Baada ya kuacha kumlea mwanangu kimayai, nimeona akiimarika

Mkuu wewe kama baba ukizembea kwenye malezi ya mtoto hasa wa kiume jua unaandaa bomu litakalo kulipukia huko baadae.

Uko kwenye right track komaa!!
 
Siku zingine mnapotaka 'Kujimwambafai' Kwetu kutokana na kupata 'Vipesa' vyenu vya Ngama ( Kubahatisha ) msiwe mnazunguka sana katika kutaka Kututangazia kwani wengine huwa tunawashtukieni mapema tu.
Mazao ya awamu ya tano ndio Kama hivi wenyewe Kila kitu mtu anaona ana onewa na kutambishiwa [emoji3][emoji3][emoji3] pole mzee
 
Binafsi naamini mtoto kutanua kwa pesa ya Mzazi wake Ni upunguani kwani unamuharibia moral ya kupambana na kuja kujipambania kivyake.

Utakuta mzazi umenunua ki gali chako au Cha mkopo kabisa usivyo na akili unampa nae akae mbele eti akiendeshe na wewe unajikenulisha meno unazani sifa . Kiufupi unaua spirit ya mtoto wako ya kujipambania na kuifanya akili yake ilalee doro .

Ndio maana watoto wakishua wengi hata wakiachiwa urithi hawawezi kuendeleza Mali zaidi ya option ya kuuza na wakiuza wanafilisika na kubakia na sifa tu mjini kuwa walikuwa nazo sijui boni hia hia..na wengine kufikia hatua ya kuwaombea wazazi mfe ili abaki na mali [emoji23][emoji23][emoji23]na kuwaona nyie ndio mnao mchelewesha katika utajiri wake.

Lkn yote hiyo tatizo Ni mzazi mwenyewe unaandaa mabomu ya kuja kukulipua mwenyewe . Lkn ukimcholea mipaka kuwa bwana wee umeona ile gari eeee....! Basi ile gari halikuhusu komaaa uje upate la kwako kwa pesa yako na ili uweze kumiliki vitu Kama hivi unatakiwa upite hapa utokeee hapa uzamie hapa uibukie kule zaidi ya hapo ndugu utaumia maishani na hii tabia yako ya kulala Kama paka.

Sasa nyie endeleeni kuwafungia watoto wenu na washinde wanagaragara kwenye hizo sofa utafikiri vijibwa vya kizungu nawa hakikishia mkikatika gafla hao watoto wenu sijui watakaa na nani mwingine anae penda kuishi na vijibwa vya kizungu na sio watu ambao wanaweza kuamka asubuhi na kufanya usafi hata kujifulia vijinguo vyao.

Mzazi pesa Ni zako wewe ndio unajua umezipataje hivyo mjengee mwanao misingi ya kuja kuzisaka zake na sio kutegemea zako.
 
Miaka miwili anaanza kujifunza kula mwenyewe akifika mitatu tayari fundi.

Waacha..!!! Mi mbona wangu ana miaka minne na nusu saiz na bado naona analishwa kila kitu kuanzia uji mpaka chakula.?πŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈπŸ™„πŸ™„
 
Waacha..!!! Mi mbona wangu ana miaka minne na nusu saiz na bado naona analishwa kila kitu kuanzia uji mpaka chakula.?πŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈπŸ™„πŸ™„
Duh pole mama yake anamuona bado hawezi.
 
Naitikia ni vizuri sana.
Unajua watu wanafikiri watoto tutakuwa nao milele, kumbe sivyo, ataondoka kwako kwenda kujitegemea. Ajifunze vitu hivuoy ni muhimu. Naamini wengine wanaodrkeza watoto wafuate.
Nimeona kwa jursni binyi smezaa akiwa nyimbani kwa mama yske. Hajui kumtinza hata mtoto wake, smemwachia mama yake amlee mjukuu. Huyu hata akoolewa sidhani majukumu ya mke ataweza kuyamudu?
 
Inasikitisha sana

Sent from my SM-J720F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…