BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Muda mfupi baada ya moto kuwaka katika Kiwanda cha GSM Industrial kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa kiwanda hicho, Salaah Mohamedi amesema wamepata hasara kubwa kutokana na moto huo uliowaka leo Jumapili Machi 13, 2022.
"Chanzo hatujui hadi sasa, nilipigiwa simu saa 12 hivi na kaka yangu Ghalib kwamba kiwandani pale panawaka moto nilifika mapema tu, bahati nzuri Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vilikuwa vimeshafika, tukapiga simu na kufanikiwa kupata magari ya kuzimia moto.
"Hatujafanya bado tathmini hatujui hasara ni kiasi gani lakini uharibifu ni mkubwa sana maana hakuna ambacho kimesalia, uharibifu ni mkubwa sana," amesema Salaah Mohamedi ambaye ni mdogo wake Ghalib Mohamed (GSM).
Pia soma > Dar: Kiwanda cha Magodoro GSM, Chawaka Moto