Wana JF
Sote humu tunaangaika kupata mtu sahihi wa kusaidiana na Rais SSH, huku tukitaka kitoona mabaki ya CCM ya zamani iliyokuwa Na malengo ya kujirundikia Mali huku ikilindana kiutawala na kufanya wanyonge tuwe maskini wa kutupwa kabla ya Rais Hayati JPM kuipangua na kuirudisha kwa wananchi. Vyeo vya kulindana na kurithishana vinaweza kurudi ikiwa hatutamchagua mwanamapinduzi wa kweli.
Dr. Charles Kimei amefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kibiashara ya kibenki mpaka akacha urithi mkubwa wa kimaendeleo benk aliyoiongoza ikapata mafanikio. Yeye akiwa mshauri wa mwenendo wa kiuchumi aliwahi kusahihisha makosa fulani tunayopitia akataka kuletewa zengwe kabla ya kuambiwa kanusha ili alinde ugali wake kwani alikuwa anakalibia kustaafu.
Kwa udhubutu wake kusema ukweli na makosa anayoyaona kiuchumi, na alighubikwa na serikali isiyotaka ukweli, sasa ni wakati wa CCM kumchagua akatuletee maendeleo kwani hana makundi. Sisi tunachotaka ni maendeleo dhabiti ya watu na vitu sio vitu tu huku wanyonge tukisaga Lami. Angalau tukimkosa Antoni Mataka naye anafaa, Mkoa wa Simiyu ulikuwa nyuma sana na ameunyoosha, ameonyesha diplomasia makini kwa kutatua migogoro ya wafanyakazi.