Ntopo Kilebente
Senior Member
- Apr 3, 2021
- 191
- 248
Kindly go to bed.
Afu iyo pic ni wewe ama umejiongeza Ili sisi kina Karucee tupitage tukikukonyeza?
Mbona unanifukuza, wacha nikule lecture ya kulea, mtoto asiwe kama Junior, konyeza tuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kindly go to bed.
Afu iyo pic ni wewe ama umejiongeza Ili sisi kina Karucee tupitage tukikukonyeza?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kina junior wana balaa mzaz ukifilisika
Kina junior wana balaa mzaz ukifilisika
Nadhani haujamuelewaHaya maisha haya unaweza ukalea mtoto hivyo baadaye linakuja kuwa tofauti.
Lea mtoto vizuri wala asipitie shida ambazo umepita kwasasa mazingira ni tofauti na tuliyokulia wengi.
Mazingira ya sasa ni mazingira ya kisasa tofauti na awamu za ujima.
Kikubwa ni kumpa stadi za maisha na sio kumpa mikazi migumu mpaka mtoto akuchukue kisa unataka kumpitisha njia uliopita.
Tutajikuta tunatengeneza kizazi cha watu wenye roho mbaya kama Magufuli , na baadaye ndio wanakuja kuwa Marais wanaanza kuwapitisha wananchi kwenye magumu kisa wao walipitia magumu.
Nadhani haujamuelewa
Hata kufua nguo zake baadhi ni kazi ngumu..
Mwisho wa siku watoto hasa wa kiume ni lazima umtengeneze kiume
Mkuu ni wapi nimeandika mtoto analelewa ili akiwa mkubwa lazima awe unavyotaka??Haya maisha haya unaweza ukalea mtoto hivyo baadaye linakuja kuwa tofauti.
Lea mtoto vizuri wala asipitie shida ambazo umepita kwasasa mazingira ni tofauti na tuliyokulia wengi.
Mazingira ya sasa ni mazingira ya kisasa tofauti na awamu za ujima.
Kikubwa ni kumpa stadi za maisha na sio kumpa mikazi migumu mpaka mtoto akuchukue kisa unataka kumpitisha njia uliopita.
Bado sijutii uamuzi nliofanya,
Hapo awali mtoto nlikuwa namlea kimayai huku nikijioa moyo sitaki apitie shida nlizopitia kumbe nlikuwa navuka mipaka kabisa ambayo haikuwa vema kwa mtoto,
Nikabadili malezi na kweli dhana yangu ya kutotaka mtoto asipate ahida nlizopitia nliendelea nayo ila iliishia tu kuhakikisha mtoto anapata chakula, anavaa, anapata elimu, n.k na sio kuvuka mipaka.
Schoolbus nliacha kulipia maana shule ipo karibu tu kutembea ni dakika 25, kuna wenzake wanaosoma shule za kata hutembea masaa sasa mimi nikaona kwani huyu ni kilema hadi asitembee??
anajifulia,,, Zamani lilikuwa jukum la haus gel ila nikaona huu upuuzi tu, kwani mikono yake imevunjika?? mama yake alisema namtesa ila nikamkumbusha adha atayopata mtoto endapo asipokua na msaada.
anapalilia bustani ndogo .
, anafyeka nyasi (sio ombi)...Saizi silipi mtubaje kufyeka,
kutandika kitanda,...Ashazoea kabisa,
kufagia uwanja ... Hapa saus gel nae kapunguza mzigo
Zamani mchana mama yake alipendelea kumwekea ratiba apikiwe wali au chips, nikaona hayo ndio ni mapenzi ya mama hasa ukiangalia uwezo wa kumudu hivi vitu upo lakini kama baba niliingilia kati hii ishu, Saizi mchana ni ugali kwa kwenda mbele nimempiga marufuku house girl kumpikia wali au chips, Saizi ni ugali tu na hii ni kwa faida ya mtoto.
Kucheza nje na wenzake,..ni haki yake, tatizo wazazibwenye uwezo huwa tunawaona watotot wetu ni kama malaika wasicheze nje na wenzao, Nlikuwa namfungia ndani nikamnunulia Playstation kuchezea game na kuangalia katuni ila kiukweli maisha halisi sio katuni bali ni watu, japo kwa tahadhari.
Shule kwangu nataka mtoto awe na uwezo kawaida tu, kipimo changu huwa ni wastani, yeye hushika nafasi ya tano kati ya wanafunzi 30 na mimi wala sina shida kabisa, sina mambo ya kuhakikisha anashika nafasi gani, ilimradi ana wastani unaoridhisha wala sina shida, ila huo wastani asipoufikia hata awe wa kwanza hapo nina shida.
Huu ni mwaka wa pili nadhani tangu nibadili style ya malezi na sijaona anakosa chochote zaidi ya kupata vingi zaidi.
Ushauri wangu kwa wazazi wenzangu ni kwamba wazazi wenye uwezo msitumie visingizio vya sitaki mwanangu aishi shida nlizopitia huku mkivuka mpaka huo na kutengeneza mtoto ambae ni mayai mayai.
hata maua ukiyamwagilia sana maji mizizi yake huwa mifupi maana maji yapo tele ila mvua kali au upepo mkali ukipita maua yanatoka kwasababu mizizi haijaenda chini kutafuta maji kama maua yanayomwagiwa wastani tu yenye mizizi mirefu inayotafuta maji yaliyo chini hata mvua kali au upepo mkali ukipita mizizi inashikilia ua halitoki.
Ni mimi yule yule mkuuToa credit kwa mleta uzi. Haya ni marudio.
Mods unganisheni na original thread.
Tuna hela ya kula tu mkuuBasi leo kila mwenye tusenti atajitokeza.
Wakaka mnajitahidigi sana mpate fursa ya kujimwambafy.
Hata wewe sky soldier ni wa kutufanyia hivyo?
😀😀😀Kina Junior wanabembelezwaga kula hao, wakati enzi zetu unabanwa pua, uchague kufa kwa kukosa hewa au uchanue mdomo chakula kipite.
Hali ya kiusalama ya zamani sio sawa na sasa,hiyo ni moja ya sababu kuu.Mambo mengine yanashangaza. Nikiwa nasoma chekechea mzazi alikuwa anakupeleka shule wiki ya kwanza tu, ukishika njia shule unaenda mwenyewe. Na hapo unavuka barabara ama na kimto
Lakini Hawa kina Junior hata Kama shule ipo nyuma ya nyumba mzazi unamfata na kumrudisha, Mtoto hajifunzi kujitegemea kabisa.
Watoto wa huku kwetu kwa mpalange miaka 12 anaendesha bajaji na shule ameacha