Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
pango la kuhukumu ndio sababu kubwa mliyofungwa nayo, kuhukumu hakujumuishi kueleza ukweli, stephano alipigwa mawe hivihivi kwa kusema ukweli, akawaambia wayahudi ni wanafiki na mioyo yao haijatahiriwa kwasababu walikuwa wanapinga Neno la Mungu kama wewe. Yesu Kristo alihangaika sana na watu ambao hawataki kuambiwa ukweli kama wewe, tujipime kwenye Neno la Mungu, kama kila jambo tunalofafanuliana la kimungu lingekuwa kuhukumu basi hata kuhubiri tusingehubiri.Unaposema liko mbioni kuhalalisha ushoga hayo maono umeyaokota wapi?
Halafu nilikwambia unipe andiko linalozidi kukupa huu ujuaji wa kuhukumu wengine naona bado upo kimya, sijui unasubiri kitu gani?!
Nyie viumbe huwa mnajiona watakatifu mnaoishi hapa ulimwenguni, sijui kwanini hampai muende mbinguni kama Eliya.
ukimwona mtu anafanya dhambi, mwambie ukweli hapo umepotea, na wala haukuhumu, unamsaidia na ndio kazi Yesu alitutuma, ukimwona mtu yupo kifungoni kama ninyi mnaoabudu bikira maria na wafu ambayo ni ibada ya sanamu, hatuwezi kuwaacha bila kuwaambia ukweli. shida ni kwamba, tukijaribu kuwaambia ukweli mnakimbilia kwamba unatuhukumu,
Ezekieli 33:8 inasema, Nimwambiapo mtu mbaya ewe mtu mbaya hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo aiache njia yake, mtu mbay ahuyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
Siku ile ya pentecost, wale walioshukiwa na Roho wakiwa 120 pale gorofani, maria naye alikuwa mmoja wapo, pamoja na mitume. kuanzia pale Petro alisimama na kuhubiri akifafanua kwanini walinena kwa lugha na watu 3000 waliokoka palepale. kanisa likaanzia pale. hivyo mariam alikuwa ni muumini tu katika kanisa hilo, waliendelea kuishi na kuhubiri (though haionyeshi popote kama lijisumbua hata kuhubiri, ila wengine walifanya), hakuna sehemu maria aliwaambia waombe kwa jina lake, au waombee wafu, kina Petro na Paulo na wengine wote hawajawahi kuomba kwa wafu au kuomba kwa maria. tuwambiapo kuomba kwa wafu kama maria na ndugu zenu waliokufa, au kuwaombea wasamehewe dhambu ni kujilisha upepo na ni ibada ya sanamu, hatuwahukumu, tunawaonya kwasababu kama mtaendelea hivyo mtakuja kuangamia motoni na kama tusipowaambia damu yenu isije kudaiwa mikononi mwetu. huko sio kuhukumu.