetea.
 
Back
Top Bottom