Huu ujinga na upumbavu wa kutengenezwa ili kutawaliwa na kufanywa watumwa kiurahisi miaka ile, umebakia Afrika tu.
Wenzetu wa mabara mengine vikiwemo vizazi vya waliotengeneza dini hizi wameachana na upumbavu huu miaka mingi sana, hali iliyopelekea nchi zao na wananchi wao kupiga hatua kielimu na kimikakati ya maisha. Wenzetu waliacha ujinga wa kutegemea miujiza kujipatia kipato, badala yake walijikita katika elimu, kufanya kaz kwa bidii na wengine kujikita katika biashara zilizowaletea mafanikio makubwa.
Afrika ni bara la giza na la hovyo katika ulimwe mzima. Ndiomaan kila takataka za kiimani, magonjwa na vita vinaletwa huku, na sisi tunavipokea na kufurahia ujinga huo.