Baada ya kuchoshwa na mateso ya Askari wa Maliasili, wananchi waamua kuchoma pori

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Wananchi wa Kijiji cha Rwamgasa, Wilaya ya Geita, wamechoma moto sehemu ya pori la akiba lililopo katika Kitongoji cha CCM wakipinga kile walichokiita uonevu na ukatili unaofanywa na askari wa Maliasili.

Tukio hilo limeibuka baada ya watoto wawili kukutwa porini wakiwa wamepigwa na kuporwa kuni walizokuwa wamekwenda kukata kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Wakizungumza na vyombo vya habari, wananchi hao walisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na madai ya mateso ya mara kwa mara, ikiwemo kupigwa, kujeruhiwa na kupokonywa mali zao kama vile baiskeli. Baadhi walidai hulazimika kulipa faini kubwa ili kurejeshewa vifaa vyao.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha CCM-Rwamgasa, Bahati Charles, amethibitisha kuwepo kwa matukio hayo akisema amepokea malalamiko ya mara kwa mara kuhusu ukatili unaofanywa na askari wa maliasili katika eneo hilo.

Aidha, wananchi wameiomba serikali kutenga sehemu ya pori hilo kwa ajili ya shughuli za kilimo na malisho, wakisema ongezeko la watu limepelekea uhaba wa ardhi na hivyo kulazimisha baadhi ya wakazi kuingia katika eneo la hifadhi.

Badala ya kuua polisi wanachoma moto pori?
UWA HAO POLICE - CCM WALA RUSHWA WAKUBWA
 
Hawa askari game huwa wanajiona sana kama nchi ni yao
 
Hao waliopelekwa kwenye hilo pori ni askari wa aina Gani? Ni hawahwa askari wanaolinda usalama wa raia?

Kitendo cha kubaka na kuvamia mali za watu pamoja na kuuwa binadamu hicho ni kitendo cha Askari?

kama ni ndiyo, basi wananchi kitendo cha kuchoma hilo pori mi naona wamefanya adhabu ndogo sana. Ilitakiwa wachome pamoja na hao Askari. Maana hao ni wauaji kama wauaji wengine. Upuuzi hautakiwi kupuuzwa.
 
Badala ya kuua polisi wanachoma moto pori?
UWA HAO POLICE - CCM WALA RUSHWA WAKUBWA
Desparate times call for desparate measures. Kuchoma pori ni namna ya ku-express hasira na kutokubaliana. Ndio maana katika guerila warfare huwa wanalipua madaraja ya reli na barabara, na inakubalika!
 
Poli limeonewa tu ,wekeni mitego polisi waingie kingi kundi kubwa mnawakamata manachoma wao

kingine isije ikawa hilo Poli liko kwenye hekta million 8 ziliuzwa Kwa wagaibuni
 
Badala ya kuua polisi wanachoma moto pori?
UWA HAO POLICE - CCM WALA RUSHWA WAKUBWA
Mkuu mbona unaongea kama umekatwa kichwa? Hao wananchi hawajawalalamikia askari Polisi bali askari wa uhifadhi wa msitu ambao wala hawana uhusiano wowote ule na Polisi.
Inaonekana una chuki sana na Polisi bwana mdogo
 
SIWAPENDI POLISI KWASABABU WENGI NI WAPUMBAVU WASIOJUA LOLOTE KUHUSU HAKI ZA WATU
 
Wamekufanya nini? Ulichukua hatua gani kukomesha hilo?
utachukua hatua gani zaidi ya kutoa rushwa? chukua hii unampelekea ndugu yako chakula pale oysterbay polisi. wewe huna pesa unayo ya chakula tu.... ukifika unaambiwa uweke kwenye mfuko mkubwa wa 1000/= tena unaambiwa ununue na maji ya 2000/= huo siyo wizi? kwa wiki wanakusanya maji mangapi na mifuko mingapi pale oysterbay
 
Ukiona hujaridhishwa na huduma uliyopatiwa au hujatemdewa haki toa taarifa kwa mkubwa wa huyo aliyekupa huduma mbovu, ndiyo maana kaunta zote za vituo vya polisi vina namba za viongozi wao mpaka IGP.
Kila boss ana boss wake acha unyonge na kulalamika, ni muda wa kuchukua hatua kuwarudisha kwenye mstari wote walio kengeuka
 
Back
Top Bottom