Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Natangulia shukrani kwa mwenye uzi kwa kututia moyo pia nina maswali machache ningeomba anisaidie:
  • shamba ameliwekea uzio?
  • umejenga nyumba yako ya kuishi kwenye shamba hilo?
  • garama za ujenzi wa nyumba yako na miundombinu ya ufugaji na mifugo na chakula cha mifugo imekugarimu kiasi gani kwa jumla?
 
Hongera sana .mi pia nalima mahindi na alizeti.nafuga nguruwe pia for the past 5 months hapo mikese.nahitaji mbegu ya kuku pia.tunaweza kushare experience through 😛jmwaikenda@gmail.com

Mkuu hongera sana,

Aina gani ya nguruwe unafuga, je ni large white au land race?
 
Natangulia shukrani kwa mwenye uzi kwa kututia moyo pia nina maswali machache ningeomba anisaidie:
  • shamba ameliwekea uzio?
  • umejenga nyumba yako ya kuishi kwenye shamba hilo?
  • garama za ujenzi wa nyumba yako na miundombinu ya ufugaji na mifugo na chakula cha mifugo imekugarimu kiasi gani kwa jumla?
. Shamba sijaliwekea Uzio mkuu. Bado nipo kwenye phase I .Katika phase hii kuna ni mradi wa kujenga mabada ya kuchukua nguruwe zaidi ya 1000. Maximum itakuwa 2,000. Phase hii itahusisha ujenzi wa mazingira ya kusaport kuku wasiopungua 40,000.

Phase II

ni ujenzi wa fance kuzungushia shamba langu lote. Hii hiyo itanichukua muda kidogo.

phase III

Ni kubadili vibanda vilivyopo na kujenga nyumba za kudumu za kuishi.

Hivyo sasa kuna nyumba ndogo ya udongo na bati anayoishi mfanyakazi wangu na mke wake. Pia kuna nyumba nyingine ya nyasi inayosubiri mtu wa kuishi. Kwa sasa Mimi naishi mjini nikitafuta pesa za kusapoti mradi kwani bado haujiendeshi. Baadaye nina mpango wa kufanya makazi huko.

Gharama za ujenzi bado napambana nazo. Ujenzi unaendelea. Bado haujakamilika.
 
. Shamba sijaliwekea Uzio mkuu. Bado nipo kwenye phase I .Katika phase hii kuna ni mradi wa kujenga mabada ya kuchukua nguruwe zaidi ya 1000. Maximum itakuwa 2,000. Phase hii itahusisha ujenzi wa mazingira ya kisaport kuku wasiopungua 40,000.

Phase II

ni ujenzi wa fance kuzungushia shamba langu lote. Hii hiyo itanichukua muda kidogo.

phase III

Ni kubadili vibanda vilivyopo na kujenga nyumba za kudumu za kuishi.

Hivyo sasa kuna nyumba ndogo ya udongo na bati anayoishi mfanyakazi wangu na mke wake. Pia kuna nyumba nyingine ya nyasi inayosubiri mtu wa kuishi. Kwa sasa Mimi naishi mjini nikitafuta pesa za kusapoti mradi kwani bado haujiendeshi. Badaye nina mpango wa kufanya makazi huk.
Mkuu naomba unieleweshe kidogo kama una uelewa wa kilimo cha mahindi na maharage,je vinastawi na unaweza kukadiria kiasi gani ya magunia kwa hekari moja?

Pili nimeona umetengeneza kisima ina maanisha upatikanaji wa maji ni mgumu?kama maji ya mito n.k
 
Mkuu hongera sana,

Aina gani ya nguruwe unafuga, je ni large white au land race?

Duh! wazee ckuwahi kujua km hawa wanyama km wana Majina! Naomba niongeze swali lauelewa hapo! Nini tofauti yao!
 
Duh! wazee ckuwahi kujua km hawa wanyama km wana Majina! Naomba niongeze swali lauelewa hapo! Nini tofauti yao!

Sio majina tu, hata koo zao ni tofauti. Ngoja nikabukue tena, nikupe tofauti ya kimaumbile ili hata kama unataka kununua basi kigezo cha kwanza kiwe umbile. Kuna masikio na idadi ya chuchu. Kuna urefu holizontally. Wajuba wasije wakakuuzia viguruwe dwarf.
 
100_4577.JPG100_4576.JPGmpwa haya ni matunda yako, nitatafuta contact zako tuongee zaidi, nilianza mwezi wa tano mwaka huu na kwa sasa wanedna vyema kabisa niliochukuwa watoto sasa ndo hao wanaingia kwa joto nategemea mwezi qwa 12 kuzalisha nguruwe sita.
 
View attachment 109444View attachment 109448mpwa haya ni matunda yako, nitatafuta contact zako tuongee zaidi, nilianza mwezi wa tano mwaka huu na kwa sasa wanedna vyema kabisa niliochukuwa watoto sasa ndo hao wanaingia kwa joto nategemea mwezi qwa 12 kuzalisha nguruwe sita.

Mpwa asante sana kwa kuthubutu. Jiandae kupanua mabanda, maana hawa jamaa wanaweza kupiga dazani kadhaa za watoto ukashindwa kuwatunza. Kama unafugia dar itakulipa sana, kuanzia piglets mpaka mbolea yake.
 
Mkuu Malila

hivi mbolea ya Noah inafaa kuzalisha bio-gas

mwenye ujuzi naomba msaada
 
Mkuu Malila

hivi mbolea ya Noah inafaa kuzalisha bio-gas

mwenye ujuzi naomba msaada

Swali zuri sana,ngoja na mimi nitafute majibu. Nitarudi na majibu toka kwa watalaam. Sikuwahi kufikiria hii kitu.
 
Mpwa asante sana kwa kuthubutu. Jiandae kupanua mabanda, maana hawa jamaa wanaweza kupiga dazani kadhaa za watoto ukashindwa kuwatunza. Kama unafugia dar itakulipa sana, kuanzia piglets mpaka mbolea yake.

nashukuru mpwa, changamoto niliyonayo kwa sasa nikupata mabanda, hapa nilipo malighafi za kujengea mabanda zipo kwa bei ya juu sana, hakuna mabanzi na kama ukifanikiwa kupata banzi linaenda kwa elfu zaba kwa moja, nipo umbali wa kilometer 1080 kutoka daresalam so soko langu nategemea kuwa mwanza maana kutoka hapa hadi mwanza ni karibia km 300
 
Mkuu Malila

hivi mbolea ya Noah inafaa kuzalisha bio-gas

mwenye ujuzi naomba msaada

Nimewauliza jamaa wa SUA, wameniambia inafaa. Ni kama samadi ya mtu. Shida ni kwamba haijazoeleka na jamii lakini tuendako itatumika hadharani bila shida sana. Tena ina-decompose haraka sana.
 
Hahaha malila bwana. Unamaanisha kuna watu wanaweza kugomea gesi ya noah? Lol.

Hongera sana kwa kilimo aisee
Nimewauliza jamaa wa SUA, wameniambia inafaa. Ni kama samadi ya mtu. Shida ni kwamba haijazoeleka na jamii lakini tuendako itatumika hadharani bila shida sana. Tena ina-decompose haraka sana.
 
Kwani banda hauwezi kujenga la miti kama nyumba za kijijini? Na unaweza kukandika pia. Nawaza tu solution ya haraka
nashukuru mpwa, changamoto niliyonayo kwa sasa nikupata mabanda, hapa nilipo malighafi za kujengea mabanda zipo kwa bei ya juu sana, hakuna mabanzi na kama ukifanikiwa kupata banzi linaenda kwa elfu zaba kwa moja, nipo umbali wa kilometer 1080 kutoka daresalam so soko langu nategemea kuwa mwanza maana kutoka hapa hadi mwanza ni karibia km 300
 
Hahaha malila bwana. Unamaanisha kuna watu wanaweza kugomea gesi ya noah? Lol.

Hongera sana kwa kilimo aisee

Bora gesi inakuwa confined ndani kwako au ktk mtungi, sasa samadi ya Noa ina nguvu sana ukitumia ktk kilimo cha mboga na matunda ya muda mfupi kama tikiti, mchicha,bamia,eggy plants kwa sababu inayeyuka haraka kuliko ya ngombe.

Sasa wenyewe wakijua,huwa wanagoma kununua,ila siku hizi hawagomi kama zamani. Halafu Noa kwa sababu yy ni omnivore halafu heavy feeder,anazalisha samadi kwa haraka sana.
 
sasa kama hukai hapo na uzio hakuna huoni bado risk ipo maana unaweza amka ukakita mifugo imeibwa au kuvamiwa na wanyama wakali?
 
sasa kama hukai hapo na uzio hakuna huoni bado risk ipo maana unaweza amka ukakita mifugo imeibwa au kuvamiwa na wanyama wakali?
Karibu uje uwaone mabaunsa wangu pale shambani. Wapo makini sana. Ninawalipa vizuri. Then ni marufuku mtu kuingia shambani kwangu bila ruhusa yangu hata kama niko mbali ni lazima nitalifiwe. Mtu hawezi kukuibia kama hakujui. Ni lazima akufahamu vizuri, afahamu milango ya mifugo yote. So u better be very careful. Katika yote mlinzi wangu number moja ni Mungu. Yeye asipolinda walindao walinda bure naam wakeshao pia wakesha bure.

Mkuu malila naendelea kukufatilia hapa. Nimevutiwa na hii aina za nguruwe na hili la mbolea ya Noah ya Dom- Moro. Hakika nitaanza kuitumia kwenye mitiki yangu.
 
Sio majina tu, hata koo zao ni tofauti. Ngoja nikabukue tena, nikupe tofauti ya kimaumbile ili hata kama unataka kununua basi kigezo cha kwanza kiwe umbile. Kuna masikio na idadi ya chuchu. Kuna urefu holizontally. Wajuba wasije wakakuuzia viguruwe dwarf.

HA HA HAAA! MKUU UMETISHA HADI KOOO!!!! NAISUBIRI KWA HAM HIYO SHULE KAKA! off topic kuna thread inahusu ufugaji wa mbuzi wa maziwa hebu tupia macho kule naamini utakuwa na neno!
 
HA HA HAAA! MKUU UMETISHA HADI KOOO!!!! NAISUBIRI KWA HAM HIYO SHULE KAKA! off topic kuna thread inahusu ufugaji wa mbuzi wa maziwa hebu tupia macho kule naamini utakuwa na neno!

Mbuzi wa maziwa nimeshawafuga, ila soko la maziwa halipo kwa sababu ya ushamba wetu.Maziwa ya mbuzi wanasema ni bora kwa viinilishe. Nyama ya mbuzi wa maziwa haijazoeleka kivile. Baada ya kuona wanasumbua sana kiafya, nikawauza wote nikaacha madume ili waboreshe kizazi cha mbuzi wa kienyeji.

Ukimwona mbuzi wa kizungu aliyekosa lishe,unaweza acha kula nyama ya mbuzi. Nikaona bora nikomae na mbuzi wa kienyeji tu kwa sasa.
 
Back
Top Bottom