Baada ya kiwanda kuwaka moto GSM wasema “Tumepata hasara kubwa sana, hakuna kilichosalia"

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Muda mfupi baada ya moto kuwaka katika Kiwanda cha GSM Industrial kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa kiwanda hicho, Salaah Mohamedi amesema wamepata hasara kubwa kutokana na moto huo uliowaka leo Jumapili Machi 13, 2022.

"Chanzo hatujui hadi sasa, nilipigiwa simu saa 12 hivi na kaka yangu Ghalib kwamba kiwandani pale panawaka moto nilifika mapema tu, bahati nzuri Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vilikuwa vimeshafika, tukapiga simu na kufanikiwa kupata magari ya kuzimia moto.

"Hatujafanya bado tathmini hatujui hasara ni kiasi gani lakini uharibifu ni mkubwa sana maana hakuna ambacho kimesalia, uharibifu ni mkubwa sana," amesema Salaah Mohamedi ambaye ni mdogo wake Ghalib Mohamed (GSM).


Pia soma > Dar: Kiwanda cha Magodoro GSM, Chawaka Moto
 
Ningekuwa serikali,huu mchezo ningeuchimba mpaka nijue kiini cha yote haya.

Makonda ana matatizo yake lakini,ninaona dalili za GSM kuwa mafia sana.

Ni mtu mpumbavu pekee ambaye atahisi Makonda ndiye kachoma.Na ninajua kwa nchi hii wapumbavu ni wengi wataamini kuwa Makonda ndiye kachoma kiwanda. Hawa GSM walijua hili.

Wao hawana hasara kwa sababu watalipwa mabilioni na bima.

Ila watu kama hawa,ni wabaya sana maana wanaonesha hawadhibitiki.

Na kitendo cha wao kujiingiza yanga,basi watanzania tutaona kila aina ya ushenzi kutoka kwa watu hawa.
 
"Tajiri kuingia kwenye Ufalme wa Mungu ni sawa na ngamia mzima kupenye kwenye tundu la Sindano ya kushonea nguo"

Tafakari kwa makini.
Wewe maskini unaweza kuthibitisha utafika mbinguni?
 
Zimamoto wametekeleza kazi yao ya kuja kupooza majivu tusiwalaumu kwa kushindwa kuzima Moto wakati hawana vifaa wabunge wanaokula tu posho kila kikao hata wakisinzia bungeni lakin zima Moto hakuna vifaa vya kutosha magari ni mabovu mnoo hayawez kukaa na mzigo mkubwa wa maji muda wote tairi zitapasuka maana zimechakaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…