Baada ya Kashfa ya Trump, Ulaya kwa kauli moja wamuambia Zelensky your not Alone you never walk alone alipo wapo ulipo tupo simamia nchi yako

Iko hivi makubaliano hayo yalimanisha kuwa Ukraine asalimishe siraha zote za nyuklia warhead zipatazo 1900 ila tu Urusi isije ikaingilia mipaka ya Ukraine. Mwaka 2014 Urusi alikiuka makubaliano kwa kuivamia rasi ya krimea, Wala USA chuni ya Obama hawakutoa ulinzi kwa Ukraine kama sehemu ya makubaliano yao. Mwaka 2022 Urusi aliivamia Ukraine kijeshi nafikiri hili Kila moja anafamu. Sasa ululitaka Ukraine ifanye kitu Gani?
 
Kwa ufupi ulaya ni wajinga wajinga yaani if you elect idiots in political positions this is what you get. Yaani hao wanasiasa they are not on front line dying hahaha yaani hakika wajinga sana.
 
Hiya haipo,Trump atalazimika kuisaidia Ukraine ikiwa Ulaya watakuwa upende wa Ukraine.
Mkuu watanzania wengi ni wajinga wasiopenda kuelewa maana ya haki. Hawahawa wanamlaumu kagame kuivamia Congo ila walamshabikia Urusi
 
Mimi ni mvivu kuandika ila kwa kifupi ni kwamba, mwaka wa 1990 kwenda 1991 jimbo la Ukraine lilipotaka kujitegemea lilikubaliwa ila kwa masharti kwamba lazima silaha zote za nyuklia zipelekwe Moscow alafu serikali yoyote itakayokuwa inatawala nchini Ukraine inapaswa kuwa na uhusiano mzuri na Urusi, Ukraine inatakiwa iwe nyutro isishirikiane kijeshi na maadui wa Urusi.

Pia kwa kuwa Urusi na Marekani ndio walikuwa masupa pawa kwa wakati huo waliwekeana mikataba kwamba NATO isijipanue kuelekea Mashariki/yani NATO isiongeze wanachama kuikaribia Urusi

Sasa kilichopelekea haya tuyaonayo leo kilianzia pale Marekani na washirika wake walipowapiga propaganda wananchi wa Ukraine mpaka wakaanzisha maandamano ya kupinga viongozi wenye uhusiano mzuri na Urusi, wakazidi hadi rais wao akaachia madaraka na kukimbilia Urusi kitu kilichoacha mwanya maadui wa Urusi wakaanza kuvinjari Ukraine huku wakianza kuweka mikakati ya kutaka Ukraine ijiunge nato kitu ambacho ilikuwa ni kama kucheza na moto.

Mwezi wa pili mwaka 2014 rais wa Ukraine alipopinduliwa waliingia manyang'au walioandaliwa na Marekani, mwezi mmoja mbele Marekani akawa anawamwagia hela tu ili wazidi kuwa mbali na Urusi. Serikali mjini Moscow haikuvumilia sana ikatuma jeshi wakachukua rasi ya Crimea sababu wananchi wengi wa mkoa huo hawakuwa tayari kukubali serikali mpya iliyofungamana na magharibi.
Mambo yalianza kwenda hovyohovyo nchi ikaanza kugeuzwa kama chumba cha mataifa ya magharibi wakiwa wanapanga mipango ya kuja kuisambaratisha Urusi, ila Urusi ilionya tu ikaanza kuwekeza sana kwenye jeshi sababu walishajua kitakachofuata baadae.
Mambo yakawa mabaya zaidi zelensky alipochaguliwa mwaka 2019 alianza kuwatenga na kuwatesa watu wanaoongea kirusi hasa majimbo ya donbass ambayo ndio hayo yalifanya Urusi kuanzisha oparesheni mwaka 2022.

Huyu zelensky akawa anaongea ujeuri sana juu ya Urusi huku akisema anajiunga NATO kitu ambacho Marekani na Urusi walishasainishana kwamba ni mwiko!
Kujidai kote kumbe nchi yake imejazwa silaha za kila aina na hawahawa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na wengine wengi alafu waowao wakawa ni wapambe wake hadi wakawa wanampa taarifa za kiintelijensia jinsi Urusi inavyoandaa jeshi... Wakampa kiburi kwamba wapo nyuma yake na watamfanya kuwa mwanachama wa NATO.

Kilichotokea ndio kama tunavyoona leo ndio maana nasema zelensky ni mtu wa hovyo sana sababu sio rahisi Marekani aingie vita vya moja kwa moja na Urusi kisa jimbo lililokuwa sehemu ya Urusi.

Huwezi kuwa karibu na mtu mwenye nguvu alafu uwe unaficha vibaka nyumbani kwako akuache... Lazima ubutuliwe tu
 
Kila siku mnajaziana maandishi na ma link ila Ukraine ndo ishaoza.Bishaneni eeeh ila lazima mjifunze kuwajua wazungu tabia na hila zao pindi wanapohitaji jambo lao.
 
Umeandika vizuri sana from perspective ya Urusi. Asante kwa muda wako mkuu.
 
Trump anaweza kuungana na URUSI kwa mlango wa nyuma kuwakomoa ulaya
ni mawazo yangu lakini
The moment Ulaya ikiamua kusimama yenyewe kiulinzi, jambo ambalo wanaliweza vizuri, Marekani itabakia kuwa nchi ya kawaida sana. Ulaya waboreshe military spending hasa kuwa na nuclear za kutosha, mchezo watakuwa wameumaliza.
 
The moment Ulaya ikiamua kusimama yenyewe kiulinzi, jambo ambalo wanaliweza vizuri, Marekani itabakia kuwa nchi ya kawaida sana. Ulaya waboreshe military spending hasa kuwa na nuclear za kutosha, mchezo watakuwa wameumaliza.
Huo muda wa kuboresha majeshi yao haupo wanaweza kushughulikiwa nje ndani kwa kuchonganishwa na bingwa wa fitina usa
Kosa kubwa ulaya ni kukubali usa awe kiranja wao
 
Zelensky yuko sahihi.Anatetea independence and territorial integrity ya nchi yake.Wa Ukreine na ULAYA wako pamoja naye.
 
Zelensky ameishashindwa vita na Nchi imeshamegwa hao EU ni maboya waliomlaghai Zelensky na magobole ya misaada aibu inawakumba🤣🤣 lazima wajitoe kimasomaso sasa hivi Hangary anawacheka tu hao EU kwa kuangukia pua
Wewe ndio unaona ameshindwa...

Umeshachagua side ya muonevu.. issue namba Moja Russia ni kuzuka yaani kaamua tu kuchukua maeneo ya Ukraine.. Ukraine hawataki.
 
Ulaya na Marekani wamegawanyika kuhusu Ukraine?
 
Wewe Bwege kweli Trump akipeleka mabomu Israel unashangllia.
 
Mbona hamueleweki, mara russia anapigana na nchi 32, mara anapigana peke yake🤣🤣🤣🤣,
Duh! Zelensky ni noma sana, zaidi ya mwaka mzima anazichapa tu na putin.
 
The moment Ulaya ikiamua kusimama yenyewe kiulinzi, jambo ambalo wanaliweza vizuri, Marekani itabakia kuwa nchi ya kawaida sana. Ulaya waboreshe military spending hasa kuwa na nuclear za kutosha, mchezo watakuwa wameumaliza.
Unadhani vikitokea vita halisi watakua pamoja? Siku ikitokea vita vya moja kwa moja haya mataifa yatagawanyika vibaya mno!
Utashangaa ndani ya Ulaya kutatokea nchi zitakazoisaidia Urusi. Alafu haya mataifa makubwa yakiingia vitani yakizidiwa huwa yanachomoa battery 😁
 
Trump anaweza kuungana na URUSI kwa mlango wa nyuma kuwakomoa ulaya
ni mawazo yangu lakini
Trump keshaungana na Putin kwa mlango wa mbele dhidi ya EU na Ukraine siku nyingi tu kabla hata hajawa Rais. He’s a great Russian asset.

Hata kwenye uchaguzi wa Marekani 2016, Russia walifanya covert campaign kubwa mitandaoni kuhakikisha Trump anamshinda Hilary Clinton.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…