HOJA Baada ya Fao la Kujitoa Kurejeshwa kisheria, Serikali imekuja na Mbinu mpya za Kuzuia Wanufaika Wasipate Mafao Yao

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wala hamna haja ya PM. Nakwambia hapa hapa, wala sio mbinu ya siri.
Jitie uchizi.
Kivipi?
Jipange, kama inawezekana kesho au keshokutwa, uende tena hizo ofisi za NSSF. Ukifika hapo kama kawaida nenda dirishani kafuatilie suala lako, wakitoa majibu yasiyoeleweka tena au kuleta dharau, waambie hutoki hapo ofisini kwao hadi tupate suluhu ya hili suala lako hivyo utalala hapo. Tia presha hapo na uwe tayari kugoma kutoka hapo wakati wanafunga ofisi, hata wakikuitia security na/au polisi, uwe tayari kwa lolote hata kulala lock up. Ukitia hiyo amsha amsha hapo, nakuahidi kuwa ndani ya masaa 48 (siku 2), mafao yako yatasoma kwenye akaunti, labda uwe na kikwazo kikubwa.
Nakuambia hivi kwa uzoefu, mzee wangu alipigwa mizungusho mwaka mzima, siku hiyo nikawa nipo likizo nikaenda kumcheki, akawa analalamika kuwa mafao yake bado. Nikamwambia mzee nikupe mbinu utakua tayari? Akaniambia nakusikiliza mwanangu. Nikampa mchongo mzima. Akasema mimi niko tayari mwanajeshi wangu. Asubuhi yake tukashindilia chai nzito na kiporo matumbo yakajaa vizuri, mzee hata hakumwambia bi mkubwa kuhusu hii plan ya kimafia, tulipiga kimya kimya. Tukabeba na maji makubwa. Tukatimba NSSF ofisi ya Iringa pale. Kaenda kuulizia, wakamzungusha pale na majibu yasiyoeleweka, wanamwambia arudi baada ya wiki tatu. Akawaambia sasa jamani nimekuja hapa nipo na mwanangu, humu ndani leo hatutoki mkifunga ofisi mtatuacha humu, hadi tupate suluhisho la hili suala. Nikaenda pale dirishani alipokua, kwanza tukazuia yule staff aliekua anamu attend pale asihudumie mtu mwingine lisaa lizima, baadae tukasogea pembeni pale tukasema hatutoki leo humu, kaa pale muda wa kufunga watu wote wameisha tukasema tuambieni suala hili linaisha lini? Wakatutishia polisi, tukawaambia waiteni tu..... Meneja akaja pale anauliza shida nini? Akaelezewa pale, anawauliza wenzake why hadi leo hajalipwa mzee? Hakuna majibu ya kueleweka. Yule meneja akatusihi sana, akasema anaomba hilo suala alifuatilie mwenyewe, na kwamba ndani ya siku 2 mzee atapata mafao labda kuwe na ishu kubwa sana. Baada ya kutusihi sana na kuahidi, tukasepa kwa hiyo ahadi kuwa ndani ya siku 2 mzigo utasoma, na tukamwambia meneja mzigo usiposoma, siku ya tatu tutakuja tena na tutalala hapo ofisini. Tukasepa, hapo tayari kumi na mbili jioni.
Kesho yake tu jioni mida ya saa 10 jioni, muamala ukasoma.
Mzee alifurahi sana, akaniambia kweli wewe jembe mwanangu.
Masai wa Town
Watu kwenye hizi ofisi huwa ni ******* sana, Sasa wanamzungusha mtu mwaka mzima kitu cha masaa kadhaa tu.

Hii mbinu inafaa kabisa kwa watumishi wanaojiona Miungu watu.

Tunajua NSSF mnapita humu acheni kutesa watu.
 
Niliwahi kuamsha kama hivi mahali aaah chap tu. Kipimo kikijaa kifuatacho kama sio mlipuko basi mfumuko!😀
 
Niliweka alama za vidole tangu mwezi wa tatu
Kama ulipata kazi serikalini na ukawadanganya huna ajira kuna namna huwa wanafuatilia kubaini..so nahisi wewe ni miongoni mwa mliodanganya,kuna uzi flani ulisema umepata kazi serikalini.
 
Mwanangu watu wengi wanadai mkoani ndo inakua haraka sana kuliko dsm kwa sababu dsm watu ni wengi kuliko mkoa sijajua wewe ni sababu gan zimefanya ichukue muda wote huo
Huyo jamaa mzushi yuko pssf tayari,nahisi nssf wamelibaini hilo ndio maana wamempiga spana.
 
Kama ulipata kazi serikalini na ukawadanganya huna ajira kuna namna huwa wanafuatilia kubaini..so nahisi wewe ni miongoni mwa mliodanganya,kuna uzi flani ulisema umepata kazi serikalini.
Hivi Kuna ubaya gani.mtu akitoka sekta binafsi akaingia serikalini na akaamua kuchukua Hela zake nssf.?
Mbona ni mifuko miwili tofauti.
Kwanini mtu asichukue Hela zake na kuanza upya.yaani kwanini mtu Hela ni zake alafu unamkatazia wakati ni michango yake na bosi wake wa zamani?
 
Sheria zao walizoziweka zinasema mpaka mtu afikishe miaka 55 ndio achukue pesa zake eti.
 
Tafadhali husika na kichwa cha uzi huu.

NSSF Wamekuja na mbinu mpya zifuatazo ili kuhakikisha wanufaika hawapati hela zao:
  1. Hawajatangaza mahali popote kwamba fao la Kujitoa limerejeshwa licha ya fao hilo kurejeshwa tangu mwaka jana Disemba. Hata mnufaika akienda ofisini kufungua madai, watamhadaa ajaze ile option ya zamani kupata 33%
  2. Kwenye NSSF portal, option ya fao la Kujitoa imewekwa ila imefichwa sana ili watu wasiione.
  3. Kwenye section ya personal details Kuna kipengele cha kujaza email, kile kipengele kimelokiwa hivyo haimruhusu mnufaika kujaza email wala kuendelea na next section kwa sababu kuna kinyota.
  4. Mbinu ya kimafya zaidi ni ile ya kusingizia kwamba kuna maboresho yanaendelea kwenye tovuti na portal hivyo maombi yote ya madai yamesitishwa. Hili swala si la kweli kwa sababu ni muda mrefu sana umepita tangu watangaza maboresho hayo. Ninavyoandika uzi huu, NSSF portal haifunguki hivyo hakuna mnufaika ataweza kutuma wala kuona maendeleo ya ombi lake la madai ya mafao.
  5. Kitengo cha Mawasiliano huduma kwa wateja Hawapokei simu wala kujibu email za wateja. Ukienda ofisini kwao majibu ni "mfumo upo kwenye matengenezo". Ukiwauliza matengenezo yatakamilika lini hawana jibu.
Hili nchi kwa kweli itazalisha waasi hivi karibuni. Kupuuzwa kwa wananchi kumezidi; Uwajibikaji hakuna kabisa; Dharau kwenye ofisi za umma zimezidi na mamlaka za juu hazichukui hatua. Haiwezekani wala haingii akilini, pesa ni yangu na nililipa kodi wakati nafanya kazi lakini After termination of contract sipatiwi akiba zangu NSSF. Sasa Nini maana ya Mfuko wa hifadhi ya jamii?

Attachments

  • Cam.png
    Cam.png
    336.1 KB · Views: 6
Sheria zao walizoziweka zinasema mpaka mtu afikishe miaka 55 ndio achukue pesa zake eti.
Unamuwekeaje mtu wa sekta binafsi sheria hyo.wakati muda wowote mkataba inaisha au anafukuzwa kazi?
PESA zangu hata nikichukua nikazitumia vibaya kwani nitawadai tena?.
Hyo sheria Kwa watu wa serikali ni sawa sio sisi ambao Kuna wowote unatimuliwa
 
Kama ulipata kazi serikalini na ukawadanganya huna ajira kuna namna huwa wanafuatilia kubaini..so nahisi wewe ni miongoni mwa mliodanganya,kuna uzi flani ulisema umepata kazi serikalini.
Hapana Mkuu, sina kazi
 
Mkuu kama hutojali naomba unitag kwenye hiyo post nikaone ulichoandika huenda kikanisaidia maana na mm ni mhanga pia
Hii ndiyo ile janja janja niligusia juzi kuwa imejaa kwenye zile taasis za kifedha/bank kwenye fixed deposits,hati fungani etc
 
Back
Top Bottom