Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Kwa nini waandishi wa habari wasiligeuze hili suala la Paul Makonda kuwa ni habari ya kiuchunguzi ili kutoa uhakika ama kukanusha tuhuma dhidi ya Makonda kwamba kaghushi cheti? Shule alizosoma zimeshatajwa, mwaka aliozaliwa umejulikana, kwa nini waandishi wa habari wasiende kwenye hizo shule na kutafuta wale waliosoma mwaka mmoja na Makonda na kuulizia ili kuupata ukweli?

Ina maana darasa zima alilosoma Makonda wakati akiwa darasa la saba wanafunzi wake wote hawajulikani walipo? Kwa nini jambo dogo kama hili waandishi wa habari wanaliachia hadi linakuzwa na kuwa jambo kubwa bila ya sababu za msingi?

Hii ni Vita ya Wote hivyo nadhani hata Wewe pia unaweza ukayafanya yote hayo na hatimaye Waandishi wa Habari hao hao wakakusifu kwa juhudi zako na ukasifika na kujulikana Tanzania nzima. Na bahati nzuri sana siku hizi kwa jinsi tasnia ya Uandishi wa Habari ilivyokuwa kuna kitu kinaitwa Citizen Journalism ambayo hata kama huna a,b,c's za Journalism still unaweza kuleta Habari na ikauzika vile vile. Najiandaa sasa na Mimi kuona Investigative Report yako juu ya hicho ulichowataka Waandishi wa Habari wakifanye, kila la kheri.
 
Kitendo cha kamanda SIRRO kumuacha Makonda akitamalaki na vyeti Feki hapa Dasalaam inaonyesha kiongozi wa kanda Maalum anapwaya.

Makonda aliwahi kuhoji utendajikazi wa kamanda Siro kuwa haukizi viwango. nimeanza kuamini,kelele zetu zote hizi na inteligensia zake ameshindwa kufungua jarada la uchunguzi dhidi ya Daudi Bashite! only in Tanzania.

Forgery is a criminal offence in the eyes of the law Kamanda Siro!
 
Hakuna cha maana hata kimoja ambacho hao wapiga kelele wake wanacho , zaidi ni upepo kama upepo mwingine na utaisha, maisha yataendelea.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya sakata la Mwigulu na lile la David Bashite. Mwigulu (kwa maelezo yaliyotolewa) alirudia darasa na kutumia jina la mtu mwingine wakati akirudia. Utaratibu kama huo huko nyuma ulikuwepo sana; yaani watu walikuwa wanafeli halafu wanaenda kurudia kwenye shule nyingine. Kuna taarifa Profesa Muhongo alirudia mara saba kabla ya kufaulu! Kujaribu kuleta issue za akina Madelu hapa ni kumpa faraja ya muda tu Bashite!

Tuhuma zinazomkabili Bashite ni kwamba alifeli kidato cha nne (alipata ziro), akachukua (kununua?) vyeti vya mtu mwingine ndio akaingilia katika chuo cha uvuvi Mwanza na kuendelea hadi kuwa bosi wa chipukizi ya chama chetu, DC Kinondoni na sasa RC Dar es Salaam! Mkuu hapa kuna kesi ya jinai ambayo mtu akipatikana na hatia, na mahakama ikafanya kazi kama JPM anavyotaka zifanye, Bashite anakula mvua saba mapema tu. Yaani kiuhalisia wakati wewe unaleta andiko lako hapa Bashite alitakiwa awe anamalizia kuandika maelezo polisi tayari kwa kufikishwa kortini kujibu jinai nyingi ambazo ziko ndani ya sakata hilo!
Umejibu vyema sana.mkuu
 
Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.
Mbowe na yeye kafoji cheti eeeeeh?
 
Kwahiyo mwizi wa n'gombe na mwizi wa mbuzi ni tofauti?
 
Kwani watumishi wa serikali walikuwa wanasakamwa? Makonda toa ufafanuzi juu ya elimu yako umalize mjadala OVA
 
Mwigulu alishaeza hapa kwamba yeye alirudia shule ndo akapewa jina la mtu aliyeacha shule akafanyia mtihani na akafaulu. Tofauti na huyu Bashite anayedaiwa kufeli kisha kanunua cheti cha mtu aliyefaulu mtihani huo ulomshinda kaifanya yake. Kagushi cheti. Kugushi cheti cha mtu ni kosa la jinai. Kuhusu Kigwangala sina maelezo ya kina.
Na tulimwelewa sijui huyu mwenzetu hakuelewa nini hapo
 
Kiukweli RC kimemponza madawa mpaka watu wanamuandama ivo ila asingejiusisha kisingeskika kitu

Na watanzania wanafata upepo
 
Wauza madawa na vibaraka wao ndio wapo kazini kumshughulikia Makonda. Yaani naomba kwa Mungu Mashetani baradhuli mauaji haya yashindwe na hila zao.
Hapa usichanganye issue ya madawa na kughushi vyeti.
Kama ni kugushi vyeti hili jambo lilikuwepo kitambo kwa viongozi wengine nadhani wakati huo Makonda alikuwa bado mwanafunzi.
Swala la kugushi vyeti lilimgharimu mbunge wa Temeke somebody Kihiyo kupoteza ubunge wake sio hilo tu alitokea bwana mmoja aliyetoa orodha ya vigogo kadhaa serikalini wakiwemo mawaziri waliotuhumiwa kuwa vyeti vyenye walakini.
Na hivi majuzi elimu ya Mwigulu na kingwangwala ilihojiwa,na hatujasikia swala hilo likihusishwa na madawa ya kulevya, sasa inakuwaje vyeti vya Makonda vinapohojiwa inaingizwa issue ya mihadarati,ilhali sasa hivi imeshateuliwa mamlaka yakushughulikia madawa ya kulevya chini ya Bw.Sianga na si Makonda tena.
 
Wapendwa, bila ya kupoteza muda ningependa tuwekane sawa kwa kile kinachoendelea kugonga vichwa vya habari ndani na nje ya jamhuri yetu tukufu ya Tanzania.

Binafsi nimekuwa nikijiuliza maswali ambayo huwa nakosa jibu la moja kwa moja kuhusu mashambulizi ya maneno yanayoelekezwa kwa mkuu wa mkoa wa dsm, je, tatizo ni kuwataja watu wanaojihusisha na unga? Au kuwa na elimu ya kuunga unga?

Pia inawezekana ni mbinu inayotumiwa na watanzania kuichallenge serikali ya awamu ya tano kupitia makonda? Vile vile ikawa ni ugumu wa maisha uliopitiliza siku za karibuni kwa watanzania walio wengi? Nauliza! Ni IPI sababi hasa ya kisakamwa bwana Paul makonda.

Mwisho ni matumaini yangu kuwa humu jukwaani kuna watu wanaoweza kuja na majibu mazuri juu ya hili na uchambuzi uliotukuka, karibuni.
Kifupi Mimi binafsi namuona kwangu kama mfano wa kuigwa na vijana wengi na kwa upande wangu nitamhesabu kama shujaa wangu ninaepaswa kuiga na kujifunza kutoka kwake sabbu.
Alianguka Mara kadhaa. Lakini hakukata tamaa aliinuka na kujifuta vumbi na kuendelea kutafuta njia yake ya mafanikio.!!
Hakupelekwa English medium na wazazi wake kama hawa wanafiki wanaojificha kwenye keyboard na kumkashifu kwa faida ya mabwana zao.! Alifeli Mara kadhaa lakini hakukata tamaa. Alipiga moyo konde na kuendelea mbele..
Hatimaye akaangukia mikononi mwa mzee Samweli Sitta R.I.P katika harakati za kuipigani ndoto yake.!!
Leo tunamuona kama mkuu wa mkoa wenye changamoto kuliko yote Tanzania mkoa wenye wakazi wengi kuliko Zanzibar! Akiwa no mkuu wa mkoa kijana kuliko wote bila shaka walio wahi ongoza jiji hilo pia labda hata kwa Nchi nzima.
Kwangu ni mfano bora wa kuigwa hata ile kuthubutu tu kuwasha moto wa kupambana na wauza madawa ya kulevya...
Tunajua kwa nguvu yao ya kishetani wanaweza washawishi watu kadhaa wakatoa kila aina ya kashfa.
Hatutasahau aina hii ya watu walifanya nini kwa Amina Chifupa alipoanzisha vita hii R.I.P.
Kwa kumnukuu makonda mwenyewe alisema" ni heri niwe mkuu wa mkoa hata kwa siku tano tu. Lakini kesho mbinguni niwe na jibu kwa dhamana niliyopewa."!
Mashetani hawa wanaweza kushinda kwa kumshawishi Rais kwa hoja zao lakini ukweli ni kuwa hawataweza kamwe kufuta historia ya Kijana huyu kwa ujasiri wake na jambo alilothubutu kulifanya kwa Nchi hii.
 
Kuna neno mleta mada umelitumia lakini sina hakika kama umelitendea haki; Kum-BLACKMAIL Rais? Hebu fafanua ulimaanisha nini?
 
Kitendo cha kamanda SIRO Kumuacha Makonda akitamalaki na vyeti Feki hapa Dasalaam inaonyesha kiongozi wa kanda Maalum anapwaya.

Makonda aliwahi kuhoji utendajikazi wa kamanda Siro kuwa haukizi viwango. nimeanza kuamini,kelele zetu zote hizi na inteligensia zake ameshindwa kufungua jarada la uchunguzi dhidi ya Daudi Bashite! only in Tanzania.

forgery is a criminal offence in the eyes of the law Kamanda Siro!
Unafiki japo ni biashara nzuri Ila huwa una mwisho na Mara nyingi mwisho wake ni aibu,!! Itendee haki nafsi yako mkuu kwa kuwa mkweli japo kidogo tu.
 
Umeuuliza jambo jema.

Makonda kagusa ngome ya madawa ya kulevya, ndivyo inaonyesha nchi hii wengi wanategemea pesa kupitia madawa hayo. Inasikitisha, watajaribu sana ila wananchi wengine tunajua ni blah blah kumchafua tu.
Kagusa ngome au kavuruga, harafu uongozi wake unaonekana wa nguvu zisizo na maarifa, ningekuwa mimi ningemrudisha shuleni akajifunze uongozi. Kupitia chuo cha magereza kwa hili kosa la kununua cheti, uongozi wake unamapungufu makubwa kiasi cha kuharibu vita ya dawa za kujevya mwrnyewe.
 
Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.
Drug dealer usiwatanie.
Wana Jamvi nimekuwa nikiangalia na kuona MAWE anayotupiwa RC Makonda kuhusu madai yanayohusu uhalali wa MAJINA na ELIMU yake.

Ninapoandika hivi sisemi Makonda hana mapungufu katika maamuzi na utendaji wake hasa wa juzi juzi, hata hivyo tukiangalia upande mwingine wa SARAFU yaonekana kuna ZAIDI ya CHETI, bali ni kutaka huyu RC afukuzwe kazi, ili WENGINE WAFURAHI.

Kwanza kabisa PROFILE ya Makonda ILIVUJWA maksudi kwa sababu ya watu walio na SABABU zao mbaya ili aonekane mbele ya Mwajiri wake ambaye ni rais kwamba yeye ni MHALIFU mkuu.

Na hivyo KUJARIBU kum influence mwajiri wake indirectly kutumia BLACKMAIL ili AMFUKUZE kazi.

Jambo hili limeendelea kwa muda sasa. Swali langu wanajamvi. Kabla ya kumtupia mawe turudi NYUMA.Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa na issue kama hii, mbona ya Makonda kila mtu ANAMTUPIA MAWE?

Ni vizuri tusiwe na DOUBLE STANDARD katika kutoa haki bali tuwe FAIR/na USAWA. bila WIVU, UBAGUZI , na FITINA. Kama Waziri Mwigulu Nchemba HAKUJIUZURU basi TUMWACHE Makonda afanye kazi. Yeye si mkamilifu mara nyingi AMEJIKWAA je hilo ndo tumpe mob justice wampige mawe. ASIYE na DHAMBI na awe wa Kwanza kutupa JIWE!
 
Kifupi Mimi binafsi namuona kwangu kama mfano wa kuigwa na vijana wengi na kwa upande wangu nitamhesabu kama shujaa wangu ninaepaswa kuiga na kujifunza kutoka kwake sabbu.
Alianguka Mara kadhaa. Lakini hakukata tamaa aliinuka na kujifuta vumbi na kuendelea kutafuta njia yake ya mafanikio.!!
Hakupelekwa English medium na wazazi wake kama hawa wanafiki wanaojificha kwenye keyboard na kumkashifu kwa faida ya mabwana zao.! Alifeli Mara kadhaa lakini hakukata tamaa. Alipiga moyo konde na kuendelea mbele..
Hatimaye akaangukia mikononi mwa mzee Samweli Sitta R.I.P katika harakati za kuipigani ndoto yake.!!
Leo tunamuona kama mkuu wa mkoa wenye changamoto kuliko yote Tanzania mkoa wenye wakazi wengi kuliko Zanzibar! Akiwa no mkuu wa mkoa kijana kuliko wote bila shaka walio wahi ongoza jiji hilo pia labda hata kwa Nchi nzima.
Kwangu ni mfano bora wa kuigwa hata ile kuthubutu tu kuwasha moto wa kupambana na wauza madawa ya kulevya...
Tunajua kwa nguvu yao ya kishetani wanaweza washawishi watu kadhaa wakatoa kila aina ya kashfa.
Hatutasahau aina hii ya watu walifanya nini kwa Amina Chifupa alipoanzisha vita hii R.I.P.
Kwa kumnukuu makonda mwenyewe alisema" ni heri niwe mkuu wa mkoa hata kwa siku tano tu. Lakini kesho mbinguni niwe na jibu kwa dhamana niliyopewa."!
Mashetani hawa wanaweza kushinda kwa kumshawishi Rais kwa hoja zao lakini ukweli ni kuwa hawataweza kamwe kufuta historia ya Kijana huyu kwa ujasiri wake na jambo alilothubutu kulifanya kwa Nchi hii.
Asante mkuu umeongea ukweli mtupu. Kuongezea hapo kuna msemo wa wahenga "kuteneza si kuanguka"
 
Back
Top Bottom