Masai wa Town
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 7,009
- 25,406
Tafadhali husika na kichwa cha uzi huu.
NSSF Wamekuja na mbinu mpya zifuatazo ili kuhakikisha wanufaika hawapati hela zao:
NSSF Wamekuja na mbinu mpya zifuatazo ili kuhakikisha wanufaika hawapati hela zao:
- Hawajatangaza mahali popote kwamba fao la Kujitoa limerejeshwa licha ya fao hilo kurejeshwa tangu mwaka jana Disemba. Hata mnufaika akienda ofisini kufungua madai, watamhadaa ajaze ile option ya zamani kupata 33%
- Kwenye NSSF portal, option ya fao la Kujitoa imewekwa ila imefichwa sana ili watu wasiione.
- Kwenye section ya personal details Kuna kipengele cha kujaza email, kile kipengele kimelokiwa hivyo haimruhusu mnufaika kujaza email wala kuendelea na next section kwa sababu kuna kinyota.
- Mbinu ya kimafya zaidi ni ile ya kusingizia kwamba kuna maboresho yanaendelea kwenye tovuti na portal hivyo maombi yote ya madai yamesitishwa. Hili swala si la kweli kwa sababu ni muda mrefu sana umepita tangu watangaza maboresho hayo. Ninavyoandika uzi huu, NSSF portal haifunguki hivyo hakuna mnufaika ataweza kutuma wala kuona maendeleo ya ombi lake la madai ya mafao.
- Kitengo cha Mawasiliano huduma kwa wateja Hawapokei simu wala kujibu email za wateja. Ukienda ofisini kwao majibu ni "mfumo upo kwenye matengenezo". Ukiwauliza matengenezo yatakamilika lini hawana jibu.