Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA

Tupe maana yake mkuu sisi maleimani.
HUB ni kituo kikubwa cha biashara cha ngazi ya dunia nzima. Dubai alipounda shirika la ndege akahakikisha asilimia tisini ya ndege zake zinapita pale kwenye jiji lake kwa maana ya safari ya transit. Utatoka nchi za mashariki ya mbali utatua pale Dubai na kisha utaendelea na safari kuja Dar. Utatoka London na kukatiza Dubai kisha utaendelea mpaka afrika ya kusini.

Alijua kule kuonwa mara nyingi kwa jiji lake ni hatua ya kwanza ya kulitangaza kimataifa. Maofisi makubwa yamejengwa pale, biashara za kila aina zimefunguliwa pale yakiwa ni matawi ya zile zilizopo katika miji mikubwa kama Paris, New York, Vancouver na mengine maarufu, hiyo ni maana ya HUB.

Hivi sasa Dubai ameingilia kwenye biashara ya madawa ya binadamu, anageuka kuwa Medicine Hub ya dunia nzima anampita umaarufu India kwenye sekta hiyo.

Samia ana mitazamo ya kisasa sana, anapokea ushauri kutoka kwa wataalam wajanja na wenye maono mapana na anao utayari wa kuyafanyia kazi. Dar inajengewa uwezo wa kuja kuwa HUB kubwa afrika na ikiwezekana duniani.

Hawa wawekezaji wawili wanaokwenda kuendesha bandari ni hatua za mwanzo tu za kujenga umaarufu kama ule wa Dubai, kwamba wepesi wa kutoa mizigo pale bandari unakwenda kuipa heshima mpya Tanzania na inaweza kuanza kuchangamkiwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka mataifa makubwa.

Maendeleo ni mbinu za kisasa, sio kuwa na akili mgando zenye ujamaa mwingi na zinazojaa hulka za kichoyo tu. Kusema sisi wenyewe tuendeshe ni kukosa maono mapana ya kidunia, unahitaji kuwa na chombo cha kibiashara cha bandari chenye kurahisisha biashara za ukanda huu, na watu wetu watajikuta wanaboresha maisha yao katika siku zijazo.
 
sina maoni, I'm waiting to see which is witch to switch the sweet in light
 
Mahakama imeona mkataba ni mbovu maana una illegality nyingi lakini imeshindwa kuuvunja kwa vile eti umepitishwa na mhimili mwingine hivyo hauwezi kuingilia.
Sasa hilo bunge ndio sauti yetu wananchi, na wabunge hawakusikia sauti zetu bali wamesikia matumbo yao hivyo wananchi tunasema HATUTAKI.
Na serikali ijue vyombo vyetu vya dola ikiwemo wale Mabakamabaka kiapo chao cha kwanza ni KUILINDA MIPAKA YA JAMHURI YA TANZANIA, WATU WAKE NA MALI ZAKE.
Bandari na fukwe zake ni mali ya JMT watazilinda, kama kuna mtu anajidanganya kuwa kazi yao ni kuwalinda wao na ufisadi wao wanajidanganya. Watainuka siku moja
 
Pascal unataka uwazi kwenye HGA wakati wenzako ndiyo wanaenda kubadilisha Sheria ili hizo HGA zisije kabisa Bungeni? au unafikiri wanaenda kubadilisha sheria kwasababu zipi hasa?

Sasa Pascal Mayalla uo uwazi unategemea utoke wapi? maana wanataka iko kifungu kitoke kisomeke kuwa Baraza la Mawaziri ndilo litakuwa la mwisho, wakiamua hapo imetoka hiyo.
 
Uzuri Pascal Mayalla wewe ni mwanasheria na unaelewa mikataba -HGA huwa ni siri ,Je hiyo transparency itapatikana kwa njia ipi?
Kwa sheria yetu ya sasa wala haikupaswa kuwa siri cos ingeingia Bunge kwenda kufanyiwa Review, changamoto kile kifungu kinachotaka mikataba inayoingiwa na Serikali inayohusu Rasimali za Taifa wanaenda kukiondoa ili wapate uhalali kuwa ni siri.
 
We nae hii nchi ni yetu wote na ndiyo maana Katiba ya JMT 1977 ina mtaka kila Mtanzania Kulinda Rasimali za Taifa, Katiba haikutaja kuwa wanajeshi au Serikali ndiyo italinda Rasimali ila imemtaka kila mtanzania hivo ni wajibu wetu kulinda na kutetea Rasimali zetu kwa ghalama yoyote.
 
Tunataka tujue wanachukua Bandari kwa muda gani na serikali yetu itapata kiasi gani.

Pia tunataka tujue wataajiri Watanzania wangapi?
Watanzania tulishaitwa ni wezi kwahiyo hakuna nafasi, hakuna mwekezaji anaweza kumwajiri mtu mwizi.
 
Tupe maana yake mkuu sisi maleimani.
HUB ni kituo kikubwa cha biashara cha ngazi ya dunia nzima. Dubai alipounda shirika la ndege akahakikisha asilimia tisini ya ndege zake zinapita pale kwenye jiji lake kwa maana ya safari ya transit. Utatoka nchi za mashariki ya mbali utatua pale Dubai na kisha utaendelea na safari kuja Dar. Utatoka London na kukatiza Dubai kisha utaendelea mpaka afrika ya kusini.

Alijua kule kuonwa mara nyingi kwa jiji lake ni hatua ya kwanza ya kulitangaza kimataifa. Maofisi makubwa yamejengwa pale, biashara za kila aina zimefunguliwa pale yakiwa ni matawi ya zile zilizopo katika miji mikubwa kama Paris, New York, Vancouver na mengine maarufu, hiyo ni maana ya HUB.

Hivi sasa Dubai ameingilia kwenye biashara ya madawa ya binadamu, anageuka kuwa Medicine Hub ya dunia nzima anampita umaarufu India kwenye sekta hiyo.

Samia ana mitazamo ya kisasa sana, anapokea ushauri kutoka kwa wataalam wajanja na wenye maono mapana na anao utayari wa kuyafanyia kazi. Dar inajengewa uwezo wa kuja kuwa HUB kubwa afrika na ikiwezekana duniani.

Hawa wawekezaji wawili wanaokwenda kuendesha bandari ni hatua za mwanzo tu za kujenga umaarufu kama ule wa Dubai, kwamba wepesi wa kutoa mizigo pale bandari unakwenda kuipa heshima mpya Tanzania na inaweza kuanza kuchangamkiwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka mataifa makubwa.

Maendeleo ni mbinu za kisasa, sio kuwa na akili mgando zenye ujamaa mwingi na zinazojaa hulka za kichoyo tu. Kusema sisi wenyewe tuendeshe ni kukosa maono mapana ya kidunia, unahitaji kuwa na chombo cha kibiashara cha bandari chenye kurahisisha biashara za ukanda huu, na watu wetu watajikuta wanaboresha maisha yao katika siku zijazo.
Hao wanaohangaika ili nchi ipate uwekezaji ni walinda katiba kama tulivyo mimi na wewe. Tusipende kuwakwaza hovyo kwa kigezo cha kulinda katiba, tunawakwaza kwa kigezo cha uhuru wetu. Sidhani kama ikulu ya JPM ingeletewa upuuzi kama huu wa waraka ingetulia tu, JPM angemkata mtu kichwa.
 
JPM katika utawala wake aikutana na Waraka 2 za Katoriki! nani ulisikia alikatwa kichwa? hivi unapomuona Hamza Johari anakuambia sio kweli kwamba tumewapa bandari zote ila tumewapa bandari ya Dar tu ila ukienda kwenye Mkataba unasomeka ni Bandari za Maziwa na Bahari we unaona sawa?
 
Kuna wawekezaji wawili wanakuja katika sekta ya bandari, unajua ndani ya mikataba yao nini kimeandikwa?.
 
Uzuri Pascal Mayalla wewe ni mwanasheria na unaelewa mikataba -HGA huwa ni siri ,Je hiyo transparency itapatikana kwa njia ipi?
Mkuu Nehemia Kilave , ni kweli contracts nyingi zina provisions za confidentiality lakini kunapotokea jambo la public interest, hiyo public interest ina overrule confidentiality na mkataba unawekwa wazi.

Hii itasaidia kuwafunga midomo ma critics wote wa hoja za kisheria, ili wajiridhe hoja zao zimezingatiwa.
P
 
Ni zaidi ya kuingilia siasa za kiuongozi. Kuandika mikataba ni shughuli inayosomewa vyuoni tena miaka na miaka, haiandikwi tu kama barua za mapenzi.

Unaposema mkataba urudi bungeni ni sawa na kudharau taaluma mzima za wanasheria waliosomeshwa ndani ya taifa letu kwa gharama kubwa.

Mkataba unasomwa mzima kwa ukamilifu wake, ukisoma kifungu kimoja ama viwili na ukavikosoa ni kujidanganya, na ni kuingilia taaluma za watu.
 
Oneni hili jitu lilivyo la hovyo, hayo tuliyokwisha ona yametusaidia nini? Ni sawa kudai kupiga chabo mkeo ambaye bado unaishi naye baada ya kumpiga chabo akiku cheat before.
 
Utaratibu wa kisheria ufuatwe tu kama Tender itangazwe tuweke masharti yetu ataekidhi sawa
Hatuoni hizi taratibu na urasimu wake kama zinachelewesha uchumi wetu kwa ujumla, hatuwezi kuona hilo suala kwa sababu wengi wetu sio wadau wa moja kwa moja wa biashara za bandari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…