Hii nchi as long as bado iko chini ya ccm tusitegemee chochote cha maana wakuu.
Kivuko kipya hakizidi bilioni 20, hapo ilipaswa viwepo 2 vya kisasa na vipya, ajabu hivyo vilivyopo ni vya miaka 20+ iliyopita. Bilioni 20 hawana ila Bashe anajipigia zaidi ya bilioni 100 yeye peke yake. Sasa chukua mawaziri waliopo wote, makatibu wakuu, wakurugenzi wa halmashauri, wakurugenzi ama wakuu wa mashirika ama taasisi za umma,
Mwendokasi imekufa tumerudi kwenye Daladala, kivuko kimekufa kumerudi kwenye Mitumbwi, ndege zimekufa sasa tunatumia mabasi na zote hizo zinauwawa kwa idadi kubwa ya wateja. Ni Tanzania pekee hapa Duniani ambapo biashara hufa kwa sababu ya kuelemewa na idadi kubwa ya wateja. Tunasubiri treni nayo ife tukae tutulie tuangaliane.