Baada ya kuacha kumlea mwanangu kimayai, nimeona akiimarika

Mambo mengine yanashangaza. Nikiwa nasoma chekechea mzazi alikuwa anakupeleka shule wiki ya kwanza tu, ukishika njia shule unaenda mwenyewe. Na hapo unavuka barabara ama na kimto

Lakini Hawa kina Junior hata Kama shule ipo nyuma ya nyumba mzazi unampeleka na kumrudisha, Mtoto hajifunzi kujitegemea kabisa.
 
Nadhani haujamuelewa
Hata kufua nguo zake baadhi ni kazi ngumu..
Mwisho wa siku watoto hasa wa kiume ni lazima umtengeneze kiume
 
Mkuu ni wapi nimeandika mtoto analelewa ili akiwa mkubwa lazima awe unavyotaka??

Nadhani hata mtoto huna au elimu ya malezi huna kabisa.

Malezi ni elimu pana sana, kasome vitabu vya malezi au nyuzi za humu ndani.

Ila huyi wangu ngoja nikomae nae, kuna baadhi ya vitu tayari anavijua ambavyo wenzake shuleni hawajui kabisa kama nlivyovitaja,

Unajua hata kuandika barua ya posa mkuu ?? 😁😁
 

nitakuja kusoma uzi huuu
 
Hali ya kiusalama ya zamani sio sawa na sasa,hiyo ni moja ya sababu kuu.
 
Malezi ya mtoto ni issue ya kubalance tu,

Usimpe sana raha wala asipate tabu sana,kikubwa awe na uwezo wa kuishi kwenye hali zote mbili,

Kama tunavyojua kua life is very short,ni lazima mtoto umuandae kuishi maisha hata kama Mungu atakuchukua,

Usimpe mtoto kila akitakacho wala usimnyime kila akitakacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…