Hivi ni kwa mujibu wa dhehebu lako mnavyoyafahamu na kuyafafanua maandiko matakatifu, Roho wa Mungu tunayeamini ndiye mwalimu mwenye kuongoza na "msemesha ndimi" za kanisa, anao utajiri makubwa wa karama, anampa huyu utambuzi na kumfumbia mwingine, yote ni kwa sifa na utukufu wa Mungu, kabla ya madhehebu yenu, kanisa katoliki lipo likifafanua maandiko kwa maongozi ya Roho wa Milele, kwa mamlaka yake kanisa linatumia vyanzo 3 vya ualimu wake, navyo ni 1. Biblia takatifu (holy scriptures) 2. Mapokeo hai (holy traditions) 3. Mamlaka funzi (magisterium). Mambo haya matatu yanatumika kwa pamoja kufafanua na kufundisha jambo moja pasipo kupingana, hivyo kila andiko ktk biblia linafundishwa kadiri ya mapokeo ya kale ya kanisa na mamlaka fundishi za kanisa linavyolipokea kupitia mababa watakatifu, makardinali na maaskofu wanavyoangaziwa na Roho wa Mungu. Kwa mfano, jambo la vitabu vya biblia takatifu, wakatoliki wanatumia biblia ya vitabu 72 tofauti na madhehebu mengine yanayotumia biblia ya vitabu 66, walioamua kupunguza vitabu 6 walikua na sababu zao na kanisa haliendeshwi kwa kusikiliza wapinzani wake wanasema nini, linamsikiliza Mungu, hivyo likaendelea na mambo yake, kwa upungufu huo wa vitabu kadhaa ktk biblia yenu, kuna taarifa nyingi mnazokosa na hivyo hatuwezi kuelewa kanisa linalofundisha kwa biblia yenye taarifa nyingi zaidi ya mlizokuwa nazo. Uhalali wa kanisa kutumia mapokeo yake upo hata ktk biblia mliyokua nayo ninyi, itoshe kusema kati ya mwaka 295BK biblia ilipoanza kutumia ktk kanisa wakati huo likiwa kanisa moja tu katoliki la mitume, Mwenyezi Mungu amefunua na kufundisha mambo mengi kwa njia zake ktk kanisa ambayo hayakuwa yameandikwa, kuna nyakati watakatifu walioko mbinguni wametokea ktk kanisa na kuleta jumbe za Mwenyezi Mungu akitaka jumbe hizo zitambulike kama "kweli za kiimani" na zishikwe na wafuasi wa "Mwanae mpenzi" pia kanisa ktk ukulu wa kiti cha Petro mtume, linapotimiza wajibu wake wa kufundisha Imani, maadili na ibada, linaelekeza historia ya wanadamu kadiri ya nyakati walizopo, mafundisho ya kanisa kipindi cha zama za utumwa na ukoloni ni tofauti na sasa kwenye zama za ubeberu, sayansi na teknolojia, haya yote ni kazi ya Roho mtakatifu, tajiri wa nyakati zote, kila siku anao ujumbe mpya kwa ajili yako ya leo na kesho pia atakua na lingine kwa ajili yako kama utamsikiliza na kumpa muda akufundishe, anafanya hivyo kwa kanisa, taifa na jamii inayompa nafasi alifundishe. Je, unampa Roho mtakatifu nafasi ktk maisha yako? Je, familia yako? Jamii? Kanisa lako? Kama kweli, basi lazima utakua unashuhudia surprise nyingi kutoka kwake, akikuelekeza jinsi ya kumjua, kumpenda na kumtumikia Mwenyezi Mungu ili mwisho mwishoni uweze kufika kwake mbinguni.
Nimefurahi kupata fursa hii kuandika kitu kuhusu Imani kuu hata hivyo yako mengi, karibu kanisa lenye misingi ya mitume, iliyotabiriwa kuwa misingi ya ulimwengu huu itapambana nayo lakini haitalishinda, mfano swali la kuombea marehemu, kwetu hata mtoto wangu wa miaka saba anayefuata mafundisho ya komunyo yakwanza analifahamu na kulieleza kinaga ubaga, wakati huko kwenu hata mchungaji mwenye PhD ya teolojia hajui chochote, hivyo ndivyo anavyoshangaza Roho mtakatifu ktk maweza yake.
Barikiwa.
ulitakiwa kuandika kwa kuweka aya, huo ndio uandishi wa wasomi. najua wewe ni msomi, na ninakuheshimu kwa hilo.
tukija kwenye hoja, Kama uliwahi kusoma Biblia hata mara moja tu, utakubaliana na mimi kwamba kanisa lako katoliki linapingana na wokovu aliouleta Yesu Kristo, na karama zote za Roho Mtakatifu. In fact, kanisa lako linamkataa Roho Mtakatifu, kwasababu hata ujazo wa Roho Mtakatifu ambao kanisa la kwanza (kitabu cha matendo) waliishi, ninyi mnakataa na hakuna yeyote kanisani mwenu hadi makao makuu vatican wanakoataka kuruhusu ushoga, ambao wanajazwa Roho Mtakatifu, hivyo usimsingizie Roho kwamba mnaye au kwamba anawaongoza.
Nitakufafanulia machache halafu ujiulize mwenyewe na ukasaidiane na wenzako wasomi kujibu.
1. Kanisa la kwanza, lile la mitume, hawajawahi kuomba kwa bikira maria, never, ila ninyi je?
2. Kanisa la kwanza walihubiri watu waokoke kwa kumwamini Yesu Kristo, na wajazwe Roho Mtakatifu, je, nini mnahubiri watu waokoke? mbona mnasema kunena kwa lugha ambako ndio kujazwa Roho haitakiwi? mbona hata karismatic wanaojaribu kupambania wokovu mnawafukuza na kuwatenga?
3. Kanisa la kwanza, hawajawahi kuomba kwa wafu, waliomba kwa Jina la Yesu Kristo, ninyi mnaomba kwa wafu, hata juzi mliomba kwa magufuli na mlimwombea.
4. Kanisa lq kwanza liliamini mtu anatakiwa kuokoka na kuacha dhambi, baada ya kifo ni hukumu na mtu anapokufa anaenda na matendo yake, ninyi mnaamini mtu akifa padre anaweza kumwombea msamaha kwa Mungu akasamehewa. hii ni ajabu kabisa. Kitabu cha Ufunuo anasema "Heri wafu wafao katika Bwana, maana matendo yao wataenda nayo", pia Waebrania inasema, kama mtu alivyoandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu. ninyi mmebadilisha kwamba mtu akifa maiti inaweza kuombewa ikasamehewa, inasamehewa ikiwa imetubu lini sasa? enyi vipofu.
5. Kanisa la kwanza liliamini matendo ya miujiza. ni kweli siku hizi kuna manabii wa uongo wengi wanafanya miujiza feki. lakini hiyo haizuii au haimaanishi miujiza halisi haipo. Ninyi, hata ukiita askofu wenu hakuna mwenye uwezo kukemea hata pepo tu, hayupo. mioyoni mwenu kuna Mungu kweli? Yesu alisema pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo...Pia Yesu alisema, enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili, aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa, na ishara hizi zitaambatana na wote waaminio, kwajina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya...., ninyi hamtaki kusema kwa lugha ya Roho, na hamtoi hata pepo kilema tu hamuwezi.
6. Kanisa la kwanza, au nisema Yesu alisema tukaihubiri injili, aaminiye na kubatizwa ataokoka. hakuna mtume au yeyote kwenye kitabu cha matendo aliyebatiza watoto wadogo, kwasababu hawawezi kuamini, ila wale wenye akili wanaoamini kwanza, na kubatizwa hao ndio wanaookoka. ninyi mnabatiza watoto wadogo, ambao hawajaamini, na hata kuokoka kwenyewe ambako Yesu alisema "ataokoka" mnakupinga. ajabu sana.
kwa hayo machache, jitafakari kama kanisa lenu hili ndilo lile lile la mitume au la. Warumi 1:26 inapinga kabisa ushoga na ufiraji, ila mnakijua mnachokifanya vatican sasaivi. okokeni muikimbie hukumu ya Mungu iliyo mbele yenu. ajabu yake ni kwamba, ninyi wenyewe mnajua fika mioyoni mwenu kwamba hamna Mungu, mnaabudu tu dini na mapokeo ya dini yenu, ila mna uhakika kabisa mioyoni mwenu kwamba hakuna Roho wala chochote cha kimungu. na wengi wa waumin iwenu wapo hapo ili wazikwe na kuombewa msamaha wakifa wakiamini kwamba wakiwa maiti watasamehewa, na huo ndio uongo mkubwa sana shetani ameuweka na unapoteza wengi jehanum.