Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Vita ya madawa ya kulevya imefeli kabla ya kuanza.
'Kwasababu inatunufaisha kifedha na tunapenda vijana wetu waendelee kuangamia kwa kupata HIV,TB Homa ya ini na hata mgonjwa ya akili kwa madawa ya kulevya kwa UJINGA wetu'
 
Paskal Mayala tupige vita madawa ya kulevya vijana wetu wanaangamia.Paul Makonda amepuliza tarumbeta kitu ambacho viongozi wengi kimewashinda.

Najua kila mmoja atatafuta taarifa za Makonda ili mradi tu ziwe ni za kumkatisha tamaa na hii ni tabia ambayo tumekuwa nayo sana watanzania pale anapojitokeza MTU kugusa maslahi yao.

Biashara hii INA mtandao mkubwa ndani na nje ya Serikali na wengi wakubwa hawajapenda pale Makonda alipolianzisha.

Kuhusu majina hilo ni personal Sina comment labda wenye taarifa.ila kwangu si la msingi sana maana hata Mimi najua kuna watu wengi tu wamesoma na majina ya watu wengine miaka ya nyuma ilikuwa kama kawaida toka primary.

La msingi kwangu mimi ni hii vita ya madawa ya kulevya lazima tupigame wote na tu support juhudi za Makonda na sio kuanza kuzizima kwa namna yoyote ile.





Usikimbilie kujificha chini ya "kivuli cha madawa ya kulevya" kama yule aliyejisalimisha jeshini na kuugeuza ufisadi wake kuwa "kombora la masafa marefu" ili usihojiwe.Hoja ya kuwa dogo anatumia jina feki ilishajadiliwa hapa jukwaani hata kabla hajapewa "kandarasi" ya kupambana na washindani wa GSM kibiashara.

Ajitokeze hadharani akiwa na vyeti halisi na atuthibitishie kuwa ni jina lake halisi,kukimbilia kuwasingizia wauza dawa kuwa ndiyo wanaomchafua hakutasaidia kuuficha Ukweli unaochomoza katikati ya uwongo na hadaa za kujilimbikizia sifa.
 
Mnamtetea Makonda kwa maslahi ya nani? Taifa hili limejaa wajinga, kama kuna taarifa kwamba Makonda alifeli na kununua cheti/jina kwa nini visiachiwe vyombo husika vichunguze? kama serikali imesimamisha mambo mengi tu kwa madai kuwa inafanya ukaguzi wa uhalali wa vyeti na ajira hewa, kwanini ishindwe kufanyia kazi taarifa kama hizi? Kelele alizopiga dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya hazipaswi kuwa defence kwake asichunguzwe. Sio ajabu yale ambayo anayafanya ni matokeo ya hicho kinachodaiwa sasa!
Hatetewi MTU hapa kama kuna MTU ana makosa na sheria ifuate mkondo wake.

Tunachosisitiza hapa ni watu kudidimiza juhudi za Makonda dhidi ya vita ya madawa ya kulevya wakati tumekuwa tu kulalamika kila siku hapa kuwa Serikali na Viongozi wake hakuna wanachofanya ktk Kudhibiti biashara hii haramu.

Sasa Makonda kapiga tarumbeta kidogo tu basi kelele kila kona as if hii biashara ni halali.Nasema tena Makonda amefanya sawa kabisa hasa kutaja majina naona sasa wenyewe mmeamka na kuanza kujitetea kila kona.

Hatuwezi kuacha Taifa linaangalia na vijana wanaziti kuchanganyikiwa mitaani kwa sababu ya madawa ya kulevya then tuwe kimya tu.

Kama Makonda kuna shida na majina yake au vyeti vyake Mamlaka zipo za kushughulika na hayo.
 
Usikimbilie kujificha chini ya "kivuli cha madawa ya kulevya" kama yule aliyejisalimisha jeshini na kuugeuza ufisadi wake kuwa "kombora la masafa marefu" ili usihojiwe.Hoja ya kuwa dogo anatumia jina feki ilishajadiliwa hapa jukwaani hata kabla hajapewa "kandarasi" ya kupambana na washindani wa GSM kibiashara.

Ajitokeze hadharani akiwa na vyeti halisi na atuthibitishie kuwa ni jina lake halisi,kukimbilia kuwasingizia wauza dawa kuwa ndiyo wanaomchafua hakutasaidia kuuficha Ukweli unaochomoza katikati ya uwongo na hadaa za kujilimbikizia sifa.
Kama wewe una ukweli si uweke hapa maana hata mtoa mada ametoa kama rumors tu.

Tuwekeeni huo ukweli mnaoufahamu kuhusu majina ya Makonda na wengine tufahamu.

Otherwise yatakuwa ni maneno ya wavaa khanga uswahili siku ya kumtoa mwali.
 
hawezi kujibu mpaka amtafute mwenye vyeti wampe pesa nyingi ndiyo aje kukanusha ndivyo siasa ya Tanzania ilivyokuwa, ukumbuke kuwa Daud Albert ni mshauri namba moja wa mkulu kwa sasa.
Nakuhakikishia hakuna kitakachobadilika, na wala ukweli halisi hautaweza kujulikana. Kama ulivyosema, mwenye cheti halisi atafumbwa mdomo, jinsi wabongo walivyo hata baraza la nanihii.... vinapokaa nanihii.... halisi pale karibu na tbc bamaga nalo wanaweza wakaingiza madudu yao ukasikia mwenye cheti halisi yy ndio feki,mwenye feki ndio halisi
 
Wanabodi,
Uwongo ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. ...

Jee tuhuma hii iliwahi kukanushwa?. Tuhuma ikitolewa isipo kanushwa, hata kama ni kwa ku ignore tuu, inamaanisha ni silence which means yes!.

Hii kitu inaweza kuwa kweli?!.
Nauliza tuu! .

Paskali.

Mkuu Paskali, wewe ni mwandishi nguri, kiasi tulitegemea uandike ukweli, badala yake nawe unabandika uvumi, au una lako jambo!

Yawezekana uvumi huo ukawa ukweli au uwongo. Vyovyote vile, wanaodai kuwa wamiliki halali wa hayo majina, kama wako hai wajitokeze hadharani wao wenyewe na ushahidi usiopingika. Kama ni marehemu, ndugu zao, ikiwa ni pamoja na wazazi wao wajitokeze hadharani.

Jana Makonda amepigiwa kelele ati anawaaibisha watu kuwataja bila ushahidi, iweje leo atajwe kutumia jina lisilo lake bila ushahidi!

Kwa nini tumehamasika kutumia mitandao, kwa ID feki, kutoa taarifa zisizo na uhakika?

Sheria ya mitandao itekelezwe ipasavyo, ili tuishi kwa kuheshimiana.
 
'Kwasababu inatunufaisha kifedha na tunapenda vijana wetu waendelee kuangamia kwa kupata HIV,TB Homa ya ini na hata mgonjwa ya akili kwa madawa ya kulevya kwa UJINGA wetu'
Inakunufaisha wewe na nani.we mtu anakula na kulala na watuhumiwa wa unga na utakatishaji fedha unategemea atakuwa na lengo thabiti la kupambana nayo.we kwa akili zako ukajua kabisa makonda ana nia njema ya kupambana na dawa za kulevya?,ile ilikuwa ni maigizo tu.we biashara ya madawa unaijua lakini?
 
Ni kweli mkuu Albert makonda anatumia jina feki, lakini mkulu aliyemteua ni vigumu aruhusu uchunguzi huru, hili sakata lingekuwa kama South Africa au kenya kwa watu wasiopenda kudanganywa wangeanika Ukweli wote lakini Tanzania wapo busy na Manji hawataki kuangalia vinginevyo hata msumbiji watanzania wanabakwa na kuuawa waziri Mahiga anamtetea Mzungu mwekezaji ni Aibu.
Anika ukweli wewe unaoujua.......
 
Jamani kama vp tuleteeni huku tumjue huyu anaeombewa mapepo yamtoke na yule mwenye chopa
 
Waswahili wanasema ukiwatawanya siafu basi ujue namna ya kuvua suruali.....
 
tehe tehe tehe wacha niende insta
Mr Daudi bwana
 
Back
Top Bottom