Baada ya Jeshi kumaliza kazi Oktoba 29 yafanyike haya

Baada ya Jeshi kumaliza kazi Oktoba 29 yafanyike haya

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
1. Kusitisha utawala wote wa kikatiba na kuanzisha utawala wa mpito wa kijeshi na wananchi. Zoezi hili litahusisha na kusimamisha Taasisi za TAKUKURU, TISS na majukumu yao kufanya na Idara za Ujasusi za Jeshi.

2. Kuundwa Baraza la Uongozi la Kitaifa litakaloundwa na Maofisa wa Kijeshi pamoja na Viongozi wachache wa Wananchi wasio hata na tone la kutiliwa mashaka na wananchi kuhusu kusimamia kwao haki na kupinga ufisadi.

Baraza hili litashika hatamu kuliongoza Taifa kwa kipindi kisichozidi miaka 2. Pia litatoka tangazo rasmi la kukifuta Chama cha Mapinduzi na shughuli zake zote nchini Tanzania. Mali zote za CCM zitarudishwa serikali kuu.

3. Kuundwa kwa Bunge la Wananchi litakalohusisha wawakilishi wa Wananchi na Makundi mbalimbali ya Watetezi wa Haki za Binadamu.

Bunge hili litasimamia Mchakato wa kuandaa na kupitisha Katiba Mpya iliyo bora kabisa. Katiba Mpya pamoja na masuala mengine itaweka marufuku ya Watumishi wa Umma na Serikali kujihusisha na siasa na kuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Pia katika kipindi cha Mpito Bunge hili litasimamia kuelekeza bajeti kuhusu Mapato na Matumizi ya Serikali.

4. Kuanza kwa Mchakato Mpya wa kuziunda upya Taasisi za POLISI, TISS, TAKUKURU, Ofisi ya DPP, Tume ya Uchaguzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Mahakama.

5. Kuanzisha mchakato wa kukamata na kuwafikisha Mahakamani Viongozi wote Mafisadi. Kesi zitaendeshwa kwenye Mahakama maalum itakayoendeshwa kijeshi tena kwa wazi.

6. Kuitishwa Uchaguzi Mpya chini ya Tume Mpya ya Uchaguzi iliyoundwa chini ya Katiba Mpya. Rais akipatikana utawala wa kiraia utarudi na Katiba Mpya itashika hatamu.

Masuala haya yote yatafanywa kwa kipindi kisichozidi miaka 2.
 
Nikajua unataka kuvaa bomu ukajiripue kumbe unawasaidia maandishi umechelewa sana Hilo jeshi Halina mda na maandishi ya watanzania
Kila jambo na wakati wake na kila mwanadamu ana kalama yake.

Wenye mawazo mazuri tutawasaidia kuwapa mazuri mazuri. Wenye uthubutu watatoa mchango wao kwenye uthubutu.

Kila mchango wa mwananchi kwenye kulikomboa na kuliweka sawa hili Taifa mliloliharibu kwa ufisadi wenu utathaminiwa vizuri kabisa.
 
Hahahahahahaaa
Ukiwa unaandika kama vile mtu..

Kumbe ni kijibwa kinachotumia uhuru wa kujieleza!

Ukiwa kijibwa, si vbaya kubweka ili watu wajue kuwa kuna kijibwa huko!
Endeleeni tu kutudharau.

Tutawekana sawa hiyo Oktoba 29.
 
Jeshi gani? Zile inshu huwa zinapigwa kimya kimya tena na wanajeshi wa kawaida tu.
 
TAKUKURU wanazingua na msg zao usiku wa manane

Hawa inatakiwa watiwe ndichi wote!
 
TAKUKURU wanazingua na msg zao usiku wa manane

Hawa inatakiwa watiwe ndichi wote!
Jeshi likichukua nchi tu Takukuru wote wanakuwa jobless automatically. Na wengine tunaweza kuwakamata na kuwashtaki kwa kushiriki kuliangamiaza hili Taifa kwa kuacha Viongozi wale rushwa na walibanange Taifa.
 
Back
Top Bottom